Nani mwenye haki ya kutamka kuwa wewe ni raia wa nchi hii au laa........??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani mwenye haki ya kutamka kuwa wewe ni raia wa nchi hii au laa........???

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ngalikihinja, Aug 17, 2010.

 1. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #1
  Aug 17, 2010
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,390
  Likes Received: 3,719
  Trophy Points: 280
  ............Baadhi ya nyaraka ambazo zimetolewa na Idara ya Uhamiaji nchini na kuonwa na Mwananchi zilionyesha kuwa Bashe aliyekuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM katika Jimbo la Nzega, ni raia wa Tanzania.

  Waraka uliothibitisha uraia wake na kutumwa kwa Katibu Mkuu wa CCM, makao makuu Dodoma ambayo gazeti hili imeuona unaeleza kuwa Bashe alikabidhiwa hati ya uthibitisho wa kuwa raia yenye Na. S/N 312 ya Agosti 10 mwaka 2009 na kivuli cha nakala hiyo kiliambatanishwa kwenye barua hiyo ya uthibitisho.............

  ..........Ingawa alipozungumzia uthibitisho ulioelezewa kwenye waraka huo Katibu Mkuu wa CCM, Yusufu Makamba alisema kuwa ni kweli ameiupata,lakini akasisitiza kuwa Bashe si raia japokuwa chama kinampenda.

  "Nimeipata barua, nimeusoma, lakini nasema Bashe si raia, tunampenda na ana uwezo wa kupigiwa kura na kushinda, lakini si raia,"alisema Makamba.

  Alisema kuwa uhamiaji huwa wanaangalia vitu vichache tu kumthibitisha mtu hivyo hakubaliani na uthibitisho wa uhamiaji.

  "Uhamiaji wanaangalia kitu kimoja tu kama ni raia labda cheti cha kuzaliwa, mimi nasema si raia, hatuwezi kumpitisha na hatukubali kwa kuwa masuala ya uraia yana mambo mengi,"alisema Makamba.........................
  Source: Mwananchi ya tarehe 17/08/2010

  Nisaidieni jamani.......................NANI MWENYE MADARAKA YA KUSEMA HUYU NIO RAIA WA NCHI HII AU LAA..........???
   
 2. SHUPAZA

  SHUPAZA JF-Expert Member

  #2
  Aug 17, 2010
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 548
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Luteni (Mstaafu) Yusuph Makamba
  Katibu Mkuu
  Sisiem
   
Loading...