Nani mvumilivu sasa....kati ya mwanaume na mwanamkeke? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani mvumilivu sasa....kati ya mwanaume na mwanamkeke?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by chrispin2008, Jan 9, 2009.

 1. c

  chrispin2008 Member

  #1
  Jan 9, 2009
  Joined: Dec 12, 2008
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimeshuhudia kuona mara nyingi katika mahusiano Mwanaume akiwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamke mwingine, huwa mwenzi wake anaweza msamehe ila kwa sisi wanaume ukigundua mwanamke wako anauhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwingine ni fujo,wengine mangumi,visu...mbaya zaidi kama ni ndoa unatoa talaka fasta .....HII NI SAWA JAMANI....NANI MVUMILIVU?
   
 2. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #2
  Jan 9, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,587
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Ndiyo nature ya wanaume, kwa upande mwingine kabla ya kutenda lazima umfikirie mwenzio, kama ingekuwa wewe umefanyiwa ungekubali? Ubinafsi kwa wanaume umetawala sana tujaribu kupuguza
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Jan 9, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,838
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 145
  Mwanamkeke ndiyo nani?
   
 4. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #4
  Jan 9, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,644
  Likes Received: 1,669
  Trophy Points: 280
  Kuna tofauti kati ya kusamehe na kuvumilia. Naona kama vile unachanganya. Kwenye title unazungumzia kuvumilia lakini ndani unazungumzia kusamehe. Mtu anaweza kuwa na vyote viwili au asiwe na vyote au akawa na kimojawapo tu. Sidhani kama hili linategemea na jinsia ya mtu bali imani, malezi, ukomavu (maturity),uzoefu, jamii inayokuzunguka, msukumo rika nk,nk.

  Wakati mwengine uvumilivu unatokana tu na kutokuwa na mbadala (alternative, option). Mwanamke anaweza kuamua kuvumilia kwa sababu tu 'anaamini' hana pa kwenda au hata kama akiachika hawezi kupata mwengine nk. Lakini kamwe hili halina maana kakusamehe kwa uliyomfanyia!
   
 5. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #5
  Jan 9, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,254
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 0
  lolz
  frankly speaking madume hatuvumilii hata chembe.....mimi binafsi namiliki password ya email zake,from thursday mpaka j3 simu zote zinazoingia kwake nime divert kwangu.....hana password zangu na n.k...
  hii sio mfumo dume ni jinsi gani ninavyomjali na anapenda kweli kweli
   
 6. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #6
  Jan 9, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,644
  Likes Received: 1,669
  Trophy Points: 280
  Kwa kuchukua password na kufanya diversion unataka ku-achieve nini? Are they reliable controls? Wanawake wengi ni wajanja sana kuliko unavyoweza kudhania. Jaribu kumfuatilia mkeo kwa karibu na pengine utagundua kwamba an email address zaidi ya moja na SIM card zaidi ya moja. Just sneak into her purse and you will surely be suprised:). But dont panic!
   
 7. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #7
  Jan 9, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 70,455
  Likes Received: 28,294
  Trophy Points: 280
  Aisee me I don't play y'all. It's one and done! My BS threshold is low.....
   
 8. A

  Aunty Lao JF-Expert Member

  #8
  Jan 9, 2009
  Joined: Jul 7, 2008
  Messages: 215
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  SMU umenikuna sanaaaaaaaaaaaaaa. That is very positively true. Kwa kweli tena kwa mwanamke ni vizuri umuache na uhuru wake kwa kutumia akili za ziada.
   
 9. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #9
  Jan 9, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,907
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145

  Yoyo, heshima yako mzee,

  Lakini unajua kwamba bahari haichungwi. Wewe utaweka doria huko kwenye simu wakati wengine wanavua sehemu nyingine. Chukulia pirates wa somalia na majeshi ya kimataifa vivyo hivyo ndo ilivyokuwa tabu kumchunga binadamu.

  Najua wajirizisha unless pia ubongo wake umeuwekea password kwenye sehemu ya kuifadhi mafaili ya kumbukumbu!!
   
  Last edited: Jan 9, 2009
 10. Netanyahu

  Netanyahu Senior Member

  #10
  Jan 9, 2009
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Katika vita wanawake huwa ni wavumilivu watumiao akili kuliko wanaume.Mfano ukivurumisha kombora katikati ya jiji ndani ya dakikia ishirini waweza kuta wanaume wote wametoroka jiji kwa spidi ya mwewe na wameshavuka kigamboni lakini utawapata wanawake wengi bado wapo.

  Sababu ya wanawake wengi kufa kwenye vita ni uvumilivu.Hawakubali kutoroka bila kuhakikisha watoto wao wako salama na huwakusanya watoto ndio wakimbie.

  Wanaume kukitokea mashambulizi mfano ya mabomu au risasi ni wabinafsi hukimbia wao na chupi zao tu kama walikuwa hawajavaa nguo na hujali roho zao tu hawajali mke yuko wapi wala watoto wako wapi mabomu yakirindima.Mwanamke kawaida lazima ahakikishe si usalama wake tu bali na wa wanae pia.Hakubali kutoroka eneo la vita bila wanae.Mwanaume yuko tayari kutoroka hajali kuna mke wala mtoto yeye ni kukimbia tu.

  Hata maisha yakiwa magumu wanaume wengi hutelekeza mke na watoto.Lakini wanawake ni nadra sana kuona wametelekeza watoto wao eti sababu hali ya maisha ni ngumu.Watoto waliotelekezwa na wanaume ni wengi kuliko waliotelekezwa na wanawake.

  Hata Obama alitelekezwa na baba yake lakini mama yake hakumtupa japo maisha yalikuwa magumu.Nadhani wanawake ni wavumilivu hasa wale waliozaa na wenye watoto kwa vigori ambao hawana mtoto sina uhakika na uvumilivu wao after all wavumilie nini wakati wanawaka na soko bado lipo linaloweza kumaliza tatizo alilonalo kwa nini avumilie wakati ufumbuzi upo usiohitaji kuvumilia?
   
 11. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #11
  Jan 9, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,275
  Likes Received: 353
  Trophy Points: 180
  Mwanamke ni mvumilivu,kinachofanya mtu amtaliki mkewe fasta most of the time ni jazba lakini naona kusameheana ndio soln.
  Bse ukiangalia hata wewe waweza kuwa unagonga nje mwenzio akigongwa unamind?
  Kwani ulikuwa unagonga mawe si wake au wachumba za watu.
  Ila uaminifu jamani tujitaidi ingawa ni ngumu
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  Jan 9, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 60,317
  Likes Received: 39,559
  Trophy Points: 280
  Ni swali rahisi sana hili. Wanaume wengi wetu hatuna uvumilivu hata kidogo tunapogundua mke au gf ametembea nje. Hii mara nyingi ni chanzo cha mwisho wa ndoa au mahusiano ya kimapenzi na GF, lakini ni tofauti na wenzetu. Wanawake wengi huweza kusamehe na ndoa au mahusiano yakaendelea pamoja na kuwa kuna dosari kubwa imeshaingia katika ndoa au mahusiano hayo ya kimapenzi.
   
 13. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #13
  Jan 9, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,254
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 0
  Mkuu hapana shaka kwa kweli nakaba niwezavyo lakini nakuambia poa tu bora nikabe nikipigwa kanzu nikubali mpigaji kyanzu kanizidi
  Mkuu nachunga changu....ni kweli ana email nyingi ambazo sizijui lakini wigo wangu nakaba kama Nsajigwa
  Nyie hamna akili mnaitaji kuchungwa mwalimu wenu kafariki zamani
   
 14. M

  Monie Member

  #14
  Jan 23, 2009
  Joined: Sep 22, 2007
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanawake ni wavumilivu kuliko wanaume, wanaweza kuvumilia waume zao walevi, wagomvi, wabahili, wazinzi n.k.
  Ukitaka kujua kuwa wanume hawana uvumilivu hata mkiwa katika tendo la ndoa once anapoanza kumaliza yeye utasikia anakoroma hamjali mwenzie kama kafika au laa, lakini kwaa uvumilivu mwanamke anajilalia huku akisikitika. Lakini iwapo mwanamke atamaliza kabla halafu amwambie mwanaume basi ugomvi huo utaamuliwa na Baba Paroko.
  Hata huyo aliyesema kuwa anayo passwod ya mke wake na simu anajidanganya kwa kusema eti anaonyesha anavyomjali. Kama kweli anamjali angempa mkewe password yake na simu pia . Kwa kuhitimisha wanaume sio wavumilivu hata kidogo na ni WABINAFSI SANA.
   
 15. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #15
  Jan 23, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,061
  Likes Received: 467
  Trophy Points: 180
  Mada nzuri sana na mwisho wake Mwanamke ndiye mvumilivu zaidi ya mwanaume.

  Wanaume ni wababe na wabinafsi sana. Akifanya kosa ambalo na wewe utalifanya kukusamehe ni ngumu sana japo wakati yeye alifanya ulimsamehe mkaendelea na maisha yenu ya kawaida.

  Pia mwanamke hachungwi na hutamuweza maana akili,maarifa na ujanja alionao hutajua anafanya nini. Utahangaika weee kumpekua lakini mume mwenzio hutamjua.
   
 16. A

  Aunty Lao JF-Expert Member

  #16
  Jan 23, 2009
  Joined: Jul 7, 2008
  Messages: 215
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kabisa, wanawake wengi huwa wavumilivu sana, na uvumilivu huo naweza kusema hujengwa kuzuia aibu (ndoa imemshinda) katika jamii. Tumeumbwa na moyo ya kujali sana tofauti na hawa wenzetu. Ila pia wanaume hudhani pale mnapoombana msamaha yakaisha huisha, No, ili nayeye moyo wake utulie nilazima naye akabanjuliwe kiaina kimya kimya hata kama ni once in a life time kutuliza moyo tuu. Kwa kweli wanawake ni viumbe vyenye siri sana tena sana, samahanini kama ntakuwa nimewagusa hapa...ila huo ndo ukweli wa hivi viumbe. Ukimkuta mwanamke anaenda kurevenge openly basi huyo ni pungwani na hajafundwa. Maana ndoa nyingi za sasa hivi ni BORA NDOA na sio NDOA BORA. asanteni.
   
 17. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #17
  Jan 24, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,981
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0

  esp wanaume wetu wa ki tz, nashindwa kuelewa mtu umejitoa kwake kwa kila kitu, umempa pendo lako lote still anakutenda, nashindwaga kuelewa kabisa, wao kufanya wanaona ni sawa, cc ndio kama hivyo tena hata akihisi tu ni balaa.
   
 18. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #18
  Jan 24, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,981
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  mimi nilipata misukosuko ya mr kwa muda wa kama miezi 3 hivi nikamwacha afanye aamualo, kichwani nasema haitazidi miezi 6 kama hajajirekebisha kila 1 achukue ustaarabu wake, na nilivumilia hivyo coz nilikuwa sitaki kutoka kwangu (mimi na yeye) then nirudi kwetu au niingie kwenye nyumba za kupanga, nilivumilia nimalize nyumba yangu niingie kwangu, na hapo kunirudisha kwake ingekuwa tabu, bahati nzuri alijirudi, hapo mimi nilivumilia mateso/shida na kudharaliwa kwa ajili ya hiyo tu nothing else, na wakati huo alinifundisha mengi sana ambayo sikuwahi kufikiria kichwani,1 wapo ni kipoozeo.
   
 19. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #19
  Jan 24, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,712
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  ...Interesting; Wazo la kuwa na KIPOOZEO lingekusaidiaje kwenye shida ulizokuwa nazo?
   
 20. A

  Aunty Lao JF-Expert Member

  #20
  Jan 24, 2009
  Joined: Jul 7, 2008
  Messages: 215
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Tena unapokuwa na shida kipoozeo ndo mda wake muafaka... maana nadhani kisingekuwa hicho kipoozeo asingeweza kuvumilia hio miezi mitatu. Tena ntakuja chumbani kwako(PM) unipe stori zaidi na kuelimishana zaidi. Tusiwape wanaume uhondo...!
   
Loading...