Nani Katuloga watanzania??Dawa imepatikana na ni hii hapa

Gembe

JF-Expert Member
Sep 25, 2007
2,483
159
Ndugu wana Jf,

Baada ya jana mie kuhitimisha kuwalemisha watanzania kuhusu Mzee Ben kuachwa kuzomewa na kupanga nini kifanyike chenye manufaa zaidi kwa ajili ya watanzania,nilikaa chini na kuanza kutafakari ni nani kawaloga watanzania,na wakati mwingine naweza kukubaliana na maneno aliyowahi kuyasema Mkapa,kwamba watu wana wivu wa kijinga.na ningependa kuelezea Hoja yangu kwa mapana kwanini nilikuwa namtetea Mzee Ben,ila nilitaka zichukuliwe hatua mashubuti za kufuatwa kuliko kuzomea tu

Nianze na mfano wa kipindi kile watu waliposhinikiza Lowassa ajiuzuru Uwaziri Mkuu,Watananzaia tulikuwa mashabiki na tulipiga kelele ausbuliwe,na kweli akasurubiwa na kuachia ngazi akiwa na wanyang'anyi wenzake,Karamagi na Msabaha.,Jamabo la kujiuliza nini kilifuata baada ya kushabikia Lowassa aachie ngazi
1. Je Dowana hawalipwi pesa zetu yaani dola million 152 kwa siku.

2.Je Lowassa amechuliwa hatua zipi za kisheria kwa kuliingiza taifa katika hasara isiyosemelka,Maana Waziri Mkuu hana kinga ya kupelekwa Mahakamani

3.Je walioshiliki NGT ,kama watanzania tumeshafanya nini ili hawa watu wachukuliwe hatu kali ikiwemo kuwajibika kwa kuachia ngazi,Naomba nikueleze jambo ambalo haulifahamu, watu wote waliohusika na NGT wamebadilishwa vituo na kupelekwa sehemu Nyeti huko Ikulu,Hii maana yake nini??

Pili,Mhe. Chenge naye tulishabikia aachie Ngazi,kweli kwa kuombwa na muungwana aliachia ngazi nafasi yake ya uwaziri,ila tujiulize hii inatosha??Je ndio hicho anastaili au sie tuliunga mkono nia ya kundi flani ambalo lilitaka kumuangusha chenge kisiasa mpaka wakafikia kuzushiana kifo??Tutafakari sana mambo haya sababu tumekuwa watu wa kufuata mkumbu na kuogopa kuchukua hatua.Rejea wakati Mhe. Dk. Mwakyembe akiwasilisha ripoti ya kuhusu RDC alisema watanzania wamekuwa waoga kuellezea wanachokijua kuhusu tuhuma flani ,na hii ni kweli watu wamekuwa wazi kunong'oneza mtu flani jinsi mtu flani anafanya ufisadi wa khali ya juu,ila hawako tayari kuchukua hatua ya kumshtaki mtu huyo

Watanzania wenzagu ,leo mchana nilipoingia JF nilikutana na hoja ya mwanakijiji kuhusu gharama ya kuendesha JF imekuwa kubwa na watu hawako tayari kuchangia ila wako tayari kusoma habari na kutupa muelekeo wa wa ambao wanafanya ufisadi,ila inapokuja suala la kuchangia nini kiganyike watu wamekuwa wagumu,na hii ni moja ya tabia zetu watanzania.inawezakana tua uoga flani,Je tunasubiri nani atoe uoga huu tulio nao?nani achangie Jf kama siyo wewe mtanzania uliye na mkakati wa kuondoa umasikini??

Nimetafakari maneno haya kwa kina,Nimeamua yafuatayo kama ushauri kwa watanzania wenzangu.

1.Kuanzia sasa tufufue yale yote yalioliingizia taifa aibu kubwa na hasara isoyosimulika kwa vizazi vijavyo ,Suala laIPTL,SONGAS,Suala la kampuni ya SAMAX,Suala la pesa za EPA,TANGOLD,MEREMETA na vifo,mbavyo vilitokea katika mazingira ya kutatanisha na vilihusu wanaharakati waliotaka wananchi wajue ukweli kuhusu nchi yao au chama flani,tufatilie nani alihusika na ikiwezekana awajibike kwa kwenda jela na watu kufilisiwa ili pesa ya umma irudi.na hata kama ilikuwa ni suala la ushirikina zitumike njia kuwatambua waliwaua waliosema ukweli

2.Suala RDC,Kwa Maoni yangu ninaomba waziri husika afanye haraka kusitisha Mkataba wa Dowans mpaka hapa uchambuzi pembunifu utakapofanyika kuhsusu gharama halisi za uendeshaji wa Umeme hu,na gharama zote ambazo zilizidishwa kwa makusudi zirudishwe serikalini zifanye kazi nyingine

3.Tuanzishe Kampeni za dhati ambazo zitaenda hadi viijijini kuelezea Vugu vugu la demokrasia makini na kupinga ufisadi nchini,inaonekana wananchi wa huko Dutwa na sehemu zingine za umasaini hawajui mambo yanayohusu ufisadi,angalia jana chenge alivyojitapa akisema Dar es salaam ndiyo wananiona sifai,hii inaonesha kwamba wanakijiji hawajui chochote kuhusu ufisadi.

4.Tuache ushabiki wa kufuata Mkumbo bali tuchukue hatua madhubuti zaidi ya kuzomea,mtu akishajulikana ni jangili,afikishwe mahakamini na akpatikana na hatia atiwe nguvuni.

Naomba kutoa hoja.

Gembe

Niandikie: gembe@jamboforums.com
 
Nani anaijua Historia ya kupata Uhuru wa nchi yetu,nadhani tukianzia hapo tutajua nini cha kufanya sababu ili kuleta maendeleo ya nchi yetu.tuangalie ni lini ufisaid wa khali ya juu ulianzia wapi..na ni nani alikuwa wa kwanza kutetea ufisadi,Kuanza kuangalia 2015 huku bado watanzania waishio kijijini ambao ndiyo wenye maisha ya taabu wamekubali kuwashabikia Mafisadi kwa kuwasifu kwa nyimbo na vifijo za kuwapamba huku sie tukiimba mapambio ya kuwakashfu na kuwazomea itakuw ani jambo gumu sana.

Na tuanze na Lowassa,ajibu swali aliloulizwa na mwalimu kwamba pesa alizitoa wapi??hapo tutajua alishiriiana na nani kupata mali hizo na nadhani Lowassa ni moja ya machimbuko ya UFISADI.
 
Gembe nimekusoma mkulu na ndio uzuri wa JF wa kupata mawazo mbali mbali na tofauti ya namna ya kufanya kazi.
 
Gembe
Mawazo yako ni mazuri kabisa na yenye malengo kwa nchi yetu
lakini hayo mawazo yako watuwamekuwa wakiyatoa hapa kila siku, tatizo ni kwamba serikali ndio yenye mamlaka ya kutekeleza hayo mawazo yako, na serikali yenyewe ndio hao mafisadi wenyewe, hakuna lolote litakalofanyika hapa, na ndio maana unaona watu wanapata jazba na kufanya watakavyo, hii ni kwa sababu solution sahii za matatizo haya hazifanyi kazi chini ya serikali hii
Haya yanawezekana kama tukichukua hatua,Huko Ghana yaliwezekana vipi??Je Kenya waliweza vipi??na siye tushindwe hatuna nini??tatizo ni suala la watu kuwekwa madarakani na pesa chafu na zinatolewa na watu wachafu na hao ndio wanaongoza nchi.

1.Kwani ni nani kawachaguia hawa viongozi kama siyo sisi?
2.bila sisi wao wanaweza kuwatawala??

Mwanakijiji kuna kipindi alisema tuwazilie nchi,ila hapana mie nadhani kuna haja sasa ya kuamka kutoka usingizini na kusema NO,tuandamane kuwang'oa mafisadi na jambo jema hizi vuguvugu zianzie vijijini,na ingekuwa vyema vuguvugu za uhuru na ardi ambazo Wangwe alizifufua ziandamane na vuguvugu za kuwaelimisha watanzania waishio vijijini ambao ni kama 76 %.tukiweza hili mie nina uhakika 2015 tutaanza na wabunge makini na mwaka 2020 Tanzania itakuwa mfano wa kuigwa.
 
Hivi nani kisheria mwenye nguvu ya kusitisha mkataba, Waziri mkuu, Raisi, AG au waziri...naomba elimu kidogo hapo
 
Hivi nani kisheria mwenye nguvu ya kusitisha mkataba, Waziri mkuu, Raisi, AG au waziri...naomba elimu kidogo hapo
Kawaida Mkataba huwa unaeleza wazi,Pande zote mbili zinaweza vunja mkataba ila kunakuwa na masharti ya kufuatwa.Kwa kifupi Rais anaweza Vunja Mkataba wowote ambao umeingiwa na kiongozi yeyote Tanzania.
 
Bado watanzania tupo kwenye lepe la usingizi mzito.Sisi tunaofahamu madhila ya kisiasa na kiuchumi yaliyotendeka ndani ya nchi yetu na ambao kusema kweli ni wachache tuna kibarua na changamoto kubwa.Iachukua miaka mingi sana kupata hata idadi ya 30% ya wabunge wa upinzani achana na wazo la kupta Rais kutoka upinzani.Hii ni kwa sababu mwenendo wa uchaguzi kabla ya miezi kama 3 hivi watu wote watakuwa wamesahau mabaya yote ya CCM tangu ilpoundwa.Watasahau ufisadi unaopigiwa kelele na utawaona Watanzania wakiwa na tabasamu,walicheza ngoma na muziki wa CCM hadi atakapotangazwa JK tena kama Rais kwa kipindi kingine tena.Hali hii husababishwa na ujinga na kutojali.Kama kuna mtu ana ndoto kuwa tutapata serikali mpya chini ya Chadema au CUF basi na abaki na ndoto zake kwa sababu Watanzania tunaendelea na kuuchapa usingizi na malezi yetu tangu awali tumekuwa programed hivyo tangu uhuru.Mabadiliko katika hali tuliyonayo sasa ni ndoto.Sijui itokee nini!
 
3.Tuanzishe Kampeni za dhati ambazo zitaenda hadi viijijini kuelezea Vugu vugu la demokrasia makini na kupinga ufisadi nchini,inaonekana wananchi wa huko Dutwa na sehemu zingine za umasaini hawajui mambo yanayohusu ufisadi,angalia jana chenge alivyojitapa akisema Dar es salaam ndiyo wananiona sifai,hii inaonesha kwamba wanakijiji hawajui chochote kuhusu ufisadi.

4.Tuache ushabiki wa kufuata Mkumbo bali tuchukue hatua madhubuti zaidi ya kuzomea,mtu akishajulikana ni jangili,afikishwe mahakamini na akpatikana na hatia atiwe nguvuni.

Gembe
Nimekusoma vema sana na umeeleweka.
Nilishwawahi kusema hapa hizi kampeni za vijijini ni muhimu sana maana wengi bado wako zama za ujima.Bado wanajua Nyerere ndo anatawala mpaka leo.
Jamii nyingi ya wa TZ asili yao ni huko vijijini,na kama wasomi wanaotegemewa na vijiji pamoja na kaya zao wana uwezo wa kubadilisha usemi huu "mafisadi".

Pili sitaki tuache kuwazomea mafisadi kwa kuwa wa kuwapeleka mahakamani ni serikali ya JK ambayo imekaa kimya.Tunachoweza kufanya kwa sasa wananchi kuzomea mpaka mwisho
 
chengesafisha.jpg

wananchi wa kijijini wakimpigia makofi chenge jana.hawa ndio ambao hawajui tulipo na wanatutegemea sana sisi kuwaleza wapi tulipo na tunaelekea wapi​
 
chengesafisha.jpg

wananchi wa kijijini wakimpigia makofi chenge jana.hawa ndio ambao hawajui tulipo na wanatutegemea sana sisi kuwaleza wapi tulipo na tunaelekea wapi​
Wana JF tuanze kampeni everywhere!
Vijijini na Mijini!
Kuwaelimisha wananchi kuhusu ufisadi,madhara yake na namna ya kujikinga nao!
NI LAZIMA TUIPE KIPAUMBELE KAMA VILE TUNAVYOFANYA KWENYE UGAIDI NA UKIMWI!
Majarida yachapishwe..makongamano na mikutano ya kuwaelimisha wananchi!
LA SIVYO WOTE TUTAGEUKA KUWA MAFISADI NA HISTORIA ITATUUMBUA!
 
chengesafisha.jpg

wananchi wa kijijini wakimpigia makofi chenge jana.hawa ndio ambao hawajui tulipo na wanatutegemea sana sisi kuwaleza wapi tulipo na tunaelekea wapi​

Gembe,
Nadhani hapo sasa tunakubaliana kabisa kuwa hakuna hila,ni muujiza pekee utakaotutoa kwenye fix tuliyonayo.Hii si Romania wala Ukraine.Si Senegal wala Botswana.Hii ni Tanzania.Imeoza.Ukombozi wa fikra utapatikana lini? Watanzania walioko vijijini na sorry hata hao walioko mijini wanaamini kuwa CCM ndiyo mwanzo na mwisho wa Tanzania.
 
Mie naamaini inawezekana kama tukichukua hatua,naweza kukawambia hapa mjini sasa watu wameamka,hakuna mtanzania anayeishi hapa dar esa salaam ambaye hajui kuhusu Jamboforums.Mie nina uhakika mabo yatakwenda vizuri kama tukiweka mikakati iliyo bora zaidi na tutafika pale ambapo ninakuona.

Tuwaelimishe watanzania wenzetu walioko Vijijini.
 
Mkuu hili suala ulilolisema ni zito sana nikiangalia Tanzania ilipo katika mwamuko wa kuleta maendeleo, mapinduzi ya fikra tunahitaji kutolala wakati mwingine.

Hivi mnajua tatizo na chimbuko la haya yote?

Watanzania njaa imekuwa kubwa sana, tumepoteza utu kwa sababu ya njaa. Kuna watu wanakuja hata hapa wanamwaga maneno tunashangaa kama kweli ni mtanzania lakini ukifuatilia unakuta ni njaa, anatafuta hili mkono uende kinywani.

Fisadi Chenge, karamagi, Lowassa pamoja na madhambi yao wameisha jua hili wanatumia weakness za watu katika kuwanyonya na kuwagandamiza.

Wale watu wenye uelewa wana kazi kubwa ktk hili. watu wa bariadi unachokiona ni njaa ndio mweshimiwa ametumia. Haiwezekani kwamba hawajui hili.

Kenya wenzetu wameisha pita ktk hatua hii wako hatua moja mbele ktk ukombozi.

Suala litakalo tusaidia haya yanayoonekana ndiyo mapungufu ya katiba yetu. Utasoma katiba yote utaimaliza utaona inatufaa, lakini haina experience tunazozipata sasa.

Tunahitaji kuwa more organized ktk kukabiliana na wezi/mafisadi. Tunahitaji kuwa mbali sana hata zaidi ya vyama vya siasa. Tunahitaji kuangalia sana Tanzania.
 
Gembe, watu wangejue kile ambacho wengine tungeweza kufanya wangetusupport.

a. Si wote wanaweza kufuatilia na kuwapigia simu na kubishana na hawa wakuu hata usiku wa manane; wengine tunaweza.

b. Si wote wana muda wa kufanya mambo hayo na wakati huo huo wakaweza kufanya mambo yao mengine na ya familia; wengine tunaweza

c. Si wote wana vipaji vya ushawishi wa watu lakini wanaweza kuwa wanajua mambo mengi; wengine tunavyo vipaji hivyo na viko at your disposal.

Mwaka jana, nilitumia karibu dola 1500 kufanya mahojiano na kufuatilia mambo mengi ambayo mengine hayakuandikwa mahali popote isipokuwa watu wachache wanayafahamu. Mwaka huu, ukata unaumiza, hali ni ngumu, na hata interviews nilizoziline up nashindwa kufanya.

Kuna interview ya aliyekuwa msaidizi wa Baba wa taifa, kuna interview ya kigogo wa Usalama wa Taifa (msidhani mada hii naivalia njuga kwa bahati mbaya), na zipo nyingine nyingi za matukio ya kila siku, lakini why should I spend my 10 dollar or 20 dollars every week to bring you these interviews?

Kuna mambo ya kijamii ambayo wengine tunaguswa nayo lakini tunashindwa kuyafuatilia. Kuna mengine ambayo watu wengine wanaguswa nayo na wangependa mtu fulani ayafuatilie lakini hilo litawezekana vipi?

Nakuhakikishia masuala ya Tangold na ndugu zao tungeyafumua kuliko watu wanavyojua lakini tunakwama. Nikitumia muda wa saa moja au masaa mawili kufuatilia mambo kwa ajili ya JF au KLHN ina maana muda huo siutumii kwa maisha yangu, so how do I reimburse myself? nothing. Inakuwa ni sadaka.

Sasa hivi, imebidi niongeze kibarua kingine, gharama za maisha zinazidi kama mnavyojua. So, vitu kama hotuba ya Zitto na mahojiano ambayo mengine nimeyafanya na ninayashikilia nashindwa kupata muda wa kuyaedit mwisho, huwa nayatupa tu yanakuwa yamepitwa na wakati.

Kuongeza hayo yote mtu unatarajiwa kuandika makala tatu kila wiki ambazo zimefanyiwa utafiti na zenye kuvutia.. how does one do that?

Tukiomba support watu wengine wanafikiria "janja ya nyani" wanataka kujitajirisha!!

Ndugu zangu, sauti hizi zitanyamaza na zitakoma. Siko ipo nafasi hii itapotezwa na tutabakia katika kabila la "waninge"! Tutabakia kutamana those "days" ...

kama mtu anataka kusupport unawasiliana na watu. Ukitaka kusupport JF wasiliana na Invisible au mimi nitafakisha ujumbe; ukitaka kunisupport mimi na shughuli hizi you know where to get me..

Lakini, majaribu ya kukubali fedha za mafisadi ni makubwa kwani the reasoning goes like "baniani mbaya, kiatu chake ni dawa"...
 
Wana JF tuanze kampeni everywhere!
Vijijini na Mijini!
Kuwaelimisha wananchi kuhusu ufisadi,madhara yake na namna ya kujikinga nao!
NI LAZIMA TUIPE KIPAUMBELE KAMA VILE TUNAVYOFANYA KWENYE UGAIDI NA UKIMWI!
Majarida yachapishwe..makongamano na mikutano ya kuwaelimisha wananchi!
LA SIVYO WOTE TUTAGEUKA KUWA MAFISADI NA HISTORIA ITATUUMBUA!

How do you do that?
 
Chama cha wanawake Madaktari Tanzania (WAMATA) waliamua kulivalia njuga suala la saratani la matiti na wamefanikiwa. Na ieleweke sio serikali iliyowapatia fedha bali wananchiwenye kupenda jamii yenye afya.

Changamoto:

Je,ni lini JF, vyama vya siasa, profeessional association (kama chama cha wanasheria), wanaharakati wengine tutachukua hatua ya kuamua mustakabali wa nchi yetu?????? Kuwashitaki mafisadi, viongozi wasiofuata maadili ya kazi, mikataba mibovu n.k
 
Ndugu wana Jf,

Baada ya jana mie kuhitimisha kuwalemisha watanzania kuhusu Mzee Ben kuachwa kuzomewa na kupanga nini kifanyike chenye manufaa zaidi kwa ajili ya watanzania,nilikaa chini na kuanza kutafakari ni nani kawaloga watanzania,na wakati mwingine naweza kukubaliana na maneno aliyowahi kuyasema Mkapa,kwamba watu wana wivu wa kijinga.na ningependa kuelezea Hoja yangu kwa mapana kwanini nilikuwa namtetea Mzee Ben,ila nilitaka zichukuliwe hatua mashubuti za kufuatwa kuliko kuzomea tu

Nianze na mfano wa kipindi kile watu waliposhinikiza Lowassa ajiuzuru Uwaziri Mkuu,Watananzaia tulikuwa mashabiki na tulipiga kelele ausbuliwe,na kweli akasurubiwa na kuachia ngazi akiwa na wanyang’anyi wenzake,Karamagi na Msabaha.,Jamabo la kujiuliza nini kilifuata baada ya kushabikia Lowassa aachie ngazi
1. Je Dowana hawalipwi pesa zetu yaani dola million 152 kwa siku.

2.Je Lowassa amechuliwa hatua zipi za kisheria kwa kuliingiza taifa katika hasara isiyosemelka,Maana Waziri Mkuu hana kinga ya kupelekwa Mahakamani

3.Je walioshiliki NGT ,kama watanzania tumeshafanya nini ili hawa watu wachukuliwe hatu kali ikiwemo kuwajibika kwa kuachia ngazi,Naomba nikueleze jambo ambalo haulifahamu, watu wote waliohusika na NGT wamebadilishwa vituo na kupelekwa sehemu Nyeti huko Ikulu,Hii maana yake nini??

Pili,Mhe. Chenge naye tulishabikia aachie Ngazi,kweli kwa kuombwa na muungwana aliachia ngazi nafasi yake ya uwaziri,ila tujiulize hii inatosha??Je ndio hicho anastaili au sie tuliunga mkono nia ya kundi flani ambalo lilitaka kumuangusha chenge kisiasa mpaka wakafikia kuzushiana kifo??Tutafakari sana mambo haya sababu tumekuwa watu wa kufuata mkumbu na kuogopa kuchukua hatua.Rejea wakati Mhe. Dk. Mwakyembe akiwasilisha ripoti ya kuhusu RDC alisema watanzania wamekuwa waoga kuellezea wanachokijua kuhusu tuhuma flani ,na hii ni kweli watu wamekuwa wazi kunong’oneza mtu flani jinsi mtu flani anafanya ufisadi wa khali ya juu,ila hawako tayari kuchukua hatua ya kumshtaki mtu huyo

Watanzania wenzagu ,leo mchana nilipoingia JF nilikutana na hoja ya mwanakijiji kuhusu gharama ya kuendesha JF imekuwa kubwa na watu hawako tayari kuchangia ila wako tayari kusoma habari na kutupa muelekeo wa wa ambao wanafanya ufisadi,ila inapokuja suala la kuchangia nini kiganyike watu wamekuwa wagumu,na hii ni moja ya tabia zetu watanzania.inawezakana tua uoga flani,Je tunasubiri nani atoe uoga huu tulio nao?nani achangie Jf kama siyo wewe mtanzania uliye na mkakati wa kuondoa umasikini??

Nimetafakari maneno haya kwa kina,Nimeamua yafuatayo kama ushauri kwa watanzania wenzangu.

1.Kuanzia sasa tufufue yale yote yalioliingizia taifa aibu kubwa na hasara isoyosimulika kwa vizazi vijavyo ,Suala laIPTL,SONGAS,Suala la kampuni ya SAMAX,Suala la pesa za EPA,TANGOLD,MEREMETA na vifo,mbavyo vilitokea katika mazingira ya kutatanisha na vilihusu wanaharakati waliotaka wananchi wajue ukweli kuhusu nchi yao au chama flani,tufatilie nani alihusika na ikiwezekana awajibike kwa kwenda jela na watu kufilisiwa ili pesa ya umma irudi.na hata kama ilikuwa ni suala la ushirikina zitumike njia kuwatambua waliwaua waliosema ukweli

2.Suala RDC,Kwa Maoni yangu ninaomba waziri husika afanye haraka kusitisha Mkataba wa Dowans mpaka hapa uchambuzi pembunifu utakapofanyika kuhsusu gharama halisi za uendeshaji wa Umeme hu,na gharama zote ambazo zilizidishwa kwa makusudi zirudishwe serikalini zifanye kazi nyingine

3.Tuanzishe Kampeni za dhati ambazo zitaenda hadi viijijini kuelezea Vugu vugu la demokrasia makini na kupinga ufisadi nchini,inaonekana wananchi wa huko Dutwa na sehemu zingine za umasaini hawajui mambo yanayohusu ufisadi,angalia jana chenge alivyojitapa akisema Dar es salaam ndiyo wananiona sifai,hii inaonesha kwamba wanakijiji hawajui chochote kuhusu ufisadi.

4.Tuache ushabiki wa kufuata Mkumbo bali tuchukue hatua madhubuti zaidi ya kuzomea,mtu akishajulikana ni jangili,afikishwe mahakamini na akpatikana na hatia atiwe nguvuni.

Naomba kutoa hoja.

Gembe

Niandikie: gembe@jamboforums.com

28bvb5t.gif
 
Mwanakijiji Nimekupata,

Mafisadi wanapenda sauti hizi zikae kimya ili waweze kutanua,Hata kuna wakti spika alishawahi kukiri kwamba JF ni chombo amabacho kinaleta changamoto katika maendeleo ya nchi yetu.

Mie nadhani kuna haja ya sasa wananchi kukaa na kufikiria nini cha kufaya ili JF iendelee Kusimama,na namsahuri Invisible aweke account namba ya JF ili watuwa weze kuchangia,nina imani watu wengi watachangai ili JF na KLH News ziweze kuwapo.

Tafadhali sana Invisible weak aaccount hapa,kuna watu kibao wanataka kuchangia na nimewasikia wakitaka kujua account namba ya JF,cha kufanya weak iwe sticky thread na watu waweze kuiona.Baada ya wiki mbili tutafanya analysis.ni kiasi gani kimepatikana

Tunahitaji kujua nini kinaendela TISS,wana mpango gani na Mafisadi,hii itasaidia nini cha kufanya.Tupo tayari kufuatilia mambo mengi msiyajua sababu tuko hapa kwa ajili yenu,tuna mdigo mipana ya kuzungumza yale wengine wanayoyaogopa.
 
4.Tuache ushabiki wa kufuata Mkumbo bali tuchukue hatua madhubuti zaidi ya kuzomea,mtu akishajulikana ni jangili,afikishwe mahakamini na akpatikana na hatia atiwe nguvuni.
Gembe,
Ulichoongea ni point zote na nimezielewa vizuri ila hapa mzee kidogo nijikwae. Harafu ni sehemu ambayo haikustahili herufi kubwa lakini...anyway nahisi hukumaanisha Kitila.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom