marveljt
JF-Expert Member
- Jan 11, 2017
- 1,503
- 1,479
Makonda akiwa na Sirro walitangaza majina ya watumiaji/wauzaji wa dawa za kulevya. Walitakiwa kufika kituo cha polisi na mmoja wao alikuwa Mbowe.
Wakati fulani Makonda alisema kabla hujaitwa tayari tumeshakuchunguza miaka 10 iliyopita na tunao ushahidi dhidi yako. Katika tukio la kumkamatwa Mbowe juzi, kupekuliwa na kuhojiwa bado ameonekana hana hatia.
Je, jeshi la polisi halikufanya uchunguzi kuhusiana na Mbowe na kupata ushahidi kuwa ni mtuhumiwa ndani ya miaka 10? Tulichaguliwa Kamishna wa dawa za kulevya, je kwa nini yeye asitoe taarifa ya kumtaka Mbowe ili amhoji bali Sirro ndiye aliyekuwa anasisitiza.
Je, Sirro kuendelea kutangaza majina hajaingilia kazi ya kamishina?
Tulisikia wabunge wakisema RC na DC waliotakiwa kuhojiwa wameambiwa wasiende kuhojiwa na jana tumeshuhudia Makonda, Sirro na Wambura kutokutii amri ya mahakama. Je, Sirro yuko juu ya Kamishna, mahakama? Je, Makonda yuko juu ya bunge na mahakama?
Kama viongozi hatii sheria ina maana sheria ni kwa ajili ya walalahoi tu?