Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,681
- 119,317
Wanabodi,
Naomba kuuliza, kati ya wanafunzi waliopata Div 1 kutoka shule za serikali, St. Kayumba na wale wanaopata Div 1 kutoka shule za Academy, ni nani ni vichwa vya ukweli? .
Hoja yangu hapa ni japo kufaulu ni kufaulu tuu na kunatokana na akili ya mtoto, lakini lazima tukubali aina ya shule na mazingira ya kusomea yana direct impact na performance ya mtoto, hivyo najaribu kulinganisha mtoto aliyesomea shule nzuri, yenye mazingira mazuri ya kosomea, vitabu, walimu, vifaa vya kutosha na huyu aliyesomea shule mbovu, hakuna vitabu, hakuna walimu, mazingira mabovu ya kusomea, na mwisho wa siku wakapata matokeo sawa, jee nani atakuwa ni kichwa kuliko mwingine?.
Mimi kwetu tumezaliwa watoto 8 na wote tulipasi shule za serikali. Nilipokuwa chuo UD, tulikutana na wenzetu waliosoma shule za academy mwisho wa siku, waliokimbiza ni hawa hawa kutoka St.Kayumba.
Hivyo mimi katika familia yangu, nikadhamiria watoto wetu wasome shule za serikali, tuligombana sana na wife kuhusu hili, mimi nikichukulia matokeo ya chuo as sampling, wife akishinikiza tuwajengee msingi imara kwenye shule bora. Niligoma na ilikuwa ugomvi.
Katika matokeo ya form kijana wangu, amepata DIV 1 ya Points 13 kutoka shule ya serikali!. Hii ni kuthibitisha ufaulu ni akili tuu ya mtu, lakini kwa ufaulu huu St.Kayumba, Jee ningekuwa na uwezo wa kumlipia Feza Boys, angeibuka na Div 1 ya points ngapi?.
Naomba muungane nami kuwapongeza wanafunzi wote waliofaulu vizuri, lakini pongezi za ziada ziwaendee wanafunzi wa shule za serikali waliofaulu vizuri, kwa sababu hawa wa serikali wao iliwabidi watafune wenyewe na kumeza, wakati wenzao, wanatafuniwa na wengine wanamezeshwa mitihani! .
Pascal