Nani Ndani Ya TRA Ananufaika na Kampuni Ya Yono Mart

Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,372
6,078
Kamati ya bunge imeamuru NSSF iifahamishe TRA kampuni ya Yono Mart usimamishe mpango wa kuuza nyumba za mradi wake wa Dege Eco Village baada ya mkandarasi wa mradi huo wa ujenzi Mutluhan kutoka nchini Uturuki kudaiwa deni la kodi la bilioni 45.
Hivi inaingia akilini kuuza mradi wa NSSF ulioitia hasara ya bilioni 270 kwa shirika hilo kwa kufidia deni la mkandarasi la bilioni 45.
TRA na Yono Mart pia walishindwa kuuza nyumba za Lugumi baada kuonekana kampuni ya Lugumi inadaiwa bilioni 13 na lakini wanataka kuuza nyumba kwa bei ambayo sio kwa thamani halisi ya nyumba hizo. Serikali itupie macho hii kampuni ya Yono Mart ambayo itailetea hasara kubwa wenye mali (wadaiwa) na TRA katika harakati zake za kupenda kupiga mali mnada kwa haraka kwa maslahi ya kampuni hiyo.
 
Umenena vema. TRA na madalali ni sawa na mvinyo wa zamani kwenye viriba vipya.

Wanakula kwa zamu, nchi ya madili tu. Ilikuwa Majembe enzi zile kisha awamu hii ni Yono.
 
Hiyo Yono ni Kampuni ya Mwana CCM mwenzenu na bila ya shaka wanaofaidika ni nyie na chama chenu!!
Ninaona kama TRA inachafuliwa sana na tamaa za madalali kama Yono. Kwanza walikuwepo majengo. Nasikia shingo ilishaelekea kibra..sijui kama alishachinjwa maana naye mali zake zilikuwa mnadani
 
Yono Auction mart ni kampuni ya mwanasisiemu aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Njombe magharibi enzi hizo akiitwa Stanley Kevela Yono.
Wanufaika ni CCm na vitambi vyao.
 
Kwanini tusibadilike tu tuanze upya tusahau yaliyopita tujenge nchi yetu. Kweli kabisa tunacheza Na maisha hasa uchumi. Miaka kumi tu we can make a big difference. Tunavyoishi inasikitisha
 
Kwanini TRA isiunde chombo au department ya kuhusika na hayo mambo kuliko kutoa hela kwa hap yono
Mkuu ukiaangalia utaratibu haufatwi kama inavyotakiwa. Mdaiwa ama wadaiwa sugu mnada unatakiwa kutangazwa kwenye gazeti na Kamishina wa TRA. Sasa cha kushangazaa Yono Mart imekuwa kama kitengo cha TRA wao ndio wanaenda kufunga biashara za watu na kuita press conference wakiwa na furaha kubwa sana kuuza mali hizo.
TRA iweke wazi ilitumia kigezo gani kutoa tenda kwa Yono Mart na analipwa kiasi gani Je hii minada ya Yono Mart hayana magumashi.
 
Kamati ya bunge imeamuru NSSF iifahamishe TRA kampuni ya Yono Mart usimamishe mpango wa kuuza nyumba za mradi wake wa Dege Eco Village baada ya mkandarasi wa mradi huo wa ujenzi Mutluhan kutoka nchini Uturuki kudaiwa deni la kodi la bilioni 45.
Hivi inaingia akilini kuuza mradi wa NSSF ulioitia hasara ya bilioni 270 kwa shirika hilo kwa kufidia deni la mkandarasi la bilioni 45.
TRA na Yono Mart pia walishindwa kuuza nyumba za Lugumi baada kuonekana kampuni ya Lugumi inadaiwa bilioni 13 na lakini wanataka kuuza nyumba kwa bei ambayo sio kwa thamani halisi ya nyumba hizo. Serikali itupie macho hii kampuni ya Yono Mart ambayo itailetea hasara kubwa wenye mali (wadaiwa) na TRA katika harakati zake za kupenda kupiga mali mnada kwa haraka kwa maslahi ya kampuni hiyo.
Wanauza haraka maana huwa commission yao ya udalali ni kati ya 10% to 20% ya pesa waliyouza, hivyo wanaangalia faida yao pekee.
 
Leo nimefurahi sana kwa wadau wa JF kuliona hili swala,nilisha wahi kujiuliza kunatofauti gani kati ya YONO na TRA mbona kama wanafanya kazi zinazofanana!!lakini kinacho sikitisha zaidi nitabia ya kuviziana waliyo nayo YONO wao huwa wanapenda sana kufilisi kuliko maelezo wao hawana notes to publication wanacho waza ni kuuza tu,lakini pia hii kampuni inalipa kodi baada ya mnada au inajificha nyuma,kwann TRA isianzishe kitengo cha kupiga mnada wadaiwa na kuachana na kampuni ambazo hazijui hata elimu ya kulipa kodi ipo je
 
Umenena vema. TRA na madalali ni sawa na mvinyo wa zamani kwenye viriba vipya.

Wanakula kwa zamu, nchi ya madili tu. Ilikuwa Majembe enzi zile kisha awamu hii ni Yono.

Hawa madalali watu wabaya sana..ukikaona kale kamama kanavyosema utafikiria kuna haki. Matunguli yana mwisho wake. Amuulize Majembe. Wasione raha kusumbua watu wasio na hatia.
 
Back
Top Bottom