Nani ni Nani Urais 2015: Edward Lowassa - Mbunge wa Monduli | Page 4 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani ni Nani Urais 2015: Edward Lowassa - Mbunge wa Monduli

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by mcubic, May 11, 2015.

 1. mcubic

  mcubic JF-Expert Member

  #1
  May 11, 2015
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 10,204
  Likes Received: 4,331
  Trophy Points: 280
  Mtatiro ameendelea kufanya uchambuzi miongoni mwa wanaotaka kugombea Urais, na leo hii anamchambua Lowasa:

   
 2. m

  mzee wa kismati JF-Expert Member

  #61
  Jun 24, 2015
  Joined: Aug 25, 2013
  Messages: 1,556
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  ushahidi
   
 3. farajakwangu

  farajakwangu JF-Expert Member

  #62
  Jun 24, 2015
  Joined: Jun 13, 2015
  Messages: 1,950
  Likes Received: 518
  Trophy Points: 280
  Rudisha hizo CV tumeishachoka
   
 4. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #63
  Jun 24, 2015
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Namshukuru Lowassa maana alituwezesha kusoma pale alipojitoa kusimamia ujenz wa shule za kata
   
 5. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #64
  Jun 24, 2015
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,764
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 145
   
 6. dindili

  dindili Member

  #65
  Jun 24, 2015
  Joined: Oct 28, 2014
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwaka 2005 mahujaji tulikwama zaidi ya siku tatu akiwa waziri mkuu alitusaidia sana kupata ndege ya kutupeleka saudi arabia.mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.
   
 7. The Tomorrow People

  The Tomorrow People JF-Expert Member

  #66
  Aug 9, 2015
  Joined: Jul 11, 2013
  Messages: 2,348
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  MTATIRO ALIWAHI KUYAANDIKA HAYA HADI KWENYE MAGAZETI.

  UDHAIFU WA LOWASSA.

  Udhaifu wa kwanza wa Lowassa ni kuwa karibu mno na watu wenye majina yenye taswira zinazotia shaka. Kuna msemo mmoja wa Kiingereza unaosema, "The bird with same feathers, flocks together" (Ndege wenye mabawa yanayofanana, huruka pamoja). Marafiki wakubwa wa Lowassa ni watu wenye pesa na matajiri, hilo linaweza kumkwamisha katika harakati zake.

  Ndiyo maana jamii imegawanyika mno juu yake, wengine wakimuona kama mtu mwenye mipango mingi ya kifedha na mfanyabiashara zaidi kuliko kiongozi wa nchi huku wengine wakimuona kama kiongozi anayethubutu.

  Ikiwa Lowassa hataweka wazi mgongano wa masilahi ulioko kati yake na baadhi ya wafanyabiashara wenye tuhuma lukuki, jamii itaendelea kumuona kama mtu asiyeweza kukemea maovu.

  Kiongozi mmoja wa CCM ameniambia kuwa, hata mwaka 1995, moja ya mambo yaliyomfanya Mwalimu Julius Nyerere asimuone Lowassa kama chaguo, ni suala la uhusiano wake na matajiri na watu wenye fedha na ilifikia wakati mwalimu akahoji, "…kijana huyu anatoa wapi fedha zote hizi?"

  Udhaifu mwingine wa Lowassa uko katika eneo la mapambano dhidi ya rushwa. Ikumbukwe kuwa Tanzania ilipofikia na uchumi wake unavyozidi kuporomoka, moja ya kazi kubwa ya Serikali ijayo itapaswa kuwa "mapambano dhidi ya rushwa" kwa maneno na vitendo vinavyoonekana.

  Alipokuwa Waziri Mkuu hakuonyesha makeke yake kwenye mapambano dhidi ya rushwa na hakutaka kujihusisha wala kujionyesha kuwa anawachukia wala rushwa. Pamoja na kuonyesha utendaji mzuri akiwa Waziri Mkuu, kipengele hiki kilimuangusha na hadi leo hii kokote kule anakokwenda hapendi kuzungumzia rushwa na wala rushwa. Huu ni udhaifu wake mwingine mkubwa.

  NINI KINAWEZA KUMWANGUSHA?
  Mambo matano yanaweza kumwangusha Lowassa. La kwanza ni makundi. Kama nilivyoeleza, yeye ndiye mtu mwenye kundi kubwa kuliko wagombea wote ndani ya CCM, ikiwa chama hicho kitaamua kumpata mtu wa kati ‘neutral' ili kukifanya chama kisitetereke, yeye ndiye atakayekuwa wa kwanza kuenguliwa.

  Lakini jambo la pili ni kashfa ya Richmond. Tangu kashfa hiyo ilipotokea, Lowassa hakuwahi kuiongelea tena na hajawahi kuwaeleza Watanzania alihusikaje na kama yeye hakuhusika ni kina nani waliohusika kwa majina. Ukweli ni jambo muhimu kwa mtu anayehitaji kuongoza nchi.

  Ukituhumiwa kwa kashfa kubwa kama ya Lowassa halafu unasema tu hukuhusika bila kueleza nani walihusika huku wewe ndiye ulikuwa Waziri Mkuu, inajenga taswira kuwa kuna jambo kubwa unalificha na husemi ukweli kwa jamii yako. Hili linaweza kumhukumu. CCM inaweza kumuondoa Lowassa ili kuondokana na mgombea mwenye madoa hata kama haina uthibitisho na madoa hayo kwa asilimia 100.

  Jambo la tatu linaloweza kumchuja Lowassa ni afya yake. Pamoja na kuwa afya ni jambo binafsi na siri ya mtu lakini kwa kiongozi, kila jambo lake ni mali ya umma. Rais Kikwete alipougua tezi dume aliutangazia umma na hakuficha. Kwa kipindi kirefu Lowassa amekuwa akionekana kama mgonjwa na si siri kuwa amekuwa akipata matibabu katika hospitali za kimataifa nje ya nchi.

  Anapaswa awaeleze Watanzania nini kinamsibu, la asipofanya hivyo wapinzani wake kisiasa wanaweza kuendelea kulitumia jambo hili ipasavyo na chama chake kikaona lina mantiki na kikalitumia kumsulubu kama "unfit person to lead the nation". Kila chama kinahitaji mgombea urais wake awe na afya bora, isiyofichwa na inayoeleweka. Anapaswa kujitokeza na kufafanua hili haraka na hasa ikizingatiwa muda umekwenda sana.

  Michango ya kujitolea kila kukicha katika taasisi mbalimbali, harambee, nyumba za ibada na maeneo mengine ni jambo jingine linaloweza kumhukumu. Lowassa amejitolea mno katika eneo hili. Chama chake kinaweza kujiuliza kwa nini mtu anayejiandaa kugombea urais ajitolee kwa kiwango hiki kusaidia kuchangisha fedha na hata yeye mwenyewe kuchangia kila panapotokea matukio makubwa?

  Je, nia yake ni sahihi? Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa "Ikulu hakuna biashara" na CCM inaweza kujitathmini ikiwa mgombea wa namna hii akiingia Ikulu hataanza kutafuta mbinu ya kujirudishia fedha alizokuwa akichangia. Eneo hili si salama kwa Lowassa
   
 8. Hoshea

  Hoshea JF-Expert Member

  #67
  Aug 9, 2015
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 3,875
  Likes Received: 1,573
  Trophy Points: 280
  Ashee!
   
 9. Mack Wild

  Mack Wild JF-Expert Member

  #68
  Aug 9, 2015
  Joined: Apr 25, 2013
  Messages: 4,668
  Likes Received: 3,087
  Trophy Points: 280
  profesor lipumba yupo kigali rwanda na
  amepangishiwa hotel chini ya ofisi ya ubalozi
  nchini rwanda.
  habari za kijasusi zinathibisha kuwa ni moja ya
  makubaliano ya kikao cha siku mbili mfululizo ofisi
  ndogo ya lumumba muda mfupi kabla ya
  kujiuzuru. Habari za kijasusi pia zinathibisha kuwa
  account yake iliyopo nmb imewekewa jana kiasi
  cha shilingi bil. 3.5 aliyeweka ni afisa wa wale wa
  suti nyeusi akisindikizana na mmoja wa maofisa
  fedha na uchumi wa ccm na fedha imewekwa
  kupitia tawi la tegeta lililopo jengo la kibo complex
   
 10. mop

  mop JF-Expert Member

  #69
  Aug 9, 2015
  Joined: Jul 11, 2015
  Messages: 863
  Likes Received: 604
  Trophy Points: 180
  asante kwa kutuletea kumbukumbu nzuri za huyo fisadi
   
 11. Nifah

  Nifah JF-Expert Member

  #70
  Aug 9, 2015
  Joined: Feb 12, 2014
  Messages: 25,891
  Likes Received: 24,284
  Trophy Points: 280
  Uwiiii nchi imeshauzwa jamani! Nimetikisika hadi nakosa cha kuongea.
  Waione slim5 Steph Curry Mmawia Diva Beyonce Hornet ngw'anapagi na makamanda wote.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. kilambalambila

  kilambalambila JF-Expert Member

  #71
  Aug 9, 2015
  Joined: Nov 16, 2013
  Messages: 7,490
  Likes Received: 3,636
  Trophy Points: 280
  sasa wanalamba matapishi yao wenyewe makanjanja wa siasa
   
 13. Tukundane

  Tukundane JF-Expert Member

  #72
  Aug 9, 2015
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 8,588
  Likes Received: 2,934
  Trophy Points: 280
  Huyo alikuwa ni Lowassa wa zamani Lowassa wa sasa ni rafiki wa masikini ili watajirike.
   
 14. Slim5

  Slim5 JF-Expert Member

  #73
  Aug 9, 2015
  Joined: Jan 7, 2014
  Messages: 17,644
  Likes Received: 16,596
  Trophy Points: 280
  Duuuh! Kweli tutafika? Tutafikaje? Siasa zetu ni ngumu sana! Ahsante Dada nifah
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. TataMadiba

  TataMadiba JF-Expert Member

  #74
  Aug 9, 2015
  Joined: Feb 7, 2014
  Messages: 9,523
  Likes Received: 3,800
  Trophy Points: 280
  Sasa wanakula matapishi yao.
   
 16. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #75
  Aug 9, 2015
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,647
  Likes Received: 3,506
  Trophy Points: 280
  Kwahiyo wameona sahivi ndo anaweza kuwa hana tena hayo mapungufu? CDM mmemtakasa Lowassa nyie mmekuwa kanisa? na je, Lowassa kutubu kwenu katubu nini? na je, Lowassa aliwakosea CDM tu ama aliwakosea watz kwa ujumla, mbona hajaja kwetu kutubu badala yake kaja kwenu tu, kwani atachaguliwa na wana CDM tu ama mnamleta achaguliwe na watz? hamuoni mmebugi?
   
 17. Mmawia

  Mmawia JF-Expert Member

  #76
  Aug 9, 2015
  Joined: Aug 20, 2013
  Messages: 58,487
  Likes Received: 23,355
  Trophy Points: 280
  Kwahiyo?
   
 18. JAMII-ASM

  JAMII-ASM JF-Expert Member

  #77
  Aug 9, 2015
  Joined: Jul 30, 2015
  Messages: 1,306
  Likes Received: 465
  Trophy Points: 180
  '' Kwa kipindi kirefu Lowassa amekuwa akionekana kama mgonjwa na si siri kuwa amekuwa akipata matibabu katika hospitali za kimataifa nje ya nchi.''

  Mh.Mtatiro..hii imekaaje..?
   
 19. Mmawia

  Mmawia JF-Expert Member

  #78
  Aug 9, 2015
  Joined: Aug 20, 2013
  Messages: 58,487
  Likes Received: 23,355
  Trophy Points: 280
  Wewe unawashwa nini wakati hayo matapishi wanakula wao?
   
 20. Mmawia

  Mmawia JF-Expert Member

  #79
  Aug 9, 2015
  Joined: Aug 20, 2013
  Messages: 58,487
  Likes Received: 23,355
  Trophy Points: 280
  Mbona hamtuletei sakata la mafisadi waliokwapua fweeza za escrow stanbic?
   
 21. zaleo

  zaleo JF-Expert Member

  #80
  Aug 9, 2015
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,768
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  CCM dola ndiyo hiyo. Wamesikiks kwamba watalamba dume kutoka ukawa, kumbe Lipumba!!!! Labda wanashindwana na Slaa, maana magari meusi ya wenye miwani myeusi kutoka ikulu wanadaiwa kupishana mlangoni kwa Slaa. Hawaijui CDM vizuri, ina macho mapana kuipita TISS!!
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...