Nani wa Kulaumiwa??

Jujuman

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2008
Messages
248
Likes
0
Points
0

Jujuman

JF-Expert Member
Joined Dec 7, 2008
248 0 0
Kwa hisani ya Wavuti blog, na mtaarishaji na mpiga picha hiyo Dr Robert K, Naomba tujiulize nani wa kulaumiwa?? Wanasiasa wa Chama tawala na serekali yao, Wanasiasa wote, Watumishi na watendaji wa serekali au Watanzania wote kwa ujumla??
"SHULE ATAKWENDA SAA NGAPI HUYU?"
Ni swali alilojiuliza Dk. Robert K. alipopiga picha hii jana Januari 14 jijini Dar Es Salaam baada ya kumwona mtoto huyu akichuuza mchicha jijini.
5855302.jpg?286
(picha imepigwa na Dk. Robert 'Bobby' K.)​

Nimeitizama picha hii nikaona sura ya matumaini iliyojaa kwa mtoto huyu ambaye inavyoelekea hana jinsi kwa sasa isipokuwa tu kuingia kwenye uchuuzi. Wakati mataifa mengine wanajitahidi kuwapa watoto wao elimu bora kutimiza haki ya mtoto ya kusoma, sisi hali ya maisha inatusukuma kuwashirikisha kwenye uchuuzi bila ya kutaka, tofauti na wenzetu wanaopelekwa kwenye biashara ya kipato kikubwa ya wazazi baada ya masomo.

Kamwe hatuendi mbali katika ujenzi wa Taifa kwa staili hii. Tuache kudanganyana bwana. Hizo nchi zilizoendelea wanathamini sana elimu kisha biashara au mashamba ya familia baada ya kutoka darasani. Hata wale matajiri wanaosomeshea watoto majumbani, walimu wakishamaliza somo ndiyo mtoto anaingia kwenye kujifunza juu ya 'family business'. Huyu kakutwa mtaani wakati wa muda wa masomo.

Jama, watoto wana haki zao na haki mojawapo ni ya Elimu! Tusiwapokonye kwa sera zetu mbovu.
 
Luteni

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Messages
2,274
Likes
10
Points
0

Luteni

JF-Expert Member
Joined Jan 9, 2010
2,274 10 0
5855302.jpg?286
(picha imepigwa na Dk. Robert 'Bobby' K.)​Nimeitizama picha hii nikaona sura ya matumaini iliyojaa kwa mtoto huyu ambaye inavyoelekea hana jinsi kwa sasa isipokuwa tu kuingia kwenye uchuuzi

Mimi nimeitazama sana picha hii naona msichana mwenye afya njema kanunua mboga kuna wageni wengi nyumbani halafu inaonekana ilikuwa wakati wa likizo shule yake haijafunguliwa.
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,740
Likes
7,522
Points
280

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,740 7,522 280
Mimi nimeitazama sana picha hii naona msichana mwenye afya njema kanunua mboga kuna wageni wengi nyumbani halafu inaonekana ilikuwa wakati wa likizo shule yake haijafunguliwa.
hata mimi nilipoangalia nilikumbuka kuuza mchicha siku za Jumamosi asubuhi kwa kujipatia pocket money! sielewi kwanini tunafikiri picha hii inasema kuwa binti alikuwa haendi shule? unless tujue kuwa ilikuwa ni kipindi cha shule ni vigumu kusema kuwa mtoto amenyimwa nafasi ya shule.
 
kimatire

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2008
Messages
367
Likes
11
Points
35

kimatire

JF-Expert Member
Joined Nov 27, 2008
367 11 35
Picha zingine hazijielezi kikamilfu kufikisha ujumbe unaopaswa kwa walengwa,Yamkini huyu binti anatoka shamba kuvuna mboga.Iweje aelezeke kwamba yuko njiani anauza na hajaenda shule?.Mbona ni kazi za kawaida tu kwa jamii zetu za dunia ya tatu kuwashirikisha watoto katika kujiongezea kipato?Tukubali ukweli kwamba watanzania walio wengi wanathamini elimu na wanajua manufaa yake pia.
 
Mamaa

New Member
Joined
Sep 27, 2007
Messages
4
Likes
0
Points
0

Mamaa

New Member
Joined Sep 27, 2007
4 0 0
hata mimi nilipoangalia nilikumbuka kuuza mchicha siku za Jumamosi asubuhi kwa kujipatia pocket money! sielewi kwanini tunafikiri picha hii inasema kuwa binti alikuwa haendi shule? unless tujue kuwa ilikuwa ni kipindi cha shule ni vigumu kusema kuwa mtoto amenyimwa nafasi ya shule.
Huyu binti anaonekana kuwa na afya njema, msafi na ana muonekano wa akili nzuri na uelewa wa kutosha. Kwa muonekano huo, na mahala alipo - inawezekana anamsaidia mama /Shangazi yake kupeleka hizo mboga ama nyumbani au Gengeni kwenye mradi wao. Hiyo haina maana kuwa hasomi shule, labda kuwe na maelezo ya ziada.
 
Ruge Opinion

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2006
Messages
1,734
Likes
337
Points
180
Age
64

Ruge Opinion

JF-Expert Member
Joined Mar 22, 2006
1,734 337 180
Huyu binti anaonekana kuwa na afya njema, msafi na ana muonekano wa akili nzuri na uelewa wa kutosha. Kwa muonekano huo, na mahala alipo - inawezekana anamsaidia mama /Shangazi yake kupeleka hizo mboga ama nyumbani au Gengeni kwenye mradi wao. Hiyo haina maana kuwa hasomi shule, labda kuwe na maelezo ya ziada.
Katika nchi zetu maskini hili swala la haki za mtoto linapaswa liangaliwe kwa namna tofauti kama wanavyoliangalia watu wa nchi tajiri. Je, huyu msichana angekuwa anatoka mtoni kuchota maji tungeoji kuhusu haki zake za kutochota maji? Huenda mama yake yuko kwenye shughuli nyingine nzito hivyo binti inabidi asaidie. Sisi tuliozaliwa vijijini kuchota maji, kutafuta kuni, kupeleka mazao sokoni ni vitu vya kawaida. Ni mchango kwa uchumi wa familia. Na shule tumekwenda na kufanya vizuri. Hakuna cha ukiukwaji wa haki hapa.
 
Forum statistics

Threads 1,191,688
Members 451,730
Posts 27,717,611