Elections 2010 Nani kuukwaa uwaziri mkuu?

Status
Not open for further replies.
Well Pinda could be the ideal candidate anything can happen and may be Pinda could be weak in some areas as well
 
Magufuli mtendaji kweli,alimfunika JK ndo maana akatupwa kupambana na wakojani kwenye uvuvi!!
u no war i mean!!

Na isitoshe ilikuwa mikakati ya kumumaliza kisiasa apotelee kwenye vumbi, lakini kamanda bado anakamua kwa kwenda mbele! du mnyonge mnyongeni haki yake mpeni!
 
hata akimnyima magufuli ....hawezi kumzuia kuwa rais 2015

Inamaana CHADEMA haitachukua madaraka 2015? Mmh labda kama mwenyekiti Mbowe atakuwa hajakamata usukani. Unamfahamu lakini vizuri huyu strategist wa CHADEMA au unadhani kuwa KUB ameenda kula tu bata? Subiri uone!
 
SINA wasiwasi na utendaji kazi wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Benard Membe. Yeye ni miongoni mwa viongozi wachapa kazi hodari ambao taifa limepata kuwa nao.
Napenda kuamini pia kuwa Mheshimiwa Benard Membe ni miongoni mwa viongozi wetu wachache ambao utendaji kazi wao ulikwenda sambamba na kaulimbiu ya 2005-2010 'Ari mpya, Nguvu mpya na Kasi mpya'. Hii ni kaulimbiu ambayo iikuwa haizungumzwi sana kwa ari, kasi na nguvu kama ilivyokuwa ikisikika wakati utawala wa awamu ya nne ulioiasisi ulipoingia madarakani miaka mitano nyuma. Kwa nini? Kila mmoja wetu ana tafsiri yake

Anyway tuachane na hayo mimi nataka kujua Hii siri ya JK imevuja, ni kuwa BM amekuwa Waziri, source ni mbea wa ikulu

Kumbe source yenyewe ni kutoka kwa mbea wa Ikulu na sio mtu timamu alieko ikulu? Kimsingi ni taabu sana kumwamini mbea. Ila kama ni kweli huyo "mbea" kapatia na yuko sahihi basi mmhhh!!! kuna walakini. Mimi siamini sana uwezo wake wa kiutendaji ila nimesikikia sikia kele za 2015 na bwana Member ndani, sasa sijui. LETS WAIT AND SEE, TIME WILL TELL
 
pinda ni kweli anafaa, tatizo kubwa yeye ni mtaalamu wa kujibu maswali bungeni, kuchair vikao, kuzima vuguvugu kitaalamu bila mtu kujua kama kuna suluhisho au hakuna, mfano richmond, leo hii nikikuuliza hata yale mambo serikali iliyoambiwa ishughulikie we unajua yamefikia wapi? Pia ni mwadilifu

inapokuja utendaje wa nje wa hayo niliyotaja hapo jamaa hayupo kabisa, mpole mno. Lowasa ni mfuatiliaji mzuri ila tatizo lake uadilifu.

Dr magufuli yeye yuko kote kote, uadilifu, kupangua hoja kwa mifano na live data, na pia ni mfuatiliaji wa mambo. Pia hana jazba ya kugombeza watu hadharani. Tukitaka tz isonge mbele kote kote, dr magufu ni mtu sahihi kwa sasa. Ila kama tunataka mtu wa kupangua hoja na kujibu maswali vizuri bungeni pinda ni mtu sahihi kwa sasa.

Ila ujue wananchi wanataka zaidi ya hapo, kuona miradi ya serikali ikikamilika kwa wakati na pia kua na value of maney. Magufuli alipokua ujenzi, ardi, uvuvi na mifugo, amefanya kazi zinazoonekana.

Hii kazi mpeni dr magufuli, ccm itarudi 2015 bila kuweka mabango kama mwaka huu. Ila wakimwachia huyu aliyetoka theni wajiandae kuongeza budget ya mabango ya kampeni mara 4 zaidi ifikapo 2015.

Dr magufuli sii mchezo, jamaa alikua anafuatilia barabara, ujenzi umefikia wapi, ameziweka kichwani, anatoa tathmini zitaisha lini, wakandarasi wazembe walipigwa chini, samaki alikua anadeal nao mpaka watu wakazika nyavu haramu wakaweka na misalaba ukidhani marehemu kumbe nyavu za kuvulia samaki. Alishawahi kukamata magari mengi ya serikali yanayofanya shuguli binafsi, anapangua hoja kwa hoja.

Pia jamaa kasomea sayansi, na unavyojua science haihitaji longolongo ni facts tu, kwenye science hamna uongo kabisa.

Mpeni dr magufuli muone, mawaziri, wakurugenzi, wakuu wa wilaya+mikoa wataacha kunukia perfume/marashi na watachapa kazi, then wananchi nao watachapa kazi

huyu jamaa dr magufu, ni mtaalamu sana, alipopewa wizara ya ardi, cha kwanza alichokifanya alienda darasani zaidi ya miezi 3 kusoma seria za ardi na mabaraza ja miji/vijiji. Alipoanza kazi ardi palianza kua pasafi, sasa sijui aligusa maslahi ya wakubwa akuchukua muda pale akapelekwa mifugo na uvuvi, nako huko akafanya mambo, meli ilikamatwa hana utani na haina maana zilikua haziibi samaki ili waliokuwepo walikua hawafuatilii

ila sisiemu tunawajua, watafanya kituko, tusubiri.

umetumwa au umejituma?
 
So kwa hali iliyopo sasa hivi kwa jinsi watu walivyo bet hicho kiti cha uwaziri mkuu its between MAGUFULI, MEMBE, ANNA TIBAIJUKA, PINDA, MWANDOSYA maana haya ndio yamekuwa yakitajwa sana lakini lolote laweza kutokea na kuletewa mtu ambaye hatukumtarajia
 
Hapo kati ya hayo majina mawili ukinipa niotoe uamuzi moja kwa moja nitakwambia ni Magufuli. Mimi ninashagazwa sana wanaomshabikia Tibaijuka. Je kuna political history yoyote inayomwonyesha mama huyu kuwa ni wa shoka kama wengine mnavyodiriki kumtukuza.

Hata record ya kuanzisha BAWATA iliyokuwa tishio kwa UWT huikumbuki?
 
Sasa kama hawasalimiani wanafanyaje kazi, magufuli alikua napelekaje ripoti yake kwa jk au lowasa alipokua waziri mkuu


mzee gomezi
 
Ahaa, hebu acha masikhara, Membe awe PM, kwa lipi alilotufanyia Wa TZ. Huyu jamaa ni too arrogance. Kujipendekeza kwa sana. Atakuwa kama yule mzee Fred Suluwali ambaye alikuwa vuvuzela la BM. Simpendi Membe, hana mvuto wa kuwa PM. Its better akarudi Mizengwe ya Kupindapinda:A S angry:.
 
Magufuli anafaa kuwa PM....................................................Lakini atamfunika mshikaji Presidaaa wa serikali yetu ya kishikaji..................
 
Kwakuwa Chama cha chaka chua matokeo kilishaanzisha mpango wa kuwajali wakina mama, mpango wa kumpa u PM mama Tibaijuka kilikuwa sahihi.
Mama huyu ana uwezo mkubwa sana ila sijui kwa mafisadi kama angefanya kwa amani.

Nionavyo mimi, hata wakimpa Magufuli atafurukuta siku mbili then kimya. CCM au chama ni system na sio individual element, system ni muunganiko wa elements kibao zinazofanya kazi pamoja ili kufanikisha au kutimiza lengo/malengo fulani. Hivyo mimi najaribu kuangalia elements zinazo unda CCM na serikali kwa ujumula napata kigugumizi kuamini kuwa kuna mtu anaaweza akasimama yeye kama yeye ndani ya CCM na kuleta mabadiliko ikiwa Mkubwa wake ni mchafu(hapa ni JK), wenzake ni wachafu ni ngumu kwake, kukuru kakara za Sitta zimeishiwa wapi?

Nadhani tuseme kweli tu, kuwa mambo yatakuwa yaleyale, mbona tunazunguka mbuyu? Kuzunguka Mbuyu sio kazi, bali kuukumbatia Mbuyu ndio kazi, hebu tukumbatiye Mbuyu.

Natoa HOJA
 
Tibaijuka ni sleki sana, hii nchi inahitaji jembe ulaya ili iende. huyo mama aende wizara ya viwanda ambayo haina kazi, na viwanda tz hakuna. kilimo kwanza hakiwezi. she is too sleki for it, naye ataishia kulia tu bungeni bila kuchukua hatua kama Pinda. we are tired of it.
 
SINA wasiwasi na utendaji kazi wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Benard Membe. Yeye ni miongoni mwa viongozi wachapa kazi hodari ambao taifa limepata kuwa nao.
Napenda kuamini pia kuwa Mheshimiwa Benard Membe ni miongoni mwa viongozi wetu wachache ambao utendaji kazi wao ulikwenda sambamba na kaulimbiu ya 2005-2010 'Ari mpya, Nguvu mpya na Kasi mpya'. Hii ni kaulimbiu ambayo iikuwa haizungumzwi sana kwa ari, kasi na nguvu kama ilivyokuwa ikisikika wakati utawala wa awamu ya nne ulioiasisi ulipoingia madarakani miaka mitano nyuma. Kwa nini? Kila mmoja wetu ana tafsiri yake

Anyway tuachane na hayo mimi nataka kujua Hii siri ya JK imevuja, ni kuwa BM amekuwa Waziri, source ni mbea wa ikulu

Jamani jamani sasa kumekucha. Hata Membe anapigiwa chapuo?????? Tumwagie sifa zake unazozifahamu hapa. Mimi namwona 'zero carrier'. Tangu uhuru, sijawahi kumwona waziri mwoga na asiyeweza kutetea hoja aliyoitoa kama Membe. Jamani, tuache kukurupuka, yaani mtu akijisikia kuachilia thread anaivumisha tu!!
 
Mnahangaika nini kumjua PM nani? Kwa nini msimuuliza Ridhiwani? Anavyopenda ujiko atawaambia tu, si mnajua yeye ndio mshika furushi la Hirizi za Baba yake? Baba yake hana ujanja na hilo 'toto tundu'
 
Wacha uongo hizo habari ulizozipata wewe kutoka huko dodoma si sahihi... kwa taarifa yenu jina halijabadilika Pinda Mizengo kanda Peter a.k.a mtoto wa mkulima anaendelea na uwari mkuu kwa kipindi kingine cha miaka mitano kama utaendelea kuamini hivyo basi sikilizia hiyo saa kumi na moja
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom