sulphadoxine
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 2,257
- 644
Zaidi ya miaka 100 iliyopita, mwanaharakati wa siasa za mapambano, Karl Marx, alidai kwamba, dini ni bangi inayolevya na kupumbaza watu, wasiweze kujua adui wao wala kupigania haki zao.
Kwa mtazamo huo, Marx aliona dini kama taasisi inayopinga mapinduzi ya wanyonge, wenye kuonewa na kunyanyaswa, akatangaza vita dhidi yake.
Ni kwa sababu hii, mpaka leo dini [kanisa] havikai meza moja na itikadi za ki-Karl Marx, kwa maana ya Ukomunisti na dhana zingine za kimapinduzi za mwanadamu duniani.
Kabla ya hapo, zaidi ya miaka 2000 iliyopita, mwasisi wa Ukristo, Yesu Kristo [Nabii Issa], wakati akijibu mashtaka dhidi yake kwenye kesi ya uhaini, kwa tuhuma za kutaka kupindua Serikali ya Kaisari, alipewa mtego, aeleze ni kwa mamlaka yapi alielekeza utii wake; naye akajibu,Cha Kaisari apewe Kaisari, na cha Mungu apewe Mungu.
Hapo ndipo ikazaliwa dhana ya kutochanganya dini na siasa, tafsiri ambayo imewasilishwa kwa kupotoshwa katika jamii mara nyingi.
Katika makala haya nitatumia neno kanisa kumaanisha jumuiya za waumini wa dini mbali mbali katika jamii pana inayotawaliwa, bila ubaguzi wa ki-madhehebu.
Kwa kifupi, kanisa ni waumini wa dini chini ya madhehebu mbali mbali, na si majengo ya kuabudia kwa madhehebu fulani fulani tu.
Kwa Karl Marx, dini na kanisa vilikuwa ni vyombo vya watawala na wenye elimu, vilivyotumika kuwakandamiza na kuwaogofya
[juu ya moto wa milele], kuwadhibiti na kuwapumbaza wanyonge kwa ahadi ya ufalme wa mbingu, kwa kujikana wenyewe ili wasielewe chanzo cha matatizo yao yenye kusababishwa na binadamu wenzao.
Kilicho wazi hapa ni kwamba, upofu wa Karl Marx haukuwa juu ya dini, bali ugomvi wake ulikuwa juu ya watawala na mwenendo wa Kanisa kwa kutekwa na ubinafsi wa watawala, wakachanganya dini na utawala kuzaa kinachoweza kuitwa taifa na utawala wa Kiotheokrasia, kwa maana ya Taifa kuongozwa kwa misingi ya kidini, au Serikali ya makasisi.
Wapo waliomtangulia Karl Marx ambao waligundua udhaifu huo wa Kanisa pekee la Roma la wakati huo [lililotekwa nyara na watawala tangu enzi za Mfalme Constantine wa I], lakini hawakushambulia dini, badala yake walishinikiza kufanyika marekebisho katika mfumo na mwenendo wa Kanisa bila kuathiri imani na nafasi ya dini katika jamii.
Hawa ni pamoja na Mchungaji Martin Luther [1483 1534] aliyeanzisha Tawi la Kilutheri la Kanisa la Roma; Mfalme Henry wa VIII wa Uingereza aliyejiengua na kutangaza Kanisa lake la Anglikana; na John Calvin [1509 1547] aliyebuni mapokeo ya Ki-Kalvin, kwa kutaja matukio machache tu.
Wakati wa enzi za Karl Marx, kulikuwa na dini kuu mbili za Kimataifa yaani, Ukristo na Uislamu. Misahafu ya dini hizi ni Biblia [Ukristo] na Kurani kwa Uislamu. Kinyume na fikra za Karl Marx, misahafu yote miwili inatetea wanyonge na kupiga vita uonevu, ukandamizaji na unyonyaji, na kutoa wito kwa wanaoonewa kuasi dhidi ya vyanzo vya uovu na maovu. Kama Marx angeisoma vyema misahafu hiyo miwili bila kuyumbishwa na matendo ya watawala walioliteka Kanisa, wakaitumia dini kwa manufaa yao, bila shaka asingejenga uhasama na ukinzani kati ya falsafa yake na dini, badala yake angekuwa mtetezi mkubwa wa dini na Kanisa.
Tuchukue mfano wa uanaharakati na uanamapinduzi wa Kristo: Kuna wakati Kristo alizua ukinzani na watawala kwa kuwataka wajisafishe kwa maovu, uonevu na dhuluma kwa wanyonge, kitendo kilichosababisha akamatwe na kusulubiwa kwa tuhuma za kuchochea maasi dhidi ya utawala wa nchi. Kati ya wanafunzi wake 12, wawili kati yao, Simon na Yuda, kabla ya kumfuata, walikuwa wanaharakati, wakereketwa [zealots] wa haki na wapiganaji dhidi ya utawala wa kikoloni wa Kirumi nchini Uyahudi.
Uanamapinduzi wa Kristo unathibitishwa pia na maneno kama, Nimekuja kutupa moto duniani; au, Sikuleta amani, bali upanga [Luka 12: 49 53] kwa maana ya mapambano ya ana kwa ana dhidi ya udhalimu katika jamii.
Na kwa sababu jamii ya wakati huo ilikuwa imejaa maovu, kama ambavyo Taifa letu linaelekea kugubikwa na rushwa kubwa na ufisadi, palitakiwa wachache kujitoa mhanga kwa manufaa ya walio wengi kama yeye alivyojitoa. Na ili kufanya hivyo alisema, Mtu ajikane mwenyewe na anifuate. Hata siku ya kusulubiwa kwake msalabani, hakujutia vita aliyoianzisha; akawaagiza wafuasi wake wauze kanzu [nguo] zao, ili wanunue mapanga kuendeleza harakati za kuwakomboa wanyonge.
Kuhusu utajiri wa kinyonyaji, aliwaonya watawala wenye uchu wa kutajirika, kwamba hawawezi kutumikia mabwana wawili, Mungu [watu] na mali [utajiri] bila kuteteresha ukweli na haki; akasema, ni rahisi ngamia [kamba nene, sio mnyama] kupita kwenye tundu ya sindano, kuliko tajiri [uchu wa mali] kuuona ufalme wa mbingu, kwa njia ya kutenda haki na kweli.
Aliwanyuka mijeledi wezi na wafanyabiashara, walioweka mbele maslahi yao binafsi kuliko utu, alipowakuta wakiuza bidhaa kwa ulanguzi hekaluni. Ikulu, kama lilivyo hekalu na msikiti ni mahali patakatifu; kwa sababu ndipo maamuzi makuu hutokea. Ni dhambi kubwa kwa wanasiasa, kama ilivyo kwa waumini kupageuza mahali patakatifu kuwa pango la walanguzi, kama alivyobaini Mwalimu Nyerere mwaka 1990, alipoona wafanyabiashara matapeli kuizoea Ikulu, Rais na familia yake.
Usawa wa binadamu katika jamii umesisitizwa vizuri pia katika Kurani tukufu kwa kuhusishwa na zaka [zakat] na sala kuwawezesha masikini kuendesha maisha mazuri kama binadamu wengine [LXX: 24 25].
Kurani tukufu inasisitiza pia juu ya utu na wajibu wa kila mtu kwa jamii [jamaa], mshikamano katika usawa, na ushirikiano kwa jamii nzima [XVII: 70].
Uislamu, kama ulivyo Ukristo, unasisitiza HAKI, wema, usawa na ukweli kwa watu wote, hata kama hayo hayatamfurahisha muumini mwenyewe, wazazi au ndugu zake [IV: 135].
Karl Marx hakuweza kuzitekeleza kwa vitendo nadharia zake, kwani alifia uhamishoni Uingereza kama mkimbizi na kuacha mabunda lukuki ya vitabu vya fikra zake.
Katika zama zetu hizi, je, dini ina nafasi yoyote katika maendeleo ya jamii au bado ni yale yale ya mtazamo wa Karl Marx? Nini chanzo na sababu za watawala kutaka viongozi wa dini wasichanganye siasa na dini? Ni kipi hicho kinachoitwa kuchanganya siasa na dini?
Ukichunguza kwa makini, utaona kuwa mambo yanayopigiwa kelele na viongozi wa dini, na ambayo watawala wanadai ni kuchanganya siasa na dini, ni pamoja na mambo kama: Tofauti