Moja ya hoja zilizotolewa na kamati zilizochunguza makontena ya mchanga ni'' Uwepo wa Mikataba mibovu. '' swali linalonisumbua mimi ni:
- Sheria zetu zimepitishwa na nani?
- Je hawa watanzania wenzetu waliopewa jukumu la usimamizi je walifuata sheria zilizopo kuingia mikataba hii?
- Je Bunge, serikali pamoja na vyombo vingine vilikuwa na nafasi yeyote kuzuia uhalifu ?
- Kama mkataba ni mbovu na ulipitishwa kihalali je anayepaswa kulaumiwa ni Afisa wa serikali, serikali, mwanasheria mkuu, baraza la mawaziri au nani?
- Ikiwa hawa watu (makampuni) wamejipataia faida kutokana na hii mikataba mibovu je wakulaumiwa ni wao au ni sisi tuliokubali kusaini mikataba mibovu?
- Ikiwa ubovu wa mikataba yetu ndiyo tatizo je hao watendaji, au hizo kampuni zitakuwa na hatia?
- Je hapa tulipofikia tulaumu hawa wawekezaji au tujilaumu sisi wenyewe kwa kutokuwa makini?
- kutokana na juhudi njema za Rais je sio muda muafaka sasa kuwepo na udharura kuunda tume ya kudumu itakayo kupitia mikataba yote mikubwa ili tusiendelee kupoteza? maana mwanya huu ukiachwa kwa wengine watajitahidi kujinasua.