Nani mkali wa Rhumba, Fere gora, Fally Ipupa, Werrason, au Koffi olomide?

Mimi nakubaliana na wewe
Najiulizaga Sana mbona hapa tz huyu mwamba hawampagi shavu kuja kutoa Rhumba znazokonga kumtima!!?
Hata mimi huwa nashangaa sana kwa nini jamaa jina lake sio kubwa huku bongo. Ila ukipita kwenye mabaa nyimbo zake zinapigwa sana mfano Vita imana na 100 kilos na watu huzipenda sana ila hawajui kaimba nani.
 
Hapo mkuu uwe na woofer sea piano au home theater system sauti ya chini!!

Kwenye suala la Rhumba, sijaona kwa Sasa mkali ZAIDI ya Ferre!
Inaonekana unazijulia sana jinsi hizi kitu zinavyotakiwa kutendewa haki katika usikilizaji wake. Pembeni uwe na kakinywaji kako taratibu hapo lazima stress zote ziondoke kichwani
 
Kumlinganisa Koffi Olomide na kina Fere Golla ni dhambi kubwa sana. Fanya kitubio
 
wa afrika tunashida sana

Hayamambo yaliyomfanya chegwavala kufeli kuwakpmboa wakongo ,MTU mzima kama wewe unajua wazi kwamba taifa linahudhunika kuhusu MBOWE kubuniwa mashitaka harafu

Harafu unakuja na maswala ya starehe hapa

Sent from my TECNO F2 using JamiiForums mobile app
Wewe umefuata nini kwenye majukwaa ya starehe kama kweli uko na masuala serious tu?
 
Ferre Gola mkali wa Rhumba,Fally anachanganya sana.
Baba lao Koffi kwakweli yule ni kumuacha tu huwezi kufananisha na hawa new generation.
Kuna Heritier Watanabe dogo anajua sana aisee.
Hao wote wanafunzi wa Koffi.
Jamaa ana album toka miaka ya70- 80 huko ,siku hizi anakumbushia tu kisasa zaidi
Ni kweli kabisa Fally Ipupa sio mkali sana kwenye Rumba ni mzuri wa Sebene na Afro Pop [siku hizi].

Sijakuelewa hapo, nani ni mwanafunzi wa koffi?
 
Ingawa kwa kweli hawa watu sijui kama ni sahihi kuwalinganisha kwa sababu ni watu wa era tofauti. Ila twende na swali lako.

Kwangu mimi Congo kutokea miaka ya 1990, hawa ndio wanamuziki wenye kuimba Rumba ninao wakubali sana.

1. Koffi Olomide.
2. Ferre Gola.
3. Le Karmapa.

Fally mzuri sana kwenye sebene na kufuse AfroPop na Sebene. Ndio maana amemzidi Ferre ambaye anafanya zaidi traditional rhumba ambayo imepoteza umaarufu Afrika.
 
Hata mimi huwa nashangaa sana kwa nini jamaa jina lake sio kubwa huku bongo. Ila ukipita kwenye mabaa nyimbo zake zinapigwa sana mfano Vita imana na 100 kilos na watu huzipenda sana ila hawajui kaimba nani.
Ferre anafanya traditional rhumba, ambayo imepoteza umaarufu afrika. Mimi ndiye Fav rhumba artist wa sasa. Sikiliza Ekoti ya Nzube. Bonge ya rumba.
 
Back
Top Bottom