Nani msemaji wa CHADEMA katika masuala ya kiintelijensia? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani msemaji wa CHADEMA katika masuala ya kiintelijensia?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanajamii, Jul 23, 2012.

 1. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #1
  Jul 23, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Nakumbuka tuhuma mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo kuhusu kutaka kuhujumiwa ama na Chama tawala au Serikali, matamko yake yamekuwa yakitolewa na katibu mkuu wa CDM, Wilbroad Slaa au Mwenyekiti wao Freeman Mbowe na wakati mwingine John Mnyika.

  Lakini hili la kwamba, kuna njama za kuingilia simu zao kwa kutumia mtambo wa waliosema kuwa umenunuliwa na mtoto wa kigogo serikalini limetolewa na mshauri wa chama katika masuala ya kiintelijensia, MABERE, NYAUCHO MARANDO.

  Ninavyofahamu mimi, tuhuma zote hizo ni za kiintelijensia. Iweje kila tuhuma itolewe na mtu mwingine badala ya mshauri wa kiitelinsia? Kitugani kimejificha hapa? Je haiwezekani kabisa kila mmoja wa viongozi kuonekana wataalamu wa kupika habari za uongo na kupewa nafasi yakufanya hivyo pindi wanapoona maji yamewafika shingoni?

  Marebe Marando ni mtu ambaye kwa muda mrefu sana amekuwa kimyan na kwa taarifa zilizopo ni kuwa alikuwa nje ya nchi kuhudhuria mafunzo zaidi ya kiusalama. Hivi haiwezekani kabisa kwamba yeye ndiye aliyetumwa na chama chake kwenda kuuleta mtambo huo ili kuingilia simu za watu wengine na kuonekana kuwa zimetoka kwao?
   
 2. R

  Raia Maskini New Member

  #2
  Jul 23, 2012
  Joined: Jul 18, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii kali! Wakuu toeni mchango kuhusu huyu, maana inaonekana naye anataka kuupotosha umma
   
 3. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,066
  Trophy Points: 280
  Unaju wewe, umejiinua ukajiinamisha, ukajiinua tena!!!...

  Marando alete mtambo kama huo serikali dhaifu ya JK ...iko wapi?

  Huo mtambo upitishwa boda gani ambayo serikali haina macho yake?

  Au ulikuja kwa kiroba kupitia holili?

  Mitambo kama ile hauziwi tu mtu binafsi hovyohovyo..........!!!  Gamba bwana lina watesa, vueni!!


  .
   
 4. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #4
  Jul 23, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Ndiyo maana ya great thinker, kaona hivyo yeye usibeze, linalowezekana kwa CCM, CDM washindwe wana nini? Hili linawezekana kabisa. Hivi kweli mbona huyu Marando kaibukia huku kwenye mitambo? ina maana hakuna masuala mengine ya kiintelijensia angweweza kuyatolea maelezo tangu aajiriwe na CDM?
   
 5. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #5
  Jul 23, 2012
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Ukisha jua msemaji then what ? Watanzania wa Ziwa victoria watakuwa wamepata meli ya abiria kama alivyo ahidi JK ?
   
 6. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #6
  Jul 23, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Tatizo lililopo sasa kwa vyama vyote ni kukosa mwenye sauti ya mwisho, jambo hili japo ni tatizo, lakini ni muhimu sana kutokea na mimi nachukulia tuko kwenye kipindi cha mpito kuelekea democrasia halisi. Yawezekana wasomi na wanazuoni wakaandika makala na kuweka kumbukumbu zenye uchambuzi yakinifu juu ya hali ilivyo sasa. Hali hii si kwa bahati mbaya hata kidogo. Tunachopaswa kuhakikisha ni kuminimise madhara hasa yanayotokana na vuguvugu hizi zinazoendelea. Intelijensia kwa uhakika kabisa imegawanyika kiimani, na kama walivyo biandamu wengine wao pia ni binadamu si mashine, hivyo basi kila mmoja anatamani penye matumaini mema. Hata hawa tunaowalaumu wanafanya visa hivi na vile viwe vya kusingiziana kisiasa au vya kutafuta utajiri waharaka haraka ni kutaka kupata matumaini mema. Wakati mwingine mtu huchagua kupigana kwakuwa angependa kuishi vema na anaona mwingine anamzuia, yaani ameingilia amani yake moyoni na dawa yake ni kumuadhibu, ila wengine hupendelea kutumia bisara zaidi kwa kumshawishi kubadilika yule anaeingilia amabni ya mwenzake.

  Sishangai kabisa kama tuhuma hizi zikawa ni za kweli, lakini hali hii ina kila dalili ya kuonyesha ni jinsi hani vyama vinashughulika na kijisafisha na kila kimoja kimenasa kwenye mtego wa mwenzake.

  Sasa basi, si CHADEMA wala si CCM au chama chochote kile (kwakuwa kwa hulkja ya binadamu siwezi kushangaa kabisa kama kitaibuka chama kingine maarufu zaidi hata ya hivi vilivyopo, ilimradi tu kinaonyesha matumaini kwa watu) kitakachoweza kuepuka mikiki-mikiki iliyopo sasa. Tunachohitaji kwa sasa ni kiongozi ambaye anauwezo pia wa kiutawala anayeweza kubalance matumainin ya watu wote bila kujuali itikadi (natumaini Mabadiliko ya katiba yatatoa nafasi hiii). Kiongozi huyu anaweza kuwa chama chochote, ilimradi mtizamo wake uwe wa kichama na kuwatizama raia wote bila kujali itikadi zao na kuwapa uongozi na matumaini ya kubadilika kwa maisha yao.
   
 7. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #7
  Jul 23, 2012
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  marando ndio mkurugenzi mkuu wa usalama wa chadema.

  CHADEMA tuache kutafuta umaarufu kwa nguvu.HUU NI UBOYA! Ona sasa vifo vya watu
   
 8. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #8
  Jul 23, 2012
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  tirarira nyiiiiiingi,vitendo kidogo.marando badala ya kujibu hoja kwanini wameua iramba.anakuja na ngonjera zisizo chezeka.
   
 9. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #9
  Jul 23, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  kama una ushahidi CDM iliua Iramba nenda kaisaidie Polisi na cha kushangaza unasema CDM waliua Iramba mbona hata kesi walizofunguliwa sio za mauaji! Kweli vilaza kama wewe ni mzigo kwa taifa
   
 10. m

  mtemi mazengo Member

  #10
  Jul 23, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  napita tu
   
Loading...