Nani kumrithi Waziri wa Nishati na Madini Prof. Muhongo?

Kwa ufupi*.

Nafasi hiyo iliachwa wazi baada ya Profesa Sospeter Muhongo kung’olewa katika wadhifa huo Mei 24, kutokana na ripoti ya kamati maalumu iliyoundwa na Rais, kuchunguza mchanga wa dhahabu katika makontena 277.

By Daniel Mjema,Mwananchi dmjema@mwananchi.co.tz


Dodoma.

Rais John Magufuli, anatarajiwa kufanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri wakati wowote kuanzia sasa ili kujaza nafasiya waziri wa Nishati na Madini.


Nafasi hiyo iliachwa wazi baada ya Profesa Sospeter Muhongo kung’olewa katika wadhifa huo Mei 24, kutokana na ripoti ya kamati maalumu iliyoundwa na Rais, kuchunguza mchanga wa dhahabu katika makontena 277.


Kamati hiyo iliyoongozwa na Profesa Abdulkarim Mruma ilisema Kampuni ya Acacia, haikutangaza kiasi cha madini yote yaliyokuwa katika makontena 277 ambayo yalizuiwa kusafirishwa nje kwa amri ya Rais.

Matokeo ya kamati hiyo yanaonyesha kuwa thamani ya madini yote yaliyopo kwenye makontena 277 ni kati ya Sh829.4 bilioni na Sh1.439 trilioni, tofauti na thamani iliyotolewa na Acacia ya Sh97.5 bilioni.


Hii ni mara ya pili kwa Profesa Muhongo kung’olewa katika wizara hiyo. Januari 24, 2015 alijiuzulu wadhifa huo baada ya kuhusishwa na kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow ikiwa ni shinikizo la Bunge, baada ya kutolewa kwa maazimio ambayo pamoja na mambo mengine, yalitaka mamlaka ya uteuzi wake imwajibishe.


Vyanzo mbalimbali vimedokeza kuwa Rais Magufuli hana jinsi zaidi ya kufanya mabadiliko madogo ya baraza lake la mawaziri ili kujaza nafasi hiyo huku wanaofaa kumrithi wakitajwa.

Majina yanayotajwa kumrithi ProfesaMuhongo, ni pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi na Waziri wa Tamisemi, George Simbachawene.

Simbachawene aliwahi kuhudumu katika wizara hiyo akiwa naibu waziri,kabla ya kuukwaa uwaziri kamili Januari 2015 baada ya kujiuzulu kwa Profesa Muhongo.


Chanzo : Mwananchi
de12816147330fb4ccf2e81ab6a545ad.jpg
 
Dr medard matogoro chananja kalemani, naibu waziri wa nishati na madini na mbunge wa Chato ndiye atakuwa.
 
Apewe mwigulu maana wataalamu wapo naye anajuaga kujiongeza kifikra!! Pia anaonesha kujali rasilimali za Taifa kuliko masifa na kujirundikia utajiri
 
Kufuatia Rais Magufuli kumtaka Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo aachie ngazi kutokana na sakata la 'mchanga wa bandarini'.

Tutoe mapendekezo yetu wakuu ni nani anayefaa kumrithi maana hii Wizara ina changamoto siyo kidogo!


mzee hata awekwe nani kwa ccm usitegemee lolote la maana isipokuwa wizi tu
 
Kufuatia Rais Magufuli kumtaka Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo aachie ngazi kutokana na sakata la 'mchanga wa bandarini'.

Tutoe mapendekezo yetu wakuu ni nani anayefaa kumrithi maana hii Wizara ina changamoto siyo kidogo!



Atakayekuwa Waziri yafaa awe na sifa hizi:
1. Awe ni mtu mnyenyekevu,
2. Awe hana rekodi yeyote ya wizi, upendeleo wala ushirikina,
3. Yafaa awe MZALENDO na mtu ambaye kweli tukimwangalia na kufuatilia maisha yake, hakuna chembe ya shaka kuwa ni MZALENDO na mwisho,
4. Awe na uwezo wa kusimamia anachokiamini.

Hebu tuorodheshe majina ya wenye hizo sifa.
 
Huu ni ushauri ninaoupeleka kwa Mamlaka ya uteuzi ya Tanzania .

Nafahamu kwamba nafasi za uteuzi wa wabunge kwa mujibu wa katiba umemalizika , lakini chini ya ccm hakuna kisichowezekana , anaweza kuondolewa Bulembo ( hakuna anachofanya bungeni ) , na akarudishwa kwenye ile nafasi yake ya Mshauri wa Rais kwenye masuala ya uteuzi.

Nampendekeza Profesa Mruma kwa sababu ambazo kila Mtanzania anazifahamu , ile kazi yake " iliyotukuka " kwenye makontena ya mchanga ?

Huyu atatusaidia .

Naomba kuwasilisha .
 
Back
Top Bottom