Uongo ni kitu cha kawaida katika mapenzi.Hata Ibrahim kwenye biblia aliongopa kuwa, Sara si mkewe,ili kuepuka mfalme asimuue yeye na kumchukua mkewe mrembo awe wake.Hata hivyo imeandikwa waongo hawatauona ufalme wa mbinguni. Tuyaache hayo. Sasa? Leo hii kwenye mapenzi watu wanaongopeana kweli kweli,tena bila sababu yoyote ya maana wamezidisha sana, utasikia,
Mara sina pesa wakati anazo kibao, mara nasafiri kumbe yupo Dar,mara nisubiri nipo karibu nakuja sasa hivi,kumbe yuko mbali sana na atatokea baada ya masaa matatu,mara sjaolewa au sina mke au mchumba wakati anae .mara nitakufanyia hivi na asitekeleze,mara nakupenda sana sili chakula wala silali usingizi kwa ajili yako,wakati anakula ananeepeana na analala hadi anachelewa kazini,mara I love you,kumbe i hate you, mara you only, kumbe wapo kama saba hivi kila siku wanaambiwa you only. Mara naumwa au sijisikii vizuri kumbe looo, hajambo kabisa,mara huyu tulisoma wote, looo ,kumbe ni mpenzi wake,mara simu iliisha chaji wakati alizima simu, mara nipo mbagala wakati yupo kimara mara nipo kazini kumbe yupo guest house au bar.Kuna wataalamu wa uongo katika mapenzi jamani. Kwani ni lazima uongope?.Hasara ya uongo ni kuumbuka na kupata aibu siku ukweli ukijulikana. Kinachonitatiza ni kumjua Nani mwongo zaidi kwenye mapenzi? ni Mwanaume au Mwanamke? naomba tuwe fair, Ili kumjua chukulia wewe binafsi umeshamwongopea au kuwaongopea mpenzi/wapenzi wako mara ngapi? na je umeshaongopewa na mpenzio/wapenzi mara ngapi?baada ya tathmini hiyo utapata upande unaozidi, kama wewe ni mwongo zaidi na ni mwanaume basi jibu litakuwa wanaume waongo zaidi kwenye mapenzi.Tukimjua nani zaidi au jinsia gani zaidi, hatutaisuta au kumsuta ila kwanza tutakuwa na tahadhali,pili tutawaomba angalau wapunguze jamani. Uongo unaharibu raha ya mapenzi ati.Unakuta mtu kutwa nzima anamwongopea mpenzi wake mara18 hivi?