Nani wa kuwajibishwa kati ya mwalimu na wizara ya Elimu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani wa kuwajibishwa kati ya mwalimu na wizara ya Elimu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KIMBURU, Dec 17, 2011.

 1. KIMBURU

  KIMBURU JF-Expert Member

  #1
  Dec 17, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 210
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Nimesikitishwa sana na kauli ya Naibu Wazili wa Elimu kuwa wanafunzi watakaobainika kuwa hawajui kusoma na kuandika na wamefaulu kwenda sekondari, watarudishwa na kisha walimu wa shule walizotoka watawajibishwa. Pia kuhusu wanafunzi ambao majibu yao yameonekana kufanana sana wamefutiwa matokeo na pia walimu wao watawajibishwa. Wizara ilitegemea nini kuanzisha mfumo wa majibu ya kuchagua (multiple choice) kwa masomo na maswali yote? Hikujua kuwa mfumo huo unatoa mwanya mkubwa kwa wanafunzi kuigiliziana majibu? na pia haikujua kuwa mfumo huo unawawezesha hata wasiojua kusoma na kuandika kubuni majibu sahihi? Miaka 50 ya uhuru bado tunaifanyia majiribio Elimu yetu? Kwa hili naomba Rais KIQUETE awawajibishe watendaji wa wizara hii ambao wameleta mfumo huu usio na mantiki; na wanajikosha kwa kukimbilia kuwaadhibu walimu wasio na makosa.
   
 2. m

  mkulimamwema Senior Member

  #2
  Dec 18, 2011
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli wanaharibu elimu wanawatupia lawama wasoihusika, inabidi wawajibishwe, sio sahihi kuachwa bila kuwajibishwa. jamani tunipeleka wapi Tanzania yetu. Ndugu mheshimiwa(kama wanvyowaiota vinongozi) tazama kwa jicho la kesho, acha ubinafsi na ufisadi ili tanzania iweze kuendelea
   
 3. Poriposha

  Poriposha JF-Expert Member

  #3
  Dec 18, 2011
  Joined: Oct 23, 2011
  Messages: 306
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  1. Yule naiibu waziri wa elimu alikuwa head master shule niliyosoma O-Level huko mbeya alikuwa anajitahidi saaana kuhakikisha shule yake ina-perform vyema kwenye kila somo na alifanikiwa kwa kiasi flani kwani kulikuwa na mchujo kila kidato ulikuwa huwezi kwenda kidato kinachofuata bila ya kufikisha wastani wa 45 kwa masomo yote na ilikuwa si masihara ila shule ilikuja kupoteza mwelekeo baada ya kudahili wanafunzi wa kidato cha nne waliofoji matokeo ya kidato cha pili.
  2. Anapenda sana kuendeleza watu kielimu kwani pale shule huwa somesha baadhi ya mwanafunzi bure ambao famiia zao hawana uwezo wa kuwasomesha ila tu Huyo mtoto awe anamorali ya kusoma na ku-perform vizuri.
  3. Huanzisha program za masomo kusaidia wanafunzi mi nakumbuka alianzisha class program za jioni na siku nyingine tulikuwa tunalala hapo shuleni.
  But All in all HILI LA MULTIPLE CHOICE KWA MASOMO YOTE MI NALIKATAAAAAAA 100% ILA TUMSUBIRIE HUYU BWANA PHILIPO MLUGO TUONE MAKUCHA YAKE HAPO
   
Loading...