Nani mwenye mapenzi ya kweli kwenye hili?

Mtanzatozo

JF-Expert Member
Mar 2, 2016
972
1,163
Habari wapendwa na poleni kwa majukumu.

Kuna jambo la kawaida kwenye maisha yetu ya kila siku nimeona si vibaya kusaidiwa kudadavua au kulijadili kwa pamoja bila upendeleo!

Kwenye maisha ya mapenzi au pengine maisha ya ndoa kuna changamoto nyingi sana na bila kujali tunapaswa kupambana nazo kila leo, sawa vipi kunapokuwa mmoja wenu hana uwezo wa kutunga mimba au kubeba uja uzito?

Naomba nieleze kwa ufupi tu, mara nyingi tumeona kwenye ndoa mwanamke anaweza kuwa na tatizo la uzazi na mwanaume akazalisha mwanamke mwingine na maisha ya ndoa yakaendelea pasi na matatizo na pengine mwanamke akamlea yule mtoto pasi na dhulma ya kimalezi na ndoa ikadumu mda wote.

Je, tuigeuze hii upande wa kiumeni, vipi mwanaume awe na haya matatizo ya uzazi na mwanamke akawa na uhitaji wa mtoto?

Mwanaume ataruhusu aletewe mtoto wa baba mwingine akiwa ndani ya ndoa?

N.B. IJADILIWE KAMA ILIVYOWASILISHWA! SHUKRANI.
 
Hiyo wanawake wanafanya sana ila kwa wale ambao uzazi huko vizuri. Wanagawa kitumbua nje then unabambikiwa mtoto. Kwa mwanaume ambaye anajua kabisa ana tatizo ni ngumu kumkubalia akazae nje ila kama mwanaume ukiwa unajua huwezi kuzalisha halafu ukamficha mkeo kuhusu hilo tatizo utaletewa watoto vizuri tu.
 
Back
Top Bottom