Nani mmiliki wa kampuni ya YONO?

choupa moting

JF-Expert Member
Dec 27, 2016
1,508
2,553
Wadau,

Ni kitu ambacho najiuliza siku nyingi ila nakosa jibu. So leo nikaona si mbaya kubadilishana fikra na ndugu zangu.

Kuna hii kampuni ya YONO ambayo kwa sasa ndio imeaminiwa na serikali ya awamu ya tano kiasi kwamba kazi nyingi za madai ya kodi na mambo mengine yanayofanana na hayo wanapewa hawa jamaa kufuatilia.

Kwa siku za karibuni naona wamekua mastar wa mbele sana, mfano tumewaona wakifungia ofisi za Manji kwa kudaiwa kodi.

Wamefanya yao pale Bluepeal, jana tumeshuhudia wakiwa wanauza nyumba za Lugumi na hali kadhalika nimepata kuona taarifa yao kwamba wanataka kupiga mnada yale magorofa ya Kigamboni Dege.

So shauku yangu ni kutaka kujua ni mtanzania gani ambaye amebarikiwa kipindi kama hiki ana-flourish kilaini hivi?

Najua hakuna kinachoshindikana JF majibu nitayapata inshaallah.
 
KEVELA......ni kada pia! Ana juhudi za kutafuta maisha siku mingi tu hata kabla ya awamu ya tano! Mama Kevela alishindwa kura za maoni na Bonah Kalua
 
Kampuni ya Yono Auction Mart siyo ya siri. Inamilikiwa na Mbunge wa Zamani wa Njombe nini nini sijui, anayeitwa Yono Kevela. Mke wake anaitwa mama Kevela, ni kichwa usipime. Sasa uliza swali lingine.

Asante sana mkuu atleast nimepata kitu.
 
Hii Kampuni ni ya jamaa mmoja anaitwa Stanley Kevela, aliwahi kuwa mbunge kipindi cha nyuma kule Iringa. Huyu Mkurugenzi Scholastica Kevela ni mke wake. By the way YONO ni jina lake pia.

Huyu bwana namfahamu vizuri kwa sababu niliishi naye wakati Fulani akiwa anafanya mitihani ya board (I think ilikuwa ni board ya mambo ya supply not sure though) mimi nikiwa nafanya undergraduate pale Mlimani. His room was adjacent to mine.

Hii Kampuni ya Yono alikuwa ameishaianzisha Tayari na alikuwa anapiga pesa mdogo mdogo (maana boom likiwa halijatoka alikuwa ananipa bia moja moja mtaani). And I remember mke wake alikuwa anakuja kumtembelea akitoka kazini...... baada ya mda akamuachia majukumu ya ku-run day today activities za kampuni. Baada ya jamaa kutingwa na siasa na shughuli nyingine. Ingawa naona siku hizi karudi kuwa active kwenye kampuni.

Siwezi kujua kwamba labda kuna wakubwa wamenunua hisa kwenye hiyo kampuni au mengineyo (maana in TZ anything is possible). But YONO ni mojawapo ya kampuni iliyoanza na very humble beginning (kipindi hicho madalali wa kutisha mjini walikuwa akina Majembe auction marts). Yule bwana hiyo kampuni alitoka nayo mbali Kiukweli. So mimi sioni ajabu....maana hapa tunaongelea almost 15-20years. kwa hiyo hayo mafanikio yanaweza kuwa sahihi kabisa.

Anavyopata kazi za serikali Kiukweli sijui. Wengine wataongezea.
 
Mkuu you’re smart enough for this. Stay blessed.
 
Na ile nyingine Majembe Auction Mart inamilikiwa na familia ya Mwamoto akiwemo mbunge wa Kilolo Venance Mwamoto na kaka yake Seth Mwamoto ambaye ndiye anayeiendesha kwa sasa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom