Nani mtetezi wa wakulima na wafanyakazi

mams

JF-Expert Member
Jul 19, 2009
614
30
Katka mfumo wa chama kimoja and backwards wakulima na wafanyakazi ni makundi makubwa yaliyotetewa na chama tawala.

Kwenye bendera ya ccm kuna jembe na nyundo ikiwa ni alama ya jembe kwa mkulima na nyundo kwa mfanyakazi.

Kundi la wafanyabiashara halikuwepo na kama lilikuwepo basi kalikuwa ni kasehemu kadogo ndani ya wafanyakazi.

Wakati ule 80s and backwards waliokuwepo wanajua maisha ya wakulima na wafanyakazi yalivyokuwa mazuri.

Jaribu kulinganisha kipindi kile na sasa utajua makundi haya mawili hayana mtetezi.

Kundi kubwa lililopo na linaneemeka ni la wafanya biashara na ambapo kuna ukaribu sana na wanasiasa. Kuna nini hapa?

Nionavyo mimi ukaribu wa wanasiasa na makundi yale mawili ya awali ni muafaka kwa maendeleo ya nchi yetu, lakini ukaribu wa wanasiasa na wafanyabiashara ni hatari sana na ndiyo zao kuu la ufisadi. Karibuni!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom