Nani wa kumrithi TB Joshua na kuendeleza huduma yake katika bara la wapenda miujiza na injili ya mafanikio (prosperity gospel?

mbwe

JF-Expert Member
Feb 23, 2018
503
1,000
Ukitaka upewe kazi ngumu basi upewe kazi ya kumshauri mwanamke anayesali kwa Mwamposa ,kazi yenyewe iwe ni kumshauri aachane na ibada ya Mwamposa .

Kwanza atakuona kama umechanganyikiwa .

Pia kama mlikuwa marafiki na urafiki wenu unaishia hapo hapo.
 

Aqua

JF-Expert Member
Jul 23, 2012
1,625
2,000
Amini nawaaambia, nimekaaa karibu na mchungaji mkubwa sana apa bongo, alinitaka niwe mchungaji kwakuwa aliniambia uko maisha yangu yatabadilika na kuwa tajili, nimuone yeye anaishi kifalme ingawa alikuwa fukala zaidi ya mimi, aliniaidi atanipa kanisa, hakika nawaaambia ishi ndani ya imani yako na muombe mungu kivyako, haya makanisa ni utapeli na mnatajilisha watu tuuuu.... amkeni na acheni kuibiwa kwa njia ya Ulokole na wokovu ni uwongo mtupu.
Ndugu pole kwa yaliyokukuta na kwa uliyo yagundua kwa kukaa karibu na huyo mhungaji.Lakini wewe siyo wa kwanza na utakubaliana na mimi kadri nitakavyokueleza.
NImekutana na watu ameumizwa na hao wanaojiita watumishi wa Mungu mpaka hawataki kusikia habari za Wokovu.
Lakini kabla sijaendelea kuna jambo unatakiwa ulijue
Kuna vitu viwili hapa duniani vina nguvu sana hata kumfanya mwanadamu afanye jambo ambalo linaweza kuwashangaza wengine,vitu hivyo ni
1.Imani
2.Mapenzi
Kwa sababu ya Imani mtu anaweza akafanya hata mambo ya ajabu,kwa mfano,kulishwa majani akiamini yatamponya,kupuliziwa dawa ya mbu,kuua watu wasio amini anachokiamini n.k
Kwa sababu ya mapenzi pia mtu anaweza akakosana na wazazi wake,akamuua mwenzi wake kwa sababu ya wivu wa mapenzi n.k
Nikirudi kwako
Naamini huyo mtumishi uliyeishi naye ni wale wako kwenye makanisa ambayo ni kama linamilikiwa na mtu mmoja au mtu mmoja ndiyoi mwenye maamuzi ya mwisho i.e kanisa hilo siyo taasisi kam RC,TAG etc.
Wokovu wa kweli upo ni wewe tu ulikutana na tapeli wa kiroho na hao ndiyo Biblia imewaita "Mbwa mwitu ndani ya ngozi ya kondoo".Soma tabia za mbwa mwitu kisha utajua kama wewe ni kondoo unatakiwa uwe karibu na mbwa mwitu?
Nawahurumia sana watu wanaojiita wakristo wakati hawana muda wa kusoma Neno la Mungu na kulitafakari,watapotezwa.Yesu akilijua hili alitusihi mapema akasema "Neno la Mungu na lijae kwa wingi mioyoni mwenu",please note amesema Neno la Mungu lijae mioyoni mwenu siyo vichwani au kwenye akili yenu.
Mungu pia akasema "watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa"
Je maarifa yanapatikanaje?Biblia imesema "Kumcha Mungu ndiyo chanzo cha maarifa".Kwa hiyo kwa lugha nyingine tuinaweza sema "Watu wangu wanaangamizwa kwa kutokumcha Mungu".
Matapeli wa kiroho ni wengi sana kwa sasa,tuombe uzima kuna mada Mungu akinijalia niatileta nataka "nitupe jiwe gizani".
Unaweza ukaja PM tukajadili zaidi au kama kuna issue unataka kujua,lakini matepeli kama uliokutana nao wapo,na wataendelea kuwepo na ni Mungu ameruhusu wawepo kama ishara ya siku za mwisho.Asomaye na afahamu.
Regards
Aqua
 

chihe

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
270
500
Toka lini kanisa hurithiwa na mtu .hii ndio shida ya haya makanisa ya mifukoni .kanisa ni la mungu sio la mtu sasa Joshua kafa watu kuulizana Nani atarithi kanisa huo ni ujinga mkubwa Kam kweli kanisa la tb Joshua lilikuwa la mungu Basi litadumu daima lkn km ni shetani Basi linaenda kufa soon.
 

Bengal

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
5,060
2,000
TB Joshua ni mtu aliyejitengenezea jina kubwa barani Africa kwa injili yake ya mafanikio. Aliwakamata wafanyakazi, maskini, matajiri, wafanyabiashara na wanasiasa wakubwa kabisa katika ngazi za Urais na wakuu wa upinzani.

Watu hawakulizungumza tu jina lake bali walisafiri hadi Nigeria katika kanisa lake alilolipa jina la Sinagogi kanisa la watu wote(SCOAN). Inasemekana kuna wakati watu 6 kati ya 10 ambao ungewakuta wakisafiri kuingia Nigeria walikuwa wanaenda kanisani kwake!

Watu mashuhuri walimwalika kwao pia. Mfano hapa Tanzania amewahi kufika na kukutana na JK, Magufuli, Mbowe na Lowassa.

Mpaka sasa nikiacha hii sababu ya hulka ya watu kupenda kuambiwa, kuhadiwa na kutabariwa mafanikio makubwa kwa yale wanayoyatamani sijui kwa uhakika hasa ni kitu gani kingine kilimfanya TB Joshua ambaye aliendesha huduma yake kwa mfumo wa Mwamposa na Mzee wa Upako kuwa maarufu mkubwa hivyo kiasi cha kuliteka bara zima na kuweza kuaminiwa hata na pande zilizokuwa mahasimu mara nyingine.

Huenda waliomuamini na kumhusudu wana sababu nyingine za msingi walizoshawishika nazo lakini sasa akiwa hayupo tena duniani ni nani watampa nafasi hiyo? Wale mlioko Mikocheni B kanisani kwa Getrude Rwakatare tuelezeni mambo yanavyoendelea kwa sasa tupate mwangaza.
Nampendekeza gwajboy
 

MESHACK WARIOBA

JF-Expert Member
Mar 29, 2017
901
1,000
Ukiwa masikini ukaingia haya makanisa uwezekano wa kuzidi kuwa hopeless na fukara kichwani ni mkubwa!
Most of riches on earth they never believe even the existence of God; Hii tu inatosha kukufanya ujue kwamba Ability ya Kupata mali na vitu vya dunia hii, ina utaratibu wa tofauti.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom