Nani mwenye shaka juu ya demokrasia ya nchi za Magaharibi hasa baada ya Waziri Mkuu Uingereza kujiuzulu?

ankai

JF-Expert Member
Nov 25, 2017
3,280
4,236
Nasubiri kuona kiongozi wetu mkuu kuiga mfano halisi wa demokrasia sahihi na hakika kutoka kwa kiongozi wa jumuiya ya madola.

Yaaani ndani ya kipindi cha mwezi mmoja na nusu tumeshuhudia kwa macho yetu wenyewe kabisa mawaziri wakuu wawili tena wa dola kubwa sana duniani wakijiuzulu kutokana tu na vionho,i wenzao kusema tu hawana imani nao.

Nafikiria apa mfano ndo ingekuwa ni katika moja wapo ya nchi za kiafrika je jambo kama hili lingewezekena? si kwamba tushuhudia umwagaji mkubwa sana wa damu yaani raia wasio na hatia kuuwawa na makundi mawili ambayo ndo yangekuwa yana hasimiana.

Natamani sana kiongozi wetu mkuu wa dola kama na yeye anagalau ata kwa unafiki kidogo tu angeiga ama kufata nyayo za baba wa jumuiya ya madola ingekuwa poa sana.

Angalau kwa kutoa basi nafasi na fursa sawa kwa wanasiasa wote wanaofanya siasa tanzania, uhuru wa kutoa maoni na uhuru wa vyombo vya habari.

Kiukweli leo ndo nimeamini wenzetu wamefika katika stage ya juu sana hasa kwenye suala la ustaarabu yaani wako very civilized wazungu wamestaarabika mno.

Nawasilisha.
 
Ajitokeze mwenye mashaka mpaka sasa na hii demokrasia ya hawa mnao waita mabeberu asee hawa jamaa wamefika level ya juu mno katika kustaarabika wako very civilised indeed!

Yaaani katika swala la ustaarabu duuuh nimewavulia kofia jamaa wana haki kabisa ya kututawala hapo awali

Wanajielewa, wanajitambua , wanaufahamu mkubwa sana, na viongozi wote wa magharibi wapo kwa ajili ya maslahai ya wanancji wao!
 
Si Europeans wote wanaelewa na kuheshimu suala la uwajibikaji. Mfano halisi ni wale madikteta wa Ulaya mashariki ambao hawana tofauti sana na madikteta na mafisadi wa kusini mwa jangwa la Sahara.

Kuna yule wa Belarus pamoja na yule mwenzake aliyeambiwa na waziri mkuu wa India kuwa "zama hizi sio zama za vita".
 
Kweli hao ni wazungu waafrika
 
“....that these dead shall not have died in vain– that this nation, under God, shall have a new birth of freedom and that government of the people, by the people, for the people, shall not perish from earth” (US President Abraham Lincoln, The Gettysburg Address, November 19, 1863)
 
Hakuna demokrasia hapo bali ni uozo mtupu, lazima kiongozi utatue matatizo ya wananchi wako sio kuya kimbia kwa kigezo cha kujihuzuru.

:Rundo la Watanzania wajinga ni mtaji wa wanasiasa mafisadi wa hii nchi [ Ccm, Chadema, Nccr, Act, Cuf n.k ]
 
25 September 2022​

Hali ya misukosuko ya kisiasa ya Italia

Italia imekuwa na historia ya misukosuko ya kisiasa. Serikali mpya itakayoundwa itakuwa ya 68 tangu mwaka 1946. Waziri Mkuu mpya ajaye atatarajiwa kukumbwa na changamoto si haba, hususan ongezeko la bei ya nishati.

Wakuu wa Umoja wa Ulaya wanaojizatiti kukuza ushirikiano wao, hasa baada ya Urusi kuivamia Ukraine, wana wasiwasi kwamba Italia itakuwa mshirika asiyetabirika kuliko ilivyokuwa chini ya uongozi wa Draghi

1666320101306.png

Rome - Ikulu ya Italia imetangaza Alhamisi wiki hii kuwa, nchi hiyo itafanya uchaguzi Septemba 25 kabla ya wakati uliopangwa, baada ya Waziri Mkuu Mario Draghi kujiuzulu na kuvunjwa kwa bunge.

Kujiuzulu kwa Draghi kumefanya serikali yake ya umoja wa kitaifa iliyoundwa Mwezi Februari 2021 kwa kuungwa mkono na muungano mpana kufikia mwisho. Uamuzi wake wa kujiuzulu umekuja baada ya washirika watatu wakuu katika muungano huo kutoshiriki katika upigaji kura ya kutokuwa na imani kwenye Bunge la Seneti siku ya Jumatano, hivyo basi kuondoa uungaji mkono wao kwa baraza la mawaziri

...
Italia yapiga kura kuchagua bunge jipya | Matukio ya Kisiasa

25 Sept 2022 — Italia inafanya uchaguzi Jumapili ambao unatarajiwa kurejesha muungano wa ... ya Umoja wa kitaifa ya aliyekuwa Waziri Mkuu Mario ...
waziri mkuu wa italia from amp.dw.com
http://www.bbc.com/swahili/live/habari-63004060
 
29 November 2021
Stockholm, Sweden

Waziri Mkuu wa kwanza mwanamke wa Sweden ajiuzulu saa chache baada ya kuchaguliwa​

Novemba 25, 2021

Kutoka maktaba Agosti 26, 2021 Muda mfupi baada ya kuchaguliwa na Bunge kuwa Waziri Mkuu wa kwanza mwanamke, Madgalena Andersson Jumatano ya Novemba 24, 2021, aliwasilisha barua ya kujiuzulu kwake huku akikabiliwa na changamoto kubwa ya kuongoza serikali ya mseto ya walio wachache.
More info:
STOCKHOLM - Muda mfupi baada ya Kiongozi wa Chama cha Social Democrat Magdalena Andersson kuchaguliwa na Bunge kuwa Waziri Mkuu wa kwanza mwanamke wa Sweden siku ya Jumatano ya wiki hii, ameandika barua ya kuomba kujiuzulu huku akikabiliwa na changamoto kubwa ya kuongoza serikali ya mseto ya walio wachache.

Saa chache tu baada ya kuchaguliwa kuwa Waziri Mkuu, Bunge la Sweden (Riksdag) lilipitisha pendekezo la bajeti lililowasilishwa na vyama vya upinzani na kusababisha mshirika wa muungano wa chama anachokiongoza Andersson, Green Party kuondoa uungaji mkono wake. Hatua hii ilimlazimu Andersson kutangaza kujiuzulu kwake.

Mwenendo wa matukio hayo ya Jumatano ulitokana na matokeo ya uchaguzi wa Mwaka 2018 ambayo hayakuamua mshindi wa jumla kuweza kuunda Serikali hivyo kusababisha mchakato mrefu wa kisiasa wa kuunda serikali ambapo vyama fulani hufanya kila liwezalo kuzuia wapinzani wao wa kiitikadi kupata ushawishi wa aina yoyote.

Sweden’s first female PM returns after resigning last week​

1666320644227.png

Sweden’s Social Democratic Party leader Magdalena Andersson has been reappointed as prime minister after she was forced to resign from the role last week within hours of election.

The Swedish parliament, the Riksdag, has now narrowly elected to reinstate Andersson as prime minister, in a vote with 101 of its 349 members voting ‘yes’. 173 members voted ‘no’ and 75 abstained. This was enough to get Andersson across the line, with the rules stating that a candidate for prime minister only needs to avoid a majority voting against them.

Andersson resigned as prime minister last week after the Green Party withdrew from her coalition government, causing it to collapse. She will now attempt to lead a one-party, minority government.

Last week, Andersson’s budget proposal failed to pass through the parliament, which led to the adoption of another budget proposal presented by three opposition parties, including th conservative Moderates, Christian Democrats, and the far-right party Sweden Democrats Source : Local Archives
 
3 August 2020
BELGIUM SIKU 592 BILA KUWA NA WAZIRI MKUU

Nchi ya Belgium imevuja rekodi, kwa kutokuwa na kiongozi wa serikali kwa siku 592.

Pia imewahi kutokea huko nyuma nchi hii ya Belgium kuendelea bila kutetereka kwa siku 541 bila kuwa na kiongozi mkuu wa serikali yaani waziri mkuu

Kuwepo kwa taasisi imara zinazoongozwa na makatibu wakuu wa mawizara na zile taasisi za serikali za Mitaa kumewezesha nchi kazi iendelee bila ya kuwepo waziri mkuu ...

The Brussels Times
https://www.brusselstimes.com › bel...
Belgium breaks own record for longest period without government

3 Aug 2020 — It has been 592 days since the previous government, led by former Prime Minister Charles Michel, collapsed over inter........
Strained negotiations after last year's elections in May have routinely collapsed as party leaders and several top government officials resign from their mission to steer the coalition negotiations.

The previous record for Belgium's longest post-election period without a government stands at 541 days and ended with the swearing-in of Former Prime Minister Elio Di Rupo after a similarly convoluted negotiation period followed the June 2010 elections Source : Belgium breaks own record for longest period without government
 
Nasubiri kuona kiongozi wetu mkuu kuiga mfano halisi wa demokrasia sahihi na hakika kutoka kwa kiongozi wa jumuiya ya madola.

Yaaani ndani ya kipindi cha mwezi mmoja na nusu tumeshuhudia kwa macho yetu wenyewe kabisa mawaziri wakuu wawili tena wa dola kubwa sana duniani wakijiuzulu kutokana tu na vionho,i wenzao kusema tu hawana imani nao.

Nafikiria apa mfano ndo ingekuwa ni katika moja wapo ya nchi za kiafrika je jambo kama hili lingewezekena? si kwamba tushuhudia umwagaji mkubwa sana wa damu yaani raia wasio na hatia kuuwawa na makundi mawili ambayo ndo yangekuwa yana hasimiana.

Natamani sana kiongozi wetu mkuu wa dola kama na yeye anagalau ata kwa unafiki kidogo tu angeiga ama kufata nyayo za baba wa jumuiya ya madola ingekuwa poa sana.

Angalau kwa kutoa basi nafasi na fursa sawa kwa wanasiasa wote wanaofanya siasa tanzania, uhuru wa kutoa maoni na uhuru wa vyombo vya habari.

Kiukweli leo ndo nimeamini wenzetu wamefika katika stage ya juu sana hasa kwenye suala la ustaarabu yaani wako very civilized wazungu wamestaarabika mno.

Nawasilisha.
Watakuroga nakwwmbia.

Uwajibikaji siyo eneo la utamaduni wetu.

Tena umesahau zile methali maafufu fufufu za
1. Ukubwa dawa
2. Mkubwa hakosei.

Tupo kwenye chupa na aliyetusomea albadiri alishafanyiwa hitima karne zilizopita
 
Hakuna demokrasia hapo, kilichopo ni vurugu tupu.

Nchi za Italy, Sweden, Belgium, Uingereza n.k zenye taasisi madhubuti za serikali kuu zenye makatibu wakuu wa mawizara na viongozi wa serikali za majimbo / serikali za mitaa madhubuti zinaweza kuendelea na kuendesha nchi hata miaka 3 na zaidi bila ya kuwa na waziri mkuu na baraza la mawaziri.

Nchi zenye taasisi dhaifu zisizokuwa huru na maafisa wakuu wa serikali makada (mfano CCM) kama makatibu wakuu na viongozi wa halmashauri za wilaya dhaifu ndiyo hutegemea jeshi la mtu mmoja yaani ulazima wa uwepo wa rais mtendaji au mkuu wa serikali waziri mkuu ili kazi ziendelee .

Mfano katiba ya nchi kumrundikia rais au waziri mkuu kuteua makatibu wakuu wa wizara, wakurugenzi wa ndani ya mawizara, wakurugenzi watendaji wa miji, halmshauri n.k ni kutengeneza taasisi hizo kuwa dhaifu.

Hii hupelekea Wateuliwa wa rais kukosa ubunifu, kushindwa kushauri, kuto kutoa nafasi ya ushiriki-mawazo wa raia na kubwa kukosa uwezo wa kufanya maamuzi makubwa kwa faida ya raia wa nchi na taifa lao maana wanangoja maelekezo ya rais ameagiza nini ametoa tamko gani, ameshauri nini n.k .
OFISI YA RAIS TAMISEMI : Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa : Hisoria ya Taasisi | PO-RALG
MALUNDE
https://www.malunde.com › 2021/08
rais samia ateua wakurugenzi wa halmashauri za wilaya ,jiji, miji ...

2 Aug 2021 — Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Wakurugenzi Watendji wa Halmashauri za Jiji, Miji, Manispaa , wilaya
 
Ajitokeze mwenye mashaka mpaka sasa na hii demokrasia ya hawa mnao waita mabeberu asee hawa jamaa wamefika level ya juu mno katika kustaarabika wako very civilised indeed!

Yaaani katika swala la ustaarabu duuuh nimewavulia kofia jamaa wana haki kabisa ya kututawala hapo awali

Wanajielewa, wanajitambua , wanaufahamu mkubwa sana, na viongozi wote wa magharibi wapo kwa ajili ya maslahai ya wanancji wao!
Bandugu wazungu wapo civilised sana tena toka zamani sana na viongozi wao hawapo kwa ajili ya kutajirika wao na familia zao bali wapo kwa ajili ya kuwaongoza watu wao na mataifa yao kwa ajili ya better life yao wote !! Maana wao huwa hawana tabia za kutambiana kwamba unanijua mimi ni nani !! Ndio maana ukiwaona akina Bill Gates na Kina Jeff Bezos unawaona ni watu wa kawaida sana. !!! Hao ndio wazungu !!
Ajitokeze mwenye mashaka mpaka sasa na hii demokrasia ya hawa mnao waita mabeberu asee hawa jamaa wamefika level ya juu mno katika kustaarabika wako very civilised indeed!

Yaaani katika swala la ustaarabu duuuh nimewavulia kofia jamaa wana haki kabisa ya kututawala hapo awali

Wanajielewa, wanajitambua , wanaufahamu mkubwa sana, na viongozi wote wa magharibi wapo kwa ajili ya maslahai ya wanancji wao!
 
Afrika mtu akiwa kiongozi wale wa chini yake wanageuka chawa, na kuanza kumsifia na unafiki mbere kwa mbere. Teuzi za kupeana kama zawadi au shukrani bila kujali sifa na uwezo.
Hii tabia ipo kuanzia chama tawala mpaka vyama vya upinzani. Hakuna uwajibikaji na kumkosoa kiongozi akiwa madarakani ni uhaini.
Nchi za afrika mfumo wa udikteta au umwinyi ndio unatufaa, demokrasia haitekelezeki kinachifanyika ni usanii.
 
Back
Top Bottom