Nani mwenye maslahi kwenye huu Ufisadi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani mwenye maslahi kwenye huu Ufisadi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bornvilla, Apr 2, 2011.

 1. Bornvilla

  Bornvilla JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 925
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Nakumbuka kama miaka 3 au 4 iliyopita nakumbuka ilipelekwa hoja na Dr.H.Mwakyembe juu ya ufisadi unaofanywa na Blue Financial Services,Bayport Financial Services,na wengine kama hao.Mfano Bayport mkopo wowote unaanza kwa miaka3 lakini mkataba huo ni wa uongo kwani utadumu kwa muda wa miaka5. Mkopaji anarudisha mara4 ya kiasi alichokopa.Mfano ukikopa milioni moja utalazimika kulipa milioni4,jamani huu ni wizi mkubwa.Mkataba halisi unaosainiwa ni miaka 3 lakini hutaamini utakapogundua uliingia mkenge.Jamani serikali iko wapi? Benki kuu iko wapi? Kama sikosei mwaka jana Mh.Zitto alilirudisha suala hili bungeni lakini hakukuwa na majibu ya kuridhisha.Tukumbuke kuwa wanaoingia mikataba hii ya kilaghai ni wafanyakazi wa serikali ambao mishahara yao haikidhi mahitaji na kwa kuwa mikopo hii ya wizi haina masharti basi wafanyakazi wengi wameumia hasa wale walioko vijijini.Nani anafaidika na wizi huu wakutisha wa mishahara ya wafanyakazi?Dr.Mwakyembe na Mh.Zitto mlifikia wapi au mlishindwa kuwasaidia wanyonge hawa ambao wanateseka na mikopo hii ya kitapeli? Na je,nani mwenye maslahi na makampuni haya? Benno Ndullu uko wapi? Mh.Mkulo je,unalijua hili? Katiba mpya iainishe na itazame vitu kama hivi la sivyo hatuipitishi.HUU NI UNYONYAJI!
   
Loading...