Kalunguine
JF-Expert Member
- Jul 27, 2010
- 2,543
- 134
Timu ya kampeni ya JK, CCM na NEC wote kwa pamoja wametumia njia ya vitisho ya vita, kufanya kampeni za kuwagawa wananchi kwa udini, kumchafua Dr. Slaa na Chadema kwa kila hali kupitia magazeti, TV na sms leo wanasema tutibu madonda ya uchaguzi, nani mtanzania atakaye kubali huu utaahira? Nchi imepasuliwa vipande vipande na CCM na timu ya kampeni ya JK ili wapate madaraka. Hapana, mapambano ndiyo kwanza yameanza. Moto uliowashwa wa kurudisha nchi mikononi mwa raia wa Tanzania unaendelea kuwaka. Chadema tunawataka watekeleze njia zote walizopanga kupinga udhalimu wa CCM. Wawatangazie mataifa wajue udikiteta wa CCM wa kulazimisha watanzania kuongozwa na JK huku hawataki kuwajibishwa kwa kura. Pia tunawataka Chadema warudi kwetu wananchi watueleze namna tulivyoporwa kura zetu tulizompigia Dr. Slaa na Chadema. Tunawataka Chadema pia wafungue kesi ya kikatiba kupinga wizi wa NEC na matumizi mabaya ya usalama wa CCM-UWT. CCM na JK wanawatia watanzania vidonda kwa makusudi. Tuliwaambia mara nyingi sana waache tamaa ya uongizi, nchi ni ya wananchi siyo ya CCM wala JK. Wakaona bora wawatie vidonda wananchi, na kuipasuapasua Tanzania vipandevipande leo wanasema tutibu vidonda, nani? Mapambano ya demokrasia ndiyo kwanza yameanza na hakuna kulala. Aliyechaguliwa kwa uhalali na wananchi ni Dr. Slaa.