Nani kati ya Marais wa Tanzania angeibuka kidedea/mshindi kwa vigezo hivi?

bernard10

JF-Expert Member
Apr 2, 2021
410
731
Tanzania ni moja Kati ya nchi chache barani Afrika ambazo zimeshafanikiwa kuwa na awamu tofauti tofauti za uongozi wa ngazi ya juu kabisa(URAISI) na ni miongoni mwa nchi chache kabisa ambazo hazijawahi kuwa na matukio makubwa yaumwagaji damu, vita vya wenyewe kwa wenyew na mapinduzi ya kijeshi yaani (COUPS)kama zilivyo nchi nyingi barani Afrika.

Sasa katika awamu zote tukimtoa Nyerere kiongozi wetu wa awamu ya Kwanza (mwanamapinduzi na baba wa taifa) na Mwinyi Ally Hassan ambaye wengi wetu kizazi hiki hatukumshuhudia Sana (either tulikuwa wadogo au hatukuwa tumezaliwa bado).

Je, ni nani Kati ya hawa wote wanne 4 waliobakia ikatokea (ingawa haiwezekani) yaani.1. Mkapa Benjamini 2. Kikwete J.k 3. Magufuli J.P.M au 4.Samia S.S.

ANGEIBUKA KIDEDEA/MSHINDI KAMA WANGESHINDANA KATIKA UCHAGUZI(FREE AND FAIRLY) kwakuzingatia.
1. Vitu walivyofanyia jamii zetu (Watanzania)kwa ujumla (legacy)
2. Ushawishi wao katika nyanja zote kisiasa kiuchumi kijamii n.k
3. Uwajibikaji wao kwa vitendo n.b (siyo porojo.)
4. Kukubalika kwao. (Hapa ni jinsi wanachi kwa ujumla walivyowachukulia, kuwapenda na kuwakubali.
5. Utu wao(utani au ucheshi, huruma, kujitolea n.k.
6. Misimamo Yao (nb. kiongozi ni misimamo.
7. Ubunifu wao kwaujumla (kwa mfano katika kuiletea nchi maendeleo, kusuruhisha matatizo ya wananchi au viongozi ushawishi n.k
8. Uvumilivu (kiongozi lazima awe na uvumilivu katika mambo yote.
9. Ushirikiano chanya yaani wenye afya katika maslai ya nchi na A. viongozi wengine ndani na nje, B. wanachi.

KWA VIGEZO HIVYO NA VINGINE KAMA VIPO JE NI NANI ANGEIBUKA KIDEDEA/MSHINDI WETU KATIKA UCHAGUZI MKUU(e.g 2025)?
 
Hata kama wangegombea Real wangeibiana Kura tu hawa.

Ila in Real situation watu wangeenda na JK
 
Pia ingetokea kushindanishwa katika uchaguzi mkuu kati ya Lisu na Lowasa nani angeibuka kidedea. Hebu angalia aina ya mikutano yao katika chaguzi kuu za 2015 picha mbili hapo juu.. na 2020 picha mbili hapo chini?

images (19).jpeg


images (14).jpeg

Mafuriko ya m'beleji T.Lisu hapo juu 👆 Mafuriko ya m'bongo E.Lowasa hapo chini 👇
images (13).jpeg


images (11).jpeg
 
Kura zingeenda kwa walioanza kuhudumu awamu yenye tarakimu witiri (wengi sio na kipato na wenye mlengo wa jamii jumuishi) wenye awamu shufwa kura zao ni kutoka (kila mmoja afanye chochote bila kubughudhiwa yaani demokrasia na matajiri)

Maana yake BWM na JPM ni kapu moja wakati JKM na SSH nao kapu ni moja kimantiki na uhalisia
 
Back
Top Bottom