Nani mwenye kosa? Serikali, anayeuza kiwanja kando ya mto au anayenunua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani mwenye kosa? Serikali, anayeuza kiwanja kando ya mto au anayenunua

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jumakidogo, Dec 22, 2011.

 1. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #1
  Dec 22, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Mvua kubwa inayoendelea kunyesha na kuwatimua watu waliojenga mabondeni imesababisha mjadala mkubwa na mgongano wa mawazo kila mtu akielekeza lawama kwa upande anaoona unafaa kulaumiwa. Hapa ni nani hasa alaumiwe? Serikali huhimiza watu wasijenge mabondeni, lakini inapokuta watu wamekiuka amri hiyo, huwaacha na kuwafikishia huduma muhimu za jamii mfano maji na umeme. Kitu ambacho watu hawa hujiona tayari wamehalalishiwa makazi yao. Upande mwingine wapo wanaowalaumu wale wanaowauzia viwanja wenzao ilihali ya kuwa wanajua maeneo hayo hayafai kwa ujenzi. Wengine wanawashangaa wale wanaonunua viwanja hali wakijua kuwa maeneo hayo ni hatari kwa maisha yao. Hapa ni nani mwenye mzigo mkubwa wa dhambi na lawama kuliko mwingine?
   
Loading...