Nani mkweli kwenye hili la uchawi kati ya FaizaFoxy na mshana jr?

Hahahaahahhaahahahah nchi ya viwanda asee itapatikana kweli ? wananch wanashindana nani anaijuwa miziziology ?

Hahahahah sasa hapa mwanga zaid ya mwenzake ni yupi Faiza Foxy vs mshana jr

Aaa safari ni ndef sasa wanga washaanza kujitokeza

Jamani leo nimeshangaa sana nmesa uzi wa mkuu mshana jr kuhusu aina za uchawi wa wasambaa kumbe mshikaji kadanganya!!!huuu hapa uzi wa mshana na comment ya faiza amekweli kaumbuliwa siamn

Mshana jr:aina uchawi wa kisambaa

Kuna habari nyingi sana za uchawi wa kila kabila Hapa nchini,
Kule Tanga milimani kwa wasambaa kuna aina nyingi za uchawi lakini aina hizi Hapa ni noma acha kabisa
1; Zongo- uchawi huu unakaa machoni, mwenye nao akikuangalia tu utaumwa tumbo kufa, au akikiangalia chakula hata kipikweje hakiivi na kikiiva kinakuwa hakina ladha kabisa na watakaokila lazima matumbo yawaume sana halafu waharishe sana

2; Banyanyi; maana yake kuchonganisha, ukipigwa aina hii ya uchawi utagombana na kila mtu

Fuiza; yaani fifisha, aina hii ikikupata kila utakachofanya hakikamiliki au hakifanikiwi

Ushinga; huu huwekewa wanawake, ambazo waume zao wana wivu sana au ambao wana wasiwasi na wake zao kuwa wanacheat,
Mwanamke aliyewekewa ushinga akizini tu na mtu mwingine tofauti na mumewe mwanaume huyo hufa ndani ya masaa sita, na uuume wale husimama dede hata baada ya kufa.

Kutua nyungu; maana yake kuvunja chungu hii hufanyika sana misibani kwenye sherehe au penye mkusanyiko wa ndugu, Hapa anayefanya hivyo ni mtu ambaye anakuwa hajaridhika au kaudhiwa chochote hivyo husaga chungu na kunuizia na kumwaga ule unga wa chungu kwenye vyombo vya maji,.Yani kila atakayekunywa hayo maji hana maisha tena ni uchawi wa mass killings

Ndele; uchawi wa kukufanya mwanaume upendwe na wanawake

Huo ni baadhi tu...Wanajamii nina access ya kupata hiyo kitu mwenye kuhitaji tuwasiliane

Faiza foxy:comment iliyomuumbua mshana jr akakaa kimya bila kujb mapiga akilalamika eti hamlazimishi mtu kuamini

Uongo mwingine ni noma.

1. "Zongo" si uchawi "zongo" ni kijicho. Au jicho la hasadi, ambalo binaadam yeyote anaweza kuwa nalo na si lazima iwe uchawi. Hata kusifia kwa uzuri pia kunaweza kuwa ni zongo. Mzazi anaweza kumdhuru kwa zongo hata mwanawe kwa kumpenda sana tu.

Waislam ndiyo maana tunafundishwa kusema "Bismillahi, Ma sha Allah" kila tunapokiona au kukisifia kitu kizuri na tunakatazwa kusifia kitu kwa kushangalia au kustuka "Doooh" au "Du", tunatakiwa tusema japo "Ma sha Allah".

2) Banyanyi, hilo ni kabila moja la Wahindi wa India "Baniani".

"Baniani mbaya kiatu chake dawa" hakuna uchawi hapo, Ni kudanganyana tu.

3. "Ndele" = hayo ni majivu yanayotokana na maiti za watu kuchomwa na hutumiwa kwa mambo ya kichawi lakini si uchawi wenyewe kuwa unaitwa "ndele".

Unaitwa unga wa ndele.

Ukiwa muongo ukumbuke kuna watu wanayajuwa mengi zaidi yako.

Hivi jamn nani.mkweli hapa?karibuni
Nouma sana...inatakiwa huu mpambano uanze upya

Kila mtu anajua lake na kwa njia yake. wewe ukijua hili mwingine anajua lile. Faiza Foxy hajawahi kucomment chochote pasi kudhihaki, kukashifu ama kujitia ujuaji zaidi. Inawezakana akajua neno kwa maana moja na mwingine akajua kwa maana nyingine na wote wakawa sahihi. Kwa vile tu maana ya jambo linatofauti na maana uijuayo wewe haimaanishi ujuha, uongo ama ulimbukeni wa ulietofautiana nae. mshana jr
We itakua umeathirika na ulaji wa kitimoto,hivi kuna mtu anajadili vitu with evidence kama faiza?sidhani,acha chuki kama uko mweupe kichwani elewa kuna watu wanauwezo mzuri wa kufahamu mambo,hebu niandikie uzushi wowote ulioletwa na faiza ntaomba mods wanitoe milele

Back
Top Bottom