Nani mwenye jukumu la kuuondoa ukoloni mamboleo barani afrika?

bbukhu

Member
Feb 25, 2012
58
1
Kwa sasa, tatizo moja sugu barani Afrika ni ukoloni mamboleo ambao ulianza rasmi katika miaka ya 80. Hii haina maana kuwa ukoloni huo kabla ya miaka hiyo haukuwepo la hasha. Msingi wa ukoloni mamboleo uliwekwa na mabepari kabla na wakati wa ukoloni mkongwe. Kipindi chote cha ukoloni, wakoloni walisomba rasilimali zote za bara la Afrika na kuzitumia kwa manufaa yao kwa kuweka kipaumbele katika maendeleo ya nchi zao. Wakoloni hao waliporidhika na unyonyaji wa rasilimali za Afrika na hasa hasa walipopata usumbufu wa kelele za kudai uhuru na haki kutoka kwa waafrika wazelendo, hawakuona sababu ya kuendelea kubaki Afrika kwani tayari walikuwa wameshaweka msingi imara wa utegemezi wa milele wa waafrika kwao.Walishajua kwamba waafrika wameshapata kilema cha maisha. Hivyo unyonyaji ni lazima uendelee hata baada ya uhuru. Ukoloni mamboleo ukawa ndio mbadala wa ukoloni mkongwe na ukawa ni mfumo rasmi wa kuendelea kuzinyonya rasilimali za bara la Afrika kiurahisi na kwa uhakika zaidi kwa njia ya kutoa misaada inayoambatana na masharti magumu yanayodumisha umaskini wa bara hili ingawa wakoloni mamboleo wanadai kupitia wanazuoni wao kuwa ili nchi za kiafrika ziendelee ni lazima zipate misaada na kufuata mkondo uleule walioufuata nchi zilizoendelea. Madai hayo kwa mfano yanatolewa na watu kama akina Nurkse, Gill, Rostow na Leibeinstein. Madai hayo yanaonesha unafiki wa hali ya juu wa wakoloni mamboleo. Wanaendelea kutupa mawazo butu yanayolenga kutubakiza waafrika katika usingizi na wao waendelee kutonyonya. Hii haiwezekani, waafrika lazima tuamke.

Njia nyingine inayotumiwa na wakoloni mamboleo kuendeleza unyonyaji wa rasilimali ni kwa kutumia vibaraka na madikteta wa kiafrika ambao wanayalinda maslahi ya mabwana wao wa kikoloni mamboleo. Kwa jitihada zao za kurahisisha unyonyaji wa rasilimali za bara lao na kuyalinda maslahi ya mabepari mamboleo, wao hupata vijizawadi kutoka kwa wazungu na maisha yao husonga mbele wakati maisha ya watu wao yamebaki taabuni.
Mswali ya msingi hapa ni; Je, ni nani mwenye jukumu la kuundoa ukoloni mamboleo? Je, ni viongozi wa bara hili au ni waafrika wanaoishi maisha ya dhiki na taabu? Je, viongozi wa kiafrika wanaoishi maisha ya pepo bila kifo kwa kujigawia kiasi kikubwa cha rasilimali ya nchi zao wanaathiriwa na ukoloni mamboleo? Je, ukoloni huo usipoondolewa nani wataumia zaidi; viongozi au waafrika wanaoishi katika umaskini? Je, wasomi wa kiafrika wana nafasi gani katika kulikomboa bara lao dhidi ya dhuluma za mabepari? Je, wasomi hao wamepata elimu ambayo inawapa uzalendo? Je, waafrika tutaendelea kuyavumilia makali ya ukoloni mamboleo hadi lini?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom