Nani kazima mtambo wa luku siku ya iddi?

Status
Not open for further replies.

Alwaz

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,055
10,723
Katika kumbukumbu zangu tangu matumizi ya umeme kwa mfumo wa Luku yaanzishwe nchini sijawahi kusikia huduma hii kukosekana kwa siku tatu mfululizo kama ilivyokuwa kuanzia Agosti 29-2011.

Hii tarehe ilikuwa ni siku ya kuangalia mwezi baada ya mfungo wa Ramadhani 1432.Siku ya pili yake ilikuwa ni Iddi mosi kwa baadhi ya waislamu.

Matayarisho ya sikukuu hii hayakwenda vizuri kwa familia nyingi za waislamu.Msemaji wa Tanesco bi Badra Masoud alisema kulikuwa na tatizo la kiufundi na mafundi walikuwa wakiendelea na matengenezo hata hivyo maelezo yaliishia hapo tu.

Kwanini tatizo hili lilitokea msimu wa Iddi na kipi kilitokea hata mitambo hiyo ikashindwa kufanya kazi.

Jee haiwezekani kwamba ni visa vya kisiasa vilivyokusudiwa kuleta malalamiko na kuleta vurugu katika jamii?.
 
Tanesco waliruhusu maeneo yote kuwa na umeme bila mgao katika siku mbili za sikukuu, swali ni kuwa je umeme huo ulitoka wapi, msemaji wa tanesco alisema kwa kuwa viwanda havitakuwa vikifanya kazi, basi umeme hautakuwa na mgawo. swali? Je viwanda vyote vina line tofauti na makazi ya watu?.

Maoni yangu: itambo ya LuKU ilizimwa ili kubalance inadi ya watu watakao kuwa na umeme, idadi kubwa ya wanchi waliingia kwenye janga hili
 
Duh ni kero kubwa sana ile siku, si tulikaa siku 2 bila umeme, halafu nimesikia eti mpaka mwisho wa mwezi huu megawati 50 na 37 za symbion zinaingia kwenye gridi...duh hawa jamaa wasanii kinoma. Smthng wrong in this sector
 
lilikuwa igizo lingine Tanesco walitoa ofa kwa wenye salio

hapo sasa,...wale tunaonunua umeme wa elfu 20,30 mara 40,...ilikua ni maaumivu...mm vibia vyangu kwenye ka friji zilikua kama maji ya moto,..nilinuna sana
 
jamani mbona hayo ni matatizo ya mtandao
Matatizo ya mitambo !,mbona hayana maelezo.Mara nyingi kukiwa na uharibifu au marekebisho maelezo hutolewa na kuombwa radhi.Mbona safari hii kulikuwa na kuombwa radhi tu.
Kabla maelezo mimi natoa hisia zangu ambazo nimezipata mtaani kwetu.Kwamba eti kuna jamaa huko Tannesco mwenye chuki na uislamu aliyedhamiria kuwaudhi tu na hivyo kuchomoa utambi na kukimbia nao.Ndio maana akina Badra hawana maelezo.
 
Matatizo ya mitambo !,mbona hayana maelezo.Mara nyingi kukiwa na uharibifu au marekebisho maelezo hutolewa na kuombwa radhi.Mbona safari hii kulikuwa na kuombwa radhi tu.
Kabla maelezo mimi natoa hisia zangu ambazo nimezipata mtaani kwetu.Kwamba eti kuna jamaa huko Tannesco mwenye chuki na uislamu aliyedhamiria kuwaudhi tu na hivyo kuchomoa utambi na kukimbia nao.Ndio maana akina Badra hawana maelezo.

Hayo ni maneno ya uchochezi usio na tija
 
<b>Tanesco waliruhusu maeneo yote kuwa na umeme bila mgao katika siku mbili za sikukuu, swali ni kuwa je umeme huo ulitoka wapi, msemaji wa tanesco alisema kwa kuwa viwanda havitakuwa vikifanya kazi, basi umeme hautakuwa na mgawo. swali? Je viwanda vyote vina line tofauti na makazi ya watu?.<br />
<br />
Maoni yangu: itambo ya LuKU ilizimwa ili kubalance inadi ya watu watakao kuwa na umeme, idadi kubwa ya wanchi waliingia kwenye janga hili</b>
<br />
<br />
Kaka hujagundua tunatawaliwa na nyota ya SIASA? Huu ndio urithi pekee tulioachiwa na mfuga majini wa Magomeni Mwembechai
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom