Nani msimamizi wa Katiba ya nchi kuhakikisha haivunjwi na kuchezewa?

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
3,086
4,881
Wadau mimi sina Uelewa mpana wa Masuala ya Katiba ya nchi, nimeamu nililete Kwenu Suala hili ili nijifunze juu ya usimamizi
wa katiba ya nchi.

Swali langu ni:
Je, ni nani mwenye mamlaka kisheria ya kuisimamia katiba ya nchi ili kuhakikisha haivunjwi na kuchezewa? na iwapo itachezewa atachukua hatua gani?
 
Wadau mimi sina Uelewa mpana wa Masuala ya KATIBA ya NCHI Nimeamua nililete Kwenu Suala hili ili nijifunze juu ya USIMAMIZI
wa KATIBA ya NCHI.
Swali langu ni:
JE NI NANI MWENYE MAMLAKA KISHERIA ya KUISIMAMIA KATIBA YA NCHI ILI KUHAKIKISHA HAIVUNJWI NA KUCHEZEWA? Na Iwapo itachezewa ATACHUKUA Hatua Gani?
Mahakama! sasa ndiye huyo Ibrahim Juma alimuogopa Jiwe kuliko anavyomuogopa Mungu
 
18 (1) katiba wananchi ndio msingi wa mamlaka yote . viongozi wote watapata mamlaka yote kutoka kwa wananchi . Tatizo wananchi hawajielewi kuwa wao ndio wenye mamlaka yote .
 
18 (1) katiba wananchi ndio msingi wa mamlaka yote . viongozi wote watapata mamlaka yote kutoka kwa wananchi . Tatizo wananchi hawajielewi kuwa wao ndio wenye mamlaka yote .

Hiki kifungu kiko kinadharia, kiuhalisia rais ndio anaamua katiba itekelezwe vipi.
 
Kila aliyetamka maneno "nitailinda na kuitetea katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama ilivyowekwa kwa mujibu wa sheria".
  • rais, wabunge, maofisa wote wa jeshi, maofisa wote wa idara ya usalama wa taifa, majaji wote n.k
  • mwananchi yeyote mwenye mapenzi mema na nchi kwa kutumia njia halali ya mahakama.
 
Wadau mimi sina Uelewa mpana wa Masuala ya KATIBA ya NCHI Nimeamua nililete Kwenu Suala hili ili nijifunze juu ya USIMAMIZI
wa KATIBA ya NCHI.
Swali langu ni:
JE NI NANI MWENYE MAMLAKA KISHERIA ya KUISIMAMIA KATIBA YA NCHI ILI KUHAKIKISHA HAIVUNJWI NA KUCHEZEWA? Na Iwapo itachezewa ATACHUKUA Hatua Gani?
Ni MAHAKAMA.
Lakini Mahakama iliyopo inaogopa mgongano na mihimili mingine yaani Serikali na Bunge.
Kwa hiyo haiwezi kutoa maamuzi ya kulinda Katiba yetu, watu wa mihimili hiyo wanaposigina Katiba na hata wanapojitungia sheria kandamizi na za kuvunja hata haki za raia na binadamu WAZIWAZI, kama ilivyokuwa kwenye awamu ya tano.
 
Wadau mimi sina Uelewa mpana wa Masuala ya Katiba ya nchi, nimeamu nililete Kwenu Suala hili ili nijifunze juu ya usimamizi
wa katiba ya nchi.

Swali langu ni:
Je, ni nani mwenye mamlaka kisheria ya kuisimamia katiba ya nchi ili kuhakikisha haivunjwi na kuchezewa? na iwapo itachezewa atachukua hatua gani?
Msimamizi wa katiba ni mvunjaji katiba Kama alivyo msimamizi wa sheria ndiye huyo mvunjaji wa sheria yaani CCM Na serikali zake
 
18 (1) katiba wananchi ndio msingi wa mamlaka yote . viongozi wote watapata mamlaka yote kutoka kwa wananchi . Tatizo wananchi hawajielewi kuwa wao ndio wenye mamlaka yote .
Kuna wengi sana hawafahamu kuwa kupata HAKI, ni haki yao/zao kwa mujibu wa Katiba na sio zawadi wala msaada kutoka mtawala.
 
1.Rais wa JMT
2.Viongozi wa serikali ya JMT
3.Watendaji/watumishi wa serikali ya JMT
4.Raia wote wa JMT
#1,2&3 wanapaswa kua mfano mwema kwa #4
 
Kila aliyetamka maneno haya wakati wa kula kiapo: "nitailinda na kuitetea katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama ilivyowekwa kwa mujibu wa sheria".
  • rais, wabunge, maofisa wote wa jeshi, maofisa wote wa idara ya usalama wa taifa, majaji wote n.k
  • mwananchi yeyote mwenye mapenzi mema na nchi kwa kutumia njia halali ya mahakama.
 
Ni wenye katiba yaani wenye nchi (wananchi).

Lkn kwa kuwa wananchi wa Tanzania ni mazoba ndiyo maana inavunjwa lkn tumetoa macho tu.
 
Wadau mimi sina Uelewa mpana wa Masuala ya Katiba ya nchi, nimeamu nililete Kwenu Suala hili ili nijifunze juu ya usimamizi
wa katiba ya nchi.

Swali langu ni:
Je, ni nani mwenye mamlaka kisheria ya kuisimamia katiba ya nchi ili kuhakikisha haivunjwi na kuchezewa? na iwapo itachezewa atachukua hatua gani?
Mahakama ndio yenye Mamlaka ya kuilinda Katiba na Sheria zote za nchi. So, kama kuna ukiukaji wa Katiba ya nchi basi anayeona kuna uvunjaji wa ibara fulani anaweza kupeleka shauri mahakamani kuitaka ikemee kitendo hicho.
 
Nafikiri ni rais ndo anaapa kuilinda na kuisimamia katiba, au la wananchi wanamwajibisha kwa kutoiheshimu katiba.....kama spika kavunja katiba na yeye anawajibishwa na wananchi walewale kupitia kwa wabunge, kama jaji mkuu kavunja katiba yeye anawajibishwa na jopo la majaji lakini atakayeanzisha huo mchakato ni rais wa nchi...
 
Nakumbuka Hayati Baba wa Taifa alikuwa Anaweza kumkemea yoyote aliyethubutu kuvunja Katiba je kwa Sasa Itokee Mhimili mmoja umevunja Katiba ina maana hakuna Mhimili unaoweza kukemea?
 
Back
Top Bottom