Nani mkali kati ya Haruna Niyonzima na Clatous Chama?

Huyu alichangia sana kuwavusha kwenye moja ya hatua muhimu kwenye CAF CL
Chama ndiye mfungaji wa goli....
Na sio kufunga goli tu alicheza vizuri sana.
Hatudharau mchango wake kwenye kuanzisha move ya goli, ila chama ndiye alituvusha.
Chama ndiye alitupeleka makundi,
Kiufupi Niyo hana Alama aliyoiacha Simba, yeye kwa simba sawa na Rashid Juma tu.

Tulivyoenda mazembe away, Niyo ni kati ya waliocheza vibaya sana japo timu nzima ilicheza Ovyo.....

Alikuwa analazimisha kupiga vyenga vyake, matokeo yake alipokonywa hovyo tu.
 
Chama kawa mchezaji bora wa ligi

Chama alisaidia simba kufika robo fainali klabu bingwa

Chama alisababisha zikaenda team 4 makundi

Chama kaipa simba ubingwa

Tupeni sifa za huyo haruna
Haruna ameisaidia timu ya Yanga kubeba vikombe vya ligi kuu zaidi ya vinne.

Akiwa Simba ameisaidia kubeba VPL 2.

Pia amewahi kuwa mchezaji bora wa LIGI KUU wa Kigeni akiwa Yanga.

Akiwa Simba alifanikiwa kuisaidia timu kufika hatua ya ROBO FAINAL.
 
Chama kawafunga as Vita na kuwatoa group stage , kawafunga nkana au ndio vitimu vilivyopanda daraja. Kiuchezaji chama na niyonzima wote ni mafundi wa kuchezea mpira ila tofauti yao chama anacheza akitafuta kufunga au kutoa pasi ya mwisho anacheza mchezo hatari, niyonzima anacheza ili kufuraisha mashabiki ni mchezaji machachari
Kweli.. kiujumla Haruna huwa hatengenezi nafasi nyingi za kufunga
 
Kumfanisha tripple c na niyonzima nikulikosea heshima soka la tanzania...nadhan hata niyozima anajua makali ya daktari ndo maana akawa mchezaji bora msimu uliopita na msimu huu atachukua tena
Msimu huu yupo KISINDA na Carlinhos mkuu
 
Unataka kusema uwezo wa Niyonzima ni level ya Sure boy na sio Chama?
Hii si kweli mkuu...Haruna kwenye ubora wake ni bora kuliko Sure boy lakini si level za Chama...ni heri hata tungemdiscuss Chama na Kamusoko (Kampa kampa tena) kwenye ubora wake,ambaye alimuonyesha Haruna jinsi ya kucheza Modern football na kuchukua namba yake pale Yanga..
 
Kwenu wadau wa Soka

Haruna Niyonzima na Clatous Chama Hawa ni Wachezaji ambao Wamejibebea Umaarufu Mkubwa kutokana na Uwezo wao wa Kucheza Soka la KIWANGO cha Juu katika Ligi Yetu ya Tanzania.

Viungo Hawa wamekuwa wakiwapa Matumaini Mashabiki wa Timu zao hasa wanapoanza katika kikosi na kufanya Mambo makubwa ndani ya Uwanja na kupelekea Timu pinzani kuonekana Kama wanaonewa na Kunyanyaswa na Wachezaji hao.

= Leo Tujue Kati ya Clatous Chota CHAMA (Mwamba wa Lusaka) na Haruna Hakizimana NIYONZIMA (Baba mzazi)

JE, NANI NI MCHEZAJI BORA ZAIDI.

"Soka ni Mchezo wa Wazi"
Hapa Itakuwa hujamtendea Haki Haruna Niyonzima ambae kiwango chake kwa sasa ni cha chini.Utofauti wa nyakati unafanya usiwe mtenda Haki hata hivyo hata Haruna wa Kiwango cha Juu bado hajamfikia Chama kwa jambo lolote
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom