Nani wa kulaumiwa kwenye hili sakata la kuibiwa rasilimali zetu?

Anold

JF-Expert Member
Jul 15, 2010
1,456
614
Moja ya hoja zilizotolewa na kamati zilizochunguza makontena ya mchanga ni'' Uwepo wa Mikataba mibovu. '' swali linalonisumbua mimi ni:
  • Sheria zetu zimepitishwa na nani?
  • Je hawa watanzania wenzetu waliopewa jukumu la usimamizi je walifuata sheria zilizopo kuingia mikataba hii?
  • Je Bunge, serikali pamoja na vyombo vingine vilikuwa na nafasi yeyote kuzuia uhalifu ?
  • Kama mkataba ni mbovu na ulipitishwa kihalali je anayepaswa kulaumiwa ni Afisa wa serikali, serikali, mwanasheria mkuu, baraza la mawaziri au nani?
  • Ikiwa hawa watu (makampuni) wamejipataia faida kutokana na hii mikataba mibovu je wakulaumiwa ni wao au ni sisi tuliokubali kusaini mikataba mibovu?
  • Ikiwa ubovu wa mikataba yetu ndiyo tatizo je hao watendaji, au hizo kampuni zitakuwa na hatia?
  • Je hapa tulipofikia tulaumu hawa wawekezaji au tujilaumu sisi wenyewe kwa kutokuwa makini?
  • kutokana na juhudi njema za Rais je sio muda muafaka sasa kuwepo na udharura kuunda tume ya kudumu itakayo kupitia mikataba yote mikubwa ili tusiendelee kupoteza? maana mwanya huu ukiachwa kwa wengine watajitahidi kujinasua.
 
Ccm ndiyo wakulaumiwa, pamoja na Chenge
 
habari wadau...

Naona Mh Rais kila anapogusa anakuta watu wamepiga... kuna hisa hadi za watu wasiojulikana..

ni vizuri tukawekana wazi kati ya awamu ya 3 chini ya Mkapa na awamu ya 4 chini ya Jk ipi imeibia sana Watanzania kwa maamuzi mabovu...

huyo atakaeonekana ameibia sana tumkomalie atolewe kinga tumpandishe kwa pilato...

maana haiwezekani kiongozi ulipwe kwa kodi zetu hela nyingi na tunakutunza mpaka kufa kwako.. huku ulikuwa hufanyi kazi yako tuliyokutuma na kuruhusu watu waibie watanzania kwa mikataba ya ajabu...

twende kwa facts.. mkapa vs jk nani alieruhusu ufisadi sana
 
Wakati Mwl Nyerere alisema haya madini tuyaache hayawezi kuoza, sasa bado watanzania hawana elimu ya kuyavuna wakipata elimu tutaanza kuyavuna.

Akaja mwingine akasema ngoja tuonje kidogo, utamu ukakolea ukakolea kweli kweli......
 
Back
Top Bottom