Elections 2010 Nani kasema tutibu madonda ya uchaguzi ya CCM, NEC na timu ya JK?

Kalunguine

JF-Expert Member
Jul 27, 2010
2,543
134
Timu ya kampeni ya JK, CCM na NEC wote kwa pamoja wametumia njia ya vitisho ya vita, kufanya kampeni za kuwagawa wananchi kwa udini, kumchafua Dr. Slaa na Chadema kwa kila hali kupitia magazeti, TV na sms leo wanasema tutibu madonda ya uchaguzi, nani mtanzania atakaye kubali huu utaahira? Nchi imepasuliwa vipande vipande na CCM na timu ya kampeni ya JK ili wapate madaraka. Hapana, mapambano ndiyo kwanza yameanza. Moto uliowashwa wa kurudisha nchi mikononi mwa raia wa Tanzania unaendelea kuwaka. Chadema tunawataka watekeleze njia zote walizopanga kupinga udhalimu wa CCM. Wawatangazie mataifa wajue udikiteta wa CCM wa kulazimisha watanzania kuongozwa na JK huku hawataki kuwajibishwa kwa kura. Pia tunawataka Chadema warudi kwetu wananchi watueleze namna tulivyoporwa kura zetu tulizompigia Dr. Slaa na Chadema. Tunawataka Chadema pia wafungue kesi ya kikatiba kupinga wizi wa NEC na matumizi mabaya ya usalama wa CCM-UWT. CCM na JK wanawatia watanzania vidonda kwa makusudi. Tuliwaambia mara nyingi sana waache tamaa ya uongizi, nchi ni ya wananchi siyo ya CCM wala JK. Wakaona bora wawatie vidonda wananchi, na kuipasuapasua Tanzania vipandevipande leo wanasema tutibu vidonda, nani? Mapambano ya demokrasia ndiyo kwanza yameanza na hakuna kulala. Aliyechaguliwa kwa uhalali na wananchi ni Dr. Slaa.
 
NEC imetawaliwa na Serikali ya CCM . Haikuwa huru, inafata maelekezo ya CCM. Tunadai uhuru wa NEC, usiofungamana na upande wowote.
 
Nec na hizo mahakama sidhani kama zitakuwa namsaada wowote, muhimu ni kubadili katiba tu, na hii kwa idadi ya wabunge wa yeboyebo sidhani kama watakubali. Tuendelee kuwahimiza wabongo ili wawachague wabunge wengi wa upinzani ili tuweze kuleta msukumo na kupata katbaba mpya, 2015 yaweza kuwa mbali but muhimu ni kuanza mapema!
 
Kila njia halali ya kupambana na wizi huu lazima itumike ikiwa ni pamoja na kwenda mahakamani kuweka ushahidi hadharani. Hatuwezi kuendelea kuwa chama cha ushindani ni lazima lengo liwe kutwaa madaraka. Hivyo kupambana na udhalimu na wizi wa CCM ni muhimu sana wakati huu kuliko wakati mwingine wowote.
 
Well said, hawa jamaa CCM walimpaka matope Dk Slaa pamoja na chama kizima cha CHADEMA kwa kuingiza ukabila na udini bila kujua kuwa CHADEMA kimekubalika kila kona ya nchi isingekuwa uchakachuaji kingepata zaidi ya viti vya ubunge 100 na Dk Slaa angelikuwa rais au angeshindwa kwa kura kama laki moja si hizo milioni mbili na ushee walizosema
 
ccm walikosea sana kukipaka matope chadema kwenye suala la ukabila na udini! madonda haya kufutika ni tabu sana! Labda wanaweza kuyafuta kwa kupambana kwa moyo safi na ufisadi kwani adui yetu mkubwa ni UFISADI KAZI KWAKO PRESIDENT!
 
Back
Top Bottom