M Z A N Z I B A R I
JF-Expert Member
- Dec 15, 2015
- 21,690
- 117,083
tofauti na miaka ya zamani, hii kazi ya uchambuzi inachukuliwa userious zaidi kwenye kizazi hiki cha ukusanyaji wa takwimu kupitia pembe tofauti kwa kuangalia zaidi eneo la analysis na research.
dunia ya sasa mashabiki wanaojielewa hawahitaji kuhadithiwa na mchambuzi jinsi gani goli limefungwa bali wanachohitaji ni kudadavuliwa jinsi goli lilivyoanza kutengenezwa mpaka kufungwa kwake, jinsi timu X inavyocheza, kwa nini mchezaji yule amecheza vizuri na mwengine hakucheza vizuri, upi udhaifu wa timu X, kwa nini mlinzi yule ananusa harufu au mikimbio ya timu pinzani na mengineo yote yanayorekodiwa kwenye mitandao inayohusika na takwimu za kimpira.
hivyo wachambuzi aina ya george ambangile na wengineo wenye sifa hii huu ndio muda wao wa kuvuna mashabiki lukuki kupitia maeneo tofauti kwa sababu wanakupa kile ambacho wewe kama mshabiki/mtazamaji wa mechi umekikosa licha ya kujaaliwa macho mawili kama George.
sijawahi kumsikiliza au kumsoma huyo bwana Ally, kama atakuwa na sifa mfano wa hizo basi ni sahihi kumweka pamoja na george ila kama itakuwa ni kinyume chake kwa dunia hii haitokuwa sahihi kumlinganisha na george.
kwa sababu george ameshavuka kwenye dunia ya usimuliaji wa soka kama anavyofanya edo kumwembe, shaffih dauda na wachambuzi wengineo waliojijengea heshima tokea zamani ila wakashindwa kujiendeleza.
ila usisahau unaweza kuwa mchambuzi hodari wa mechi lakini ukawa kocha mbovu ndani ya touchline zinazopatikana uwanjani, mfano gary neville