Nani mwenye akili kati ya makamba na mzee kisumo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani mwenye akili kati ya makamba na mzee kisumo?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lokissa, Dec 30, 2010.

 1. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #1
  Dec 30, 2010
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  WANAJF hebu tutizame busara na akili za hawa watu.Hivi nani mwenye akili na busara?nani mzalendo wa kweli?

  Mimi kama Makamba siwezi kusema lolote ila Kamati Kuu ya CCM ndio pekee inayoweza kukaa na kujadili mapungufu yaliyopo katika katiba na kutoa ushauri kwa serikali,''alisema na kuongeza: "Lakini Serikali ni CCM na CCM ndio Serikali, hivyo kukiwa na lolote, lazima chama kijadili kwanza kiundani na baadaye kupeleka mapendekezo serikalini kwa ajili ya utekelezaji.

  " Makamba alitoa kauli hiyo kujibu hoja la Mdhamini wa CCM, Peter Kisumo ambaye alitaka CCM itolee kauli suala hilo na isiogope kuongoza mjadala wa katiba kwani suala hilo sasa limeshakuwa la jamii.

  "Tunaheshimu mawazo ya mzee wetu Kisumo kwani ikilazimika CCM tutakaa na kujadili hili suala kiundani na kama vipi ndugu yangu tutatoa tamko kama tulivyoshauriwa "alisema Makamba. Juzi mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini la Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kisumo, alikitaka chama hicho kutoa tamko linaloonyesha msimamo wake kuhusu mjadala huo.
  Kisumo alisema CCM haipaswi kuogopa kuongoza mchakato wa mabadiliko ya Katiba kwa kuwa mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa yaliyotokea nchini tangu mwaka 1977, yanalazimisha kuwapo kwa Katiba mpya.

  Kisumo, aliitahadharisha CCM na kuitaka iitazame vizuri agenda ya mabadiliko ya Katiba vinginevyo itaonekana ni agenda ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kukipa umaarufu wa bure chama hicho.

  “Tusiogope suala la kuleta mabadiliko ya Katiba na mimi naitahadharisha CCM kama haitakuwa msitari wa mbele kuongoza agenda hii basi itaonekana ni agenda ya Chadema kama ilivyotokea katika suala la vita ya ufisadi,”alisema Kisumo.

   
 2. J

  JokaKuu Platinum Member

  #2
  Dec 30, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,747
  Likes Received: 4,967
  Trophy Points: 280
  ..wote inaonekana hawana idea na nini kinatakiwa kufanyika.

  ..kinachotakiwa ni katiba inayoendana na mazingira ya sasa hivi ya Tanzania, na itakayokuwa na manufaa kwa wananchi wote.

  ..suala la chama gani kinaongoza, au chama kipi kipo juu ya mwenzake, mchakato wa majadiliano hayo halina msingi.

  ..wananchi tungependa ushirikiano baina ya vyama vya siasa ktk mchakato mzima wa katiba mpya.
   
Loading...