Kwa hisani ya Wavuti blog, na mtaarishaji na mpiga picha hiyo Dr Robert K, Naomba tujiulize nani wa kulaumiwa?? Wanasiasa wa Chama tawala na serekali yao, Wanasiasa wote, Watumishi na watendaji wa serekali au Watanzania wote kwa ujumla??
"SHULE ATAKWENDA SAA NGAPI HUYU?"
Nimeitizama picha hii nikaona sura ya matumaini iliyojaa kwa mtoto huyu ambaye inavyoelekea hana jinsi kwa sasa isipokuwa tu kuingia kwenye uchuuzi. Wakati mataifa mengine wanajitahidi kuwapa watoto wao elimu bora kutimiza haki ya mtoto ya kusoma, sisi hali ya maisha inatusukuma kuwashirikisha kwenye uchuuzi bila ya kutaka, tofauti na wenzetu wanaopelekwa kwenye biashara ya kipato kikubwa ya wazazi baada ya masomo.
Kamwe hatuendi mbali katika ujenzi wa Taifa kwa staili hii. Tuache kudanganyana bwana. Hizo nchi zilizoendelea wanathamini sana elimu kisha biashara au mashamba ya familia baada ya kutoka darasani. Hata wale matajiri wanaosomeshea watoto majumbani, walimu wakishamaliza somo ndiyo mtoto anaingia kwenye kujifunza juu ya 'family business'. Huyu kakutwa mtaani wakati wa muda wa masomo.
Jama, watoto wana haki zao na haki mojawapo ni ya Elimu! Tusiwapokonye kwa sera zetu mbovu.
"SHULE ATAKWENDA SAA NGAPI HUYU?"
Ni swali alilojiuliza Dk. Robert K. alipopiga picha hii jana Januari 14 jijini Dar Es Salaam baada ya kumwona mtoto huyu akichuuza mchicha jijini.
(picha imepigwa na Dk. Robert 'Bobby' K.)