Nani wa kulaumiwa Mama au Baba???

Eng. Smasher

JF-Expert Member
Nov 13, 2010
745
0
Leo katika kucheki Mwanachi ya leo nikakuta habari nzuri isemayo MAMA AJIFUNGUA WATOTO 5! Nilifurahi sana nikasema hana haja ya kuongeza watoto wengine wametosha.
Nilipoendelea kusoma newz hii, huyu mama ni uzazi wake wa 10! Pia ameshawahi kujifungua mapacha mara 6,jumla ana watoto 20 now!!!
Hivi hili ni kosa la nani hasa Baba au Mama? Jamani 2punguze offside uwanjani!!!
 
Kimbweka

JF-Expert Member
Jul 16, 2009
8,601
2,000

Ni furaha yao
Kwa nini kuwaingilia familia yao
Maamuzi ni yao
Jibu wanalo wenyewe:A S-alert1:
 
MadameX

JF-Expert Member
Dec 27, 2009
7,812
2,000
Kosa la wote, halafu jamani already watu mna 6 pairs, why would wanna try for more!
 
Gad ONEYA

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
2,633
1,195
Wenzenu hawafanyi kwa mawazo ya namba ila utamu tu, hiyo namba inakuja yenyewe bila wao kuihesabu!
 
Kashaijabutege

JF-Expert Member
Oct 20, 2010
2,696
1,195
Okuku anazikwa lini?

Hakuna mwenye kosa. Kila mtoto na riziki yake. Hivyo ndivyo inatakiwa kuwa. Apandaye penye rutuba hupata mazao zaidi.
 
Eng. Smasher

JF-Expert Member
Nov 13, 2010
745
0
[Hakuna mwenye kosa. Kila mtoto na riziki yake. Hivyo ndivyo inatakiwa kuwa. Apandaye penye rutuba hupata mazao zaidi.[/QUOTE]

Duh! Issue ipo kwenye kuwalea mkuu, hapo naona ni kwapa mateso watoto na kuishi maisha ya taabu hapa duniani!!
 
Lizzy

JF-Expert Member
May 25, 2009
24,900
2,000
Kama wana uwezo wa kifedha sawa yao...ila kama ni maisha yakubangaiza hawawatendei haki hao watoto kabisa!
 
Eng. Smasher

JF-Expert Member
Nov 13, 2010
745
0
Kama wana uwezo wa kifedha sawa yao...ila kama ni maisha yakubangaiza hawawatendei haki hao watoto kabisa!
Huo ndo ukweli but huko kijijini kweli maisha yao yatakuwa mazuri zaidi ya kufuga ng'ombe na kilimo!!!!
MUNGU waepushe na hili balaa watoto hawa!!!
 
Baba_Enock

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
6,996
2,000
Hamna kosa - "..Zaeni mkaijaze nchi.."

Watoto ni zawadi - kutoka kwa Muumba - (right?)
 
Lizzy

JF-Expert Member
May 25, 2009
24,900
2,000
Huo ndo ukweli but huko kijijini kweli maisha yao yatakuwa mazuri zaidi ya kufuga ng'ombe na kilimo!!!!
MUNGU waepushe na hili balaa watoto hawa!!!
Kumbe wako kijijini?Labda hawajui kuna kitu kinaitwa uzazi wa mpango!
 
Eng. Smasher

JF-Expert Member
Nov 13, 2010
745
0
Hamna kosa - "..Zaeni mkaijaze nchi.."

Watoto ni zawadi - kutoka kwa Muumba - (right?)

Upo sawa Mkuu lakini unapoijaza dunia hii uangalie na Mateso watakayopata hawa watoto!!!
Hivi sehemu ya Kulala 2 cjui kama inawatosha na Msosi wa hii familia vp?? Afya ya Mama vipi??
Kweli Mama Enock unawza kruhusu apate Mateso kama haya!!
 
AMARIDONG

JF-Expert Member
Jun 24, 2010
2,502
0
Leo katika kucheki Mwanachi ya leo nikakuta habari nzuri isemayo MAMA AJIFUNGUA WATOTO 5! Nilifurahi sana nikasema hana haja ya kuongeza watoto wengine wametosha.
Nilipoendelea kusoma newz hii, huyu mama ni uzazi wake wa 10! Pia ameshawahi kujifungua mapacha mara 6,jumla ana watoto 20 now!!!
Hivi hili ni kosa la nani hasa Baba au Mama? Jamani 2punguze offside uwanjani!!!

badilisha picha yako inatisha
 
Msindima

JF-Expert Member
Mar 30, 2009
1,019

Ndugu ulisoma hii habari vizuri ukaimaliza? Hajawahi kuzaa mapacha mara sita ila uzazi wa sita ndo ilikua tena mapacha, na hana watoto 20 gazeti limesema ana watoto 13.
 
Msindima

JF-Expert Member
Mar 30, 2009
1,019
1,195
Leo katika kucheki Mwanachi ya leo nikakuta habari nzuri isemayo MAMA AJIFUNGUA WATOTO 5! Nilifurahi sana nikasema hana haja ya kuongeza watoto wengine wametosha.
Nilipoendelea kusoma newz hii, huyu mama ni uzazi wake wa 10! Pia ameshawahi kujifungua mapacha mara 6,jumla ana watoto 20 now!!!
Hivi hili ni kosa la nani hasa Baba au Mama? Jamani 2punguze offside uwanjani!!!

Mama ajifungua watoto watano Send to a friend Monday, 13 December 2010 20:47

Shija Felician, Kahama
MWANAMKE mmoja mkazi wa Kijiji cha Bulungwa kilicho wilayani Kahama amejifungua watoto watano, wakiwemo watatu wa kike na wato wanaendelea vizuri.
Mama huyo, Shija Maige, 33, ambaye anatokea Kata ya Bulungwa, amejifungua watoto hao katika uzazi wake wa kumi na mara sita kati ya hizo alijifungua watoto mapacha.

Habari zimeeleza kuwa Maige alijifungua watoto hao juzi katika kituo cha afya cha Bulungwa, lakini baadaye alihamishiwa Hospitali ya Wilaya ya Kahama kwa huduma zaidi.
Kwa mujibu wa habari hizo, mama na watoto hao wote sasa wanaendelea vizuri hospitalini hapo.
Wauguzi wa hospitali hiyo ya wilaya waliliambia gazeti hili jana kuwa mwanamke huyo alifikishwa hospitalini hapo saa 12:00 alfajiri juzi na gari la wagojwa.

Walisema gari hilo lilienda kumchukua baada ya uongozi wa kituo hicho cha afya kutoa taarifa za tukio hilo kwenye uongozi wa wilaya.
Mganga mkuu wa Wilaya ya Kahama, Leonard Subi alisema mwanamke huyo alianza kupatwa na uchungu na kuanza kujifungua akiwa nyumbani kwake.
"Baadaye familia yake ikaamua kumkimbiza kwenye kituo hicho cha afya cha Bulungwa kwa ajili ya huduma za kitaalamu," alisema Dk Subi.
Dk Subi alisema baada ya kufikishwa katika kituo hicho cha afya, wauguzi walianza kutoa huduma kabla gari hilo la wagonjwa kufika. Baada ya gari hilo kufika alihamishiwa hospitali ya wilaya.
"Jambo la kwanza alipofika, aliongezewa damu iliyopungua kutokana na harakati za kujifungua," alisema mganga huyo.

Mganga huyo alisema mama huyo alijifungua salama, lakini uzito wa watoto wake haukuwa wa kawaida.
"Uzito wao ni kuanzia kilo 1. 250 hadi kilo 1.700. Uzito huo uko chini sana kwa vile wastani mzuri wa watoto kuzaliwa hapa kwetu Tanzania ni uzito wa wastani kuanzia Kilo 2.5.

Mama huyo aliwaambia waandishi wa habari hospitalini hapo kuwa mimba hiyo aliyojifungua watoto watano ni ya kumi.
Alisema aliwahi kujifungua mapacha katika mimba ya sita na kwa uzao huo wa sasa, idadi ya watoto wake imefikia 13.
Maige alieleza kuwa ameolewa na anaishi na mume wake aliyemtaja kwa jina la Charles Marco.
Hata hivyo, ameomba msaada kutoka kwa wasamaria wema na mashirika mbalimbali ili kuweza kuwalea watoto hao.
 
Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
89,983
2,000
Kutotoa vichanga 13 ni shughuli pevu kweli kweli. Najaribu kupiga picha hiyo "mashine" yake....somethings are just better left unsaid!

We Dena jana ulikuwa wapi mi nimekutafuta siku nzima bana...
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom