Nani wa kunyooshea kidole ukiukwaji wa maadili Tanzania

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Tanzania tuna pitia mabadiliko makubwa ya kimfumo kuanzia utamaduni wetu mpaka uongozi.

Tumeruhusu mwingiliano wa tamaduni za kigeni kuwa sehemu ya maisha yetu. Tumepoteza staraha ya kiubinadamu na kuvaa miwani ya mbao, tukiamini jamii haituoni.

Kwa juhudi kubwa ya kulinda utamaduni wetu, serikali ilitoa mwongozo wa mavazi yatakiwayo katika ofisi za umma. Waraka huo wa mavazi, ulisambazwa kote nchini. Hii ni kuonyesha jinsi gani tunavyo linda maadili ya jamii yetu.

Kwa kulijua hilo serikali iliweza kulinda mazingira ya viongozi wake kwa kuanzisha vyuo vya utumishi wa umma vyenye lengo la kuwandaa viongozi wetu katika malezi yenye kuakisi tamaduni zetu katika muonekano wa kioo cha jamii.

Nachelea kuandika haya kutokana na mwitikio mpya wa serikali katika kulinda uvunjifu ulio shamiri wa maadili ya kijamii, kwa kuwa mdau namba moja wa uvunjifu huo wa maadili.

Leo hii mavazi ya vijana yanayo ingizwa nchini na kulipiwa ushuru yana sikitisha, huwezi kujua yupi mzima na yupi kichaa, kwa kuwa wote wana hali moja kimavazi.

Vijana wanavaa nguo zilizo chanika mpaka kuonyesha maungo ya ndani, ukiuliza wanakwenda na wakati.

Hali hiyo hali kadhalika imeshababisha serikali kukurupuka katika uteuzi wa watendaji wake, wanao hakisi jamii wanayo kwenda kuiongoza.

#Ambitious za watanzania hazijulikani kwa kuwa tumeacha utamaduni wa kuwandaa wananchi kuwa nani ndani ya jamii zetu, tumepoteza umakini kama taifa, hatuna mipango ya kesho tunataka kuwa nani.

Mathalani, unaweza kuona kijana kaandaliwa kuwa model toka utoto wake, hata mavazi yake yana kuwa na mwelekeo huo. Haiwezekani leo miss aliyezoea kutembea uchi na kushindwa kuhifadhi nyeti zake awe kiongozi wa umma. Huu ni mfumo mpya kabisa katika maisha yetu, anawezaje kukemea maadili ilihali picha zake za nusu uchi zimezagaa kwenye mitandao ya kijamii.

#Uwezo mdogo wa usalama wa taifa katika kushauri aina ya viongozi wapaswao kuteuliwa. Zamani enzi za maadili, usalama ulifanya uchambuzi wa kina ili kumsaidia rais asipotee katika uteuzi wake, lakini siku hizi naona kazi hiyo kaachia rais aifanye binafsi hali inayo zua tafrani kwa wanao kwenda kuongozwa.

#Uzembe au uoga wa kitengo cha protokali na itifaki kushauri na kuelekeza wasifu wa kiongozi anaye teuliwa. Ikiwa mwenendo huu tunao kwenda nao utaachwa uende kama ulivyo kwa kuwa hapangiwi na mkimshauri ndo mnaharibu kabisa, tutegemee kushuka kwa maadili kwa kasi ya SGR.

Chama cha CCM kilikuwa na utaratibu mzuri wa kuwandaa viongozi wake, kulikuwa na chuo cha itifaki na uongozi wa umma ambao kupitia huko walizalishwa viongozi bora kama kina mama Makinda, mama Mongella, Annah Abdallah na wengineo. Utaratibu huu umepotelea wapi?

Hatuna kikwazo na uwezo wa mtu, tuna umizwa na utamaduni mpya wa uteuzi usio zingatia maadili ya kitanzania.

Katika mambo ya msingi tuliyo achiwa na waasisi wa taifa hili na kuyapa kisogo ni jinsi ya kuandaa viongozi wetu, pia kuwanyima fursa ya seminar elekezi kama mwongozo wa kazi na majukumu yao, hali hii imepelekea kukidhalilisha chama na serikali kwa watendaji wake kufanya double standard ya kiwango cha juu. Leo akisimama kiongozi akatoa kauli unapatwa na ukakasi kama kweli aliandaliwa kuwa kiongozi.

Turudi kwenye maadili, ikulu siyo sehemu ya kupeana fadhila, urais ni taasisi, wamsaidie rais ili kuepuka kadhia hii inayo jitokeza.
 
Back
Top Bottom