Nani ni waziri mkuu bora tangu uhuru?

Kwangu mm naona ni mh F. SUMAYE ,Sifa zake _sio mwoga,ana uwezo wa kumshauri mkubwa wake kama alivyofanya kwa mh mkapa,anapenda kushindana kwa hoja,hapendi watu kujaa gerezani,alipenda askari kuwa karibu na raia na kulinda mali zao,ana huruma,upendo,kushauriana maana binadamu si mkamilifu,hapendi umaskini na anatamani kila raia wa tzania kuwa tajiri ,mwisho anapenda m2 anayefuata katiba.!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Usisahau alikuwa anaitwa Mr. Zeroo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sumaye aliitwa Mr Zero. Hakujua chanzo cha umaskini wa nchi hii mpaka alipokwenda kusoma nje ya nchi baada ya kuwa waziri mkuu kwa kipindi cha miaka kumi.

..kwa maoni yangu, kwa nchi yetu, ukiona waziri mkuu halaumiwi, basi huyo hamsaidii mkuu wake wa kazi ambaye ni Raisi.

..waziri mkuu wa tanzania ndiye msimamizi wa shughuli za kila siku za serekali, kiranja wa mawaziri wote.

..Yeye ndiye anayekuwa mstari wa mbele kutekeleza maamuzi ya serekali, yawe mazuri au mabaya, na muda mwingi ndiye hubeba lawama mambo yakienda mrama.

..Waziri Mkuu asipobeba lawama, maana yake mkuu wa nchi / raisi atabeba lawama hizo. Na kwangu mimi hilo likitokea basi waziri mkuu huyo siyo msaada kwa mkuu wa nchi.
 
Back
Top Bottom