Nani msemaji wa elimu aliyebaki Bungeni? Naona walimu wa private wananyanyaswa sana

Ikitotanzila

JF-Expert Member
Sep 22, 2020
1,409
2,263
Kuna shule flani kule Arusha inanyanyasa sana walimu na hakuna wa kuwasemea. Waajiri wanatumia kukosekana kwa ajili kunyanyasa walimu.

Hiyo shule ukiajiriwa tu unanyanganywa simu huruhusiwi kutumia kabisa, huruhusiwi kuingia na kitabu darasani, walimu wanavaa uniform kama wanafunzi, wanakula chakula cha ajabu; yaani uji wa wanafunzi, walimu wanafanywa mazezeta kabisa.

Mmiliki wa hiyo shule ni Mbunge lakini ananyanyasa sana wafanyakazi.

Vipindi vinaanzia saa kumi na moja alfajiri mpaka saaa mbili usiku mshara laki mbili.

Jamani waziri husika tembelea private schools jionee manyanyaso kwa walimu analau jaribu kuwatetea.

Shule inaitwa Nyahili Memorial School iko Arusha.
 
Private nyingi sasa hivi wanalipa laki 2 tu. Kuna dogo langu/ndugu yangu anafundisha Iringa shule ya mwana CCM mmoja inaitwa KITWIRU SEKONDARI analipwa laki 2 tu. Tena kazi ni saa moja asubuhi hadi saa 11 jioni.

Waalimu wanapata tabu sana wasio na ajira.
 
Tatizo la ajira na wingi wa walimu mitaani vimewapa viburi sana wamiliki wa shule binafsi. Hayo ya kunyang'anywa simu na kuvalishwa uniform sio huko Arusha tu. Hata hapa Dar Nenda Libermann ukaone wanavyovalishwa uniform.

Kwa kweli hali ni mbaya sana.. Walimu wanatumikishwa muda mrefu sana bila kulipwa overtime. Wakati mwingine wanafanya kazi mpaka Jumamosi na Jumapili kwa malipo madogo.

Inasikitisha zaidi pale ambapo unakuta hata malipo yao ya mifuko ya hifadhi za jamii hayawakilishwi, bima za matibabu hawana. Ukihoji unafukuzwa kazi mara moja. Mamlaka zinazohusika hebu ziwaangalie hawa wenye shule binafsi jamani. Huu ni unyanyasaji uliopitiliza.
 
Una hoja genuine kabisa.

Walimu private sector wananyanyasika sana.

Hii nchi sio kwenye elimu tu, private sector kwa ujumla ina mateso sana. Watumishi wengi wa private sector wanalipwa mshahara kwa shida sana na kwa manyanyaso makubwa.

Watu wanakaa hadi siku 90 hawajalipwa mshahara.

Hii nchi mfumo wa ajira rasmi nje ya ajira za serikali bado una changamoto nyingi sana ndio maana kila mtu anatamani kuajiriwa serikalini ambapo ingawa mshahara ni midogo ila ina uhakika wa kupatikana.

Private sector sehemu kubwa mishahara midogo, uhakika wa kulipwa haupo, uhakika kua mwezi ujao bado utakua mfanyakazi wao haupo. Tabu tupu.
 
Mfumo wenyewe umeishajifia. Nashangaa kuona vyuo vinaendelea kufyatua walimu, wakati mtaani wamefurika hawana pa kwenda.
 
Mshahara ni mapatano baina ya mwajiri na mwajiriwa, kama mlipatana mlipane laki mbili, hapo hakuna cha kulaumu.

Kuhusu kuvalishwa uniform kwa walimu nako sioni tatizo, ni sehemu ya taratibu za shule husika, huwezi kumpangia mmiliki wa shule na hakuna tatizo lolote ikiwa lengo ni unadhifu wa walimu. Ni mambo ya nidhamu tu. Askari polisi, mgambo, jeshi na magereza wanavaa uniform na huoni wakilalamika popote.

Ushauri wangu kwa wahusika ni kujitafakari kama wana sababu ya kuendelea kufanya kazi katika taasisi ambazo wanaona zinawapunja. Dawa ni kuacha kazi na kwenda kufanya mambo mengine. Walimu msiendelee kuwa wajinga na wanyonge, hakuna mtu wa kuja kuwasaidia au kuwaonea huruma, pambaneni na hali zenu.
 
Hii fani aisee! Ingawa waweza kukuta bora hata hao wanaondoka na laki mbili serikalini mwalimu mshahara (take home) anaweza ambulia laki moja tu kutokana na madeni kwani wakipatacho hakiendani na uhalisia hivyo kujikuta kuingia kwenye kukopa tu!
 
Kwani huyo mheshimiwa mbunge mmiliki wa hiyo shule huko bungeni kwa siku kama posho anaramba bei (kwa lugha ya kariakoo) gani?
 
Private nyingi sasa hivi wanalipa laki 2 tu. Kuna dogo langu/ndugu yangu anafundisha Iringa shule ya mwana CCM mmoja inaitwa KITWIRU SEKONDARI analipwa laki 2 tu. Tena kazi ni saa moja asubuhi hadi saa 11 jioni.
Waalimu wanapata tabu sana wasio na ajira.
Hao watakuwa hawajaajiriwa,wanafanya kiti kinaitwa"Tempo"....ilikuaga 80 elfu. Kama ni laki 2 basi imepanda sana.
Hakuna mwalimu mwenye akili timamu ana diploma au degree yake akapokee laki 2 mshahara. Hao wanajitolea tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huko private shida ni kuwa wamiliki wengi wa shule ni wabubhe na watumishi wa serikali ambao ni makada watiifu wa CCM kwa hiyo wanasigina haki zenu kwa sababu wanajua hamna pa kuwapeleka.

Kuna mikataba ya hovyo sana huko, watu wanafukuzwa kazi bila kufuata utaratibu, michango yao haipelekwi NSSF na mbaya zaidi wanafanyishwa kazi overtime na hakuna malipo ya ziada.
 
Mshahara ni mapatano baina ya mwajiri na mwajiriwa, kama mlipatana mlipane laki mbili, hapo hakuna cha kulaumu.

Kuhusu kuvalishwa uniform kwa walimu nako sioni tatizo, ni sehemu ya taratibu za shule husika, huwezi kumpangia mmiliki wa shule na hakuna tatizo lolote ikiwa lengo ni unadhifu wa walimu. Ni mambo ya nidhamu tu. Askari polisi, mgambo, jeshi na magereza wanavaa uniform na huoni wakilalamika popote.

Ushauri wangu kwa wahusika ni kujitafakari kama wana sababu ya kuendelea kufanya kazi katika taasisi ambazo wanaona zinawapunja. Dawa ni kuacha kazi na kwenda kufanya mambo mengine. Walimu msiendelee kuwa wajinga na wanyonge, hakuna mtu wa kuja kuwasaidia au kuwaonea huruma, pambaneni na hali zenu.
Hii kisu imekata kwenye mfupa, hao walimu wanaofanya kazi kwa munung'uniko wajitathimini, upya!
 
Back
Top Bottom