Nani katika Serikali hii awamu ya tano mwenye huu uwezo wa kuongea na Wanahabari?

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,228
113,575
Miaka mitano inakaribia kukatika sasa tokea serikali hii ya Rais Magufuli iingie madarakani.

Lakini tokea iingie madarakani, sijaona, kuanzia Rais mwenyewe hadi hao wateule wake, wakifanya mikutano na waandishi wa habari, hususan waandishi wa habari wa vyombo vya kimataifa.

Kuna wakati fulani hivi Rais Magufuli alikuwa na Rais Museveni, wakaulizwa maswali mawili matatu hivi. Hiyo nayo inahesabika kama mkutano na waandishi wa habari?

Sasa nimewaza hapa nilipo. Hivi ni nani kwenye serikali hii ya Magufuli mwenye uwezo wa kufanya mkutano na waandishi wa habari wa kimataifa, iwe kwa lugha ya Kiingereza au Kiswahili?

Nimeangaza wee, lakini sijaona. Kuanzia Rais mwenyewe hadi kwa Gavana wa Dar es Salaam, naona wote hawana umahiri wa kufanya hivyo.

Nani kwenye hii serikali mnadhani anao uwezo huo?

Kwenye hii video hapa chini, Rais Julius Nyerere alikuwa New Delhi na akafanya mkutano na waandishi wa habari kwa kujiamini kabisa.






Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ngabu,

Hakuna anayeweza kufanya mahojiano hata kujieleza wanaongea chini ya sekunde 60 kama clip hii iliyojaa cream ya viongozi wateule mawaziri, wakuu wa taasisi n.k

March 1, 2020

Tanzania's Vision year 2025 Massive investment in Infrastructure, Industrialization, Energy, SGR Railway network, Reforming Mining Sector and Geopolitics in East, Central and Southern Africa

Tanzania is an unforgettable destination. The land of the Kilimanjaro, the Serengeti and the beautiful beaches of Zanzibar, Tanzania offers adventure, excitement and splendor in all forms. With a young and growing population, Tanzania's new business blueprint is in line with the country's consolidated efforts to market itself as an investment hub within the African continent.



Special thanks to:
Dr. Hassan Abbasi, Freddy Manongi, Dr.Hamisi Andrea Kigwangalla , Prof. Florens Luoga, Dotto Biteko, Jaffari Matundu, Cosmas Kimario, Allan Kijazi, Sanjay Rughani, Jared H. Zebre, Saifuddin Khanbhai, Mahmud Thabit Kombo, Ney wa Mitego, Joseph Iha Wanje, Masanja Kadogosa, Dr. Edwin Mhede, Abdulmajid Musa Nsekela, Mohamed Hassan, Eric Zurrin, Simon Karikari, Hisham Hendi, David Kibebe, Theobald Sabi and James Kilaba
 
Hapa Benjamin Mkapa na Kofi Annan wakizungumza na waandishi wa habari.

Mkapa na Annan ni Waafrika weusi kama tu walivyo Magufuli na Makonda.

 
Back
Top Bottom