Nani wa kuwajibishwa kati ya mwalimu na wizara ya Elimu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani wa kuwajibishwa kati ya mwalimu na wizara ya Elimu?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by KIMBURU, Dec 17, 2011.

 1. KIMBURU

  KIMBURU JF-Expert Member

  #1
  Dec 17, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 210
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Nimesikitishwa sana na kauli ya Naibu Wazili wa Elimu kuwa wanafunzi watakaobainika kuwa hawajui kusoma na kuandika na wamefaulu kwenda sekondari, watarudishwa na kisha walimu wa shule walizotoka watawajibishwa.

  Pia kuhusu wanafunzi ambao majibu yao yameonekana kufanana sana wamefutiwa matokeo na pia walimu wao watawajibishwa.

  Wizara ilitegemea nini kuanzisha mfumo wa majibu ya kuchagua (multiple choice) kwa masomo na maswali yote? Hikujua kuwa mfumo huo unatoa mwanya mkubwa kwa wanafunzi kuigiliziana majibu? na pia haikujua kuwa mfumo huo unawawezesha hata wasiojua kusoma na kuandika kubuni majibu sahihi?

  Miaka 50 ya uhuru bado tunaifanyia majiribio Elimu yetu?

  Kwa hili naomba Rais KIQUETE awawajibishe watendaji wa wizara hii ambao wameleta mfumo huu usio na mantiki; na sasa wanajikosha kwa kukimbilia kuwaadhibu walimu wasio na makosa.

   
 2. d

  dada jane JF-Expert Member

  #2
  Dec 17, 2011
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Aje aadhibu hao walimu. Atapewa ukweli wake. Asidhani bado ni walimu wa mwaka 47.
   
 3. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #3
  Dec 17, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,947
  Likes Received: 1,272
  Trophy Points: 280
  mtawalaumu walimu bure, mchawi ni JK, toka alivyotukana wafanyakazi mke wangu kasema hatofundisha ila benki wa kwanza
   
 4. deojames

  deojames JF-Expert Member

  #4
  Dec 18, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 323
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  kama serikali ingekuwa imeweka mitihani ya kutoka darasa moja kwenda lingine kuwa ya muhimu bila shaka ingepunguza tatizo la wanafunzi kumaliza bila kujua kusoma. Nowdays ule mtihani wa darasa la nne uwe umefaulu au no wewe unasonga mbele, sasa hapa wanategemea nini! Dawa ni kuweka mtihani kila unapotaka kwenda darasa lingine lazima ufaulu, hili swala lingepunguza wanafunzi mambumbu na watu wangekuwa serious na elimu.
   
 5. s

  sugi JF-Expert Member

  #5
  Dec 18, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  Tatizo siasa imeingilia taaluma,ni kwamba kila mtoto anatakiwa kusoma sekondari,ki taalam si kweli maana wanafunzi wanatofautiana katika uelewa,wapo ambao sekondari kwao ni mzigo tu maana understanding capacity yao ni ndogo saana
   
Loading...