Nani kati ya hawa wanasiasa Chadema anafaa kuwa Raisi wa Tanzania?

Kwangu mimi kama sio mbowe second choice Zito anafaa sana hawa wengine nawapotezea tu.
 
Full magarasa! Labda awe Rais wa kwaya fulani naweza kuwafikiria!
 
Kadri siku sinazokwenda inajidhihilisha kuwa ni Vyama Vitatu tu ambavyo vina uewezekano usiopingika wa kutoa Raisi wa awamu ya tano Tanzania (CCM, CHADEMA NA CUF).
Nisingependa kuongelea Wagombea Uraisi binafsi mpaka hapo katiba mpya itakapo litambua hilo.
Kwa kuanzia na hii toli (thread), ningependa mchangiaji utoe mawazo yako ya nani anafaa kati ya hawa Wanasiasa wa CHADEMA na sababu zipi zinakufanya ufikilie kama ana uwezo kisiasa wa kuwashinda wagombea wa vyama vingine ya siasa.
Pia kama unafikilia katika orodha hii kuna Mwanasiasa sikumtaja, tafadhali bandika jina lake na utoe sababu lakini kumbuka katiba ya Tanzania, Ibara ya 39, Ibara ndogo ya (1), kifungu kidogo (a-e ). Mwanasiasa lazima awe na umri si chini ya miaka 40 na haisemi lolote juu ya kiwango gani cha elimu, kwa maana hii, elimu siyo kigezo kinachomzuia Mtanzania kugombea nafasi ya Uraisi.


Nitatoa majina pia ya Wanasiasa wa vyama vya CCM na CUF katika toli(thread) nyingine ili wana janvi tuchangie.


Ikumbukwe dhumuni langu kuu siyo kupiga kura za maoni au kutoa kashfa zisizo zibitishwa bali ni kuchangia mawazo kuona ni jinsi gani sisi kama wananchi wa kawaida tungependelea awe kiongozi wetu wa Taifa.
Nitakuwa ninakusanya maoni kila baada ya saa sita usiku na kuona ni Mwanasiasa yupi wanamtandao mnafikilia zaidi kama awe ni kiongozi wa Taifa.


Janvi ni lako, litawaliwe na nguvu za hoja na sio hoja za nguvu.


Changia...


Freeman Aikaeli Mbowe-Mwenyekiti
Dk. Willibrod Peter Slaa-Katibu
Tundu Lissu-Mbunge(Singida Mashariki)
Philemon Kiwelu Ndesamburo-Mbunge(Moshi Mjini)
Prof. Kulikoyela Kanalwanda Kahigi-Mbunge(Bukombe)
Simon Peter Msigwa-Mbunge(Iringa Mjini)
Mabere Marando-Mjumbe wa Kamati kuu
John Magale Shibuda-Mbunge(Maswa Mashariki)
Joseph Roman Selasini-Mbuge(Rombo)
Mustapha Boay Akunaay-Mbunge(Mbulu)
Said Amour Arfi-Mbunge(Mpanda Mjini)
Prof. Mwesiga Baregu-mshauri wa kisiasa
naona mmejazana huko vya kutosha kabisa.
 
Back
Top Bottom