Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Mapema leo niliweka andiko hapa kuhusu overview ya bajeti ya wizara ya viwanda, Biashara na Uwekezaji ya Tanzania na wenzetu wa Kenya. Kwenye Bajeti ya mwaka huu Tanzania imetenga Bilioni 81.8 kwa ajili ya matumizi yote ya vieanda (ya kawaida na ya maendeleo) ya Wizara hiyo.
Wenzetu Kenya kwny makisio ya Bajeti yao (Propasal for the Kenyan Budget), wanakisia kutumia KZS Bilioni 42 sawa na karibu Trilioni 1 za Kitanzania kwenye sekta ya viwanda. Hii ni mara 12 zaidi ya bajeti yetu yote ya wizara yetu ya viwanda, au mara 26 ya bajeti ya maendeleo kwny wizara hiyo.
Baadhi ya watu akiwemo Ndugu Samwel Shamy wametetea kiasi kidogo cha Bajeti ya Viwanda kilichotengwa na serikali kwa madai kuwa SERIKALI HAIJENGI VIWANDA. Eti viwanda hujengwa na sekta binafsi na hivyo serikali ya JPM itajiimarisha kuwezesha sekta binafsi kujenga viwanda. Ktk maelezo yake Ndugu Shamy anasema policies za SAP kupitia WB na IMF zinalazimisha uchumi kumilikiwa na sekta binafsi.
Shammy akanitaka nisijadili masuala ya Uchumi kwa kuwa si "taaluma yangu" lakini wakati huohuo yeye akawa anajadili Uchumi ambao sio taaluma yake pia (kichekesho).!
Lakini Je, hivi jambo lisipokua la taaluma yako ni marufuku kujadili?? Kama Shamy alimaanisha wanasheria wajadili sheria tu, walimu wajadili elimu tu, na taaluma nyingine hivyohivyo basi hakuwaza sawasawa.
Kwangu mimi sidhani kama kujadili jambo lisilo taaluma yako ni kosa, ili mradi tu usipotoshe. Katika kujadili ndio tunapata kujifunza zaidi. Kama jambo hatujui tunatoa fursa kwa wanaojua zaidi watuelimishe. Na hii ndio maana ya elimu. Sasa kama Shamy anataka tujadili mambo ya taaluma zetu tu, je vp kwa wasio na taaluma? Wao watajadili nini?
Shamy anasema mimi "Layman" ktk uchumi akitaka tuwaachie "Experties" wa Uchumi wajadili. Ni kweli mimi ni "layman" wa Uchumi kama yeye, lakini haimaanishi kwamba sijui chochote kwny uchumi. Nina "ABC" kdg za Uchumi ambazo huniongoza. Nimesoma both Micro & Macro Economics, na Business Statistics kwny Undergraduate kama subsidiary courses. Pia nasoma Health Economics kwny masomo yangu ya sasa. Kwahiyo atleast nina "basic knowledge" ya Uchumi, sipo "blank" kama anavyodhani.
Anyway letz back to the topic. Je ni kweli serikali haijengi viwanda kama alivyosema Shamy?. Je ni kweli kwamba sekta binafsi ndiyo inayopaswa kujenga viwanda kutokana na uchumi wa dunia kubebwa policies za SAP.? Jibu la haraka ni kwamba SI KWELI.
#FACT_number1
Katika Uchumi wa soko huria (Free market Economy) njia KUU za uzalishaji huachwa chini ya sekta binafsi lakini si njia ZOTE. (Kuna tofauti kati ya Njia zote na Njia Juu). Na haya ni maazimio ya WB na IMF kupitia mpango wa kukuza uchumi ujulikanao kama Structural Adjustment Programs (SAPs).
Maana yake ni kwamba serikali ina fursa ya kumiliki njia za uzalishaji japo kwa kiasi kidogo. Njia kuu zinakuwa kwny mikono ya sekta binafsi. Kwahiyo kusema serikali ya Tanzania haiwezi kujenga wala kumiliki kiwanda kwa sababu wenye jukumu hilo ni sekta binafsi hiyo ni hoja mufilisi.
#Fact_number2
Kwenye mfumo wa uchumi wa soko huria, upo uwezekano wa serikali kumiliki viwanda vichache ambavyo ni "essential" ktk sekta anuai japo fursa kubwa zaidi hutolewa kwa sekta binafsi.
Kwa mfano viwanda vya silaha humilikiwa na dola (serikali). Huwezi kuruhusu sekta binafsi kumiliki viwanda vya silaha kisa tu policies za SAP zinataka viwanda kumilikiwa na sekta binafsi. Marekani ndiye baba wa Ubepari duniani lakini hakuna kiwanda binafsi cha kutengeneza silaha nchini humo ambacho hakina ubia na serikali.
#Fact_number3
Baadhi ya viwanda kutokana na umuhimu wake vinapaswa kumilikiwa na serikali au viendeshwe kwa ubiya kati ya serikali na na sekta binafsi. Na ikitokea hivyo inabidi serikali iwe na hisa nyingi zaidi. Hii hufanyika ili kuzuia hujuma (sabotage).
Kuna viwanda vikimilikiwa na sekta binafsi vinafanyiwa sabotage ili kufavour wafanyabiashara wanaoagiza bidhaa za aina hiyo kutoka nje (za bei rahisi) ili ku-earn super normal profit.
Nchini Venezuela viwanda vya sukari vilikuwa vinamilikiwa na serikali. Kwa hiyo wafanyabiashara waliokua wakiingiza sikari kutoka nje wakawa wanapata ushindani mkubwa wa sukari iliyokua ikizalishwa palepale nchini. Kwahiyo wakashawishi viwanda kubinafsishwa.
Wakavinunua kisha wakavifanyia sabotage, vikaanza kuzalisha chini ya kiwango, na vingine vikafa. Kwahiyo demand ya sukari ikaongezeka na supply ikapungua (soma Venezuela Sugar crisis). Matokeo yake wale mabepari (waliosabotage viwanda) wakaruhusiwa kuingiza sukari kutoka nje kwa wingi ili kucover deficit. Na hapo lengo lao likawa limetimia. Wakapata faida kubwa sana (super normal profit) kwa biashara ya sukari kutoka nje.
Baadae serikali ikawashtukia na kutaifisha viwanda vyote vikarudi chini ya umiliki wa serikali. Na vikaanza uzalishaji unaotosheleza mahitaji.
#Fact_Nunber4
Serikali inaweza kumiliki baadhi ya viwanda ktk nchi (si vyote bali vile vichache vya muhimu) ili kusaidia kufanya Protectionism (policy). Kwa mfano kama cement kutoka nje inauzwa Sh.10,000/= na ya ndani inauzwa 12,000/= maana yake ni kwamba watu watakimbilia kununua cement ya nje na hivyo cement ya ndani itakosa soko na hatimaye viwanda kufa.
Sasa serikali inaweza kufanya protectionism kwa kuingia ubiya (partnership) na viwanda vya ndani. Kwahiyo ikawa inatoa ruzuku, na rasilimali nyingine ili kusaidia kiwanda kupunguza gharama ya uzalishaji (cost of production). Hii itasaidia kupunguza bei ya cement pia. Badala ya kuuzwa 12,000/= kwa mfuko inaweza kuuzwa 8,000/= na hivyo kuweza kushindana na cement ya nje.
#Fact_Number5
Serikali inaweza kumiliki baadhi ya viwanda kama policy kumlinda mlaji (Protection of final consumer) hasa kwenye bidhaa znazotumiwa na watu wa kipato cha chini (inferior goods) au bidhaa ambazo ni muhimu kutumiwa ktk matumizi ya kila siku (essential goods).
Kwa mfano sukari ni "essential good" lakini viwanda vilivyopo nchini havitoshelezi mahitaji. Kwa hiyo serikali iliruhusu wafanyabiashara wakubwa waagize sukari kutoka nje ili kucover deficit. Matokeo yake wapo baadhi ya wafanyabiashara (si wote) walikua wakinunua sukari iliyo-expire na kuja kuifunga upya na kuiuza nchini. Matokeo yake watu wanapatwa magonjwa ya ajabu ikiwemo kansa kwa kutumia sukari hiyo iliyopita muda wake.
Lakini hawa wafanyabiashara wasingeweza kwenda kununua sukari nje kama ya ndani tungekuwa na sukari ya kujitosheleza. Kwahiyo serikali inaweza kujenga kiwanda kitakachozalisha sukari ya kucover deficit ya viwanda vilivyopo na hivyo kuzalisha sukari ya kujitosheleza. Maana yake ni kwamba hakutakua na haja ya kuagiz sukari kutoka nje, na hivyo kumlinda mlaji wa mwisho dhidi ya bidhaa isiyokidhi viwango (final consumer).
NB:
Kwahiyo SI KWELI kwamba serikali hairuhisiwi kujenga viwanda eti kisa kuna masharti ya WB na IMF kupitia policy za SAP. Yapo mazingira yanayoruhusu serikali kujenga viwanda kama nilivyoeleza hapo juu. SAP haitoi total restriction ya serikali kumiliki au kujenga kiwanda. Inategemea na situation. Soma paper iitwayo "Structural Adjustment Programes; the Environment and Sustainable Development" iliyoandikwa na David Reed, mwaka 1996.
Leo Tanzania tunalia uhaba wa sukari. Zipo sababu nyingi zilizochangia ukosefu wa sukari nchini lakini sababu mojawapo ni kwamba wafanyabiashara wakubwa wa sukari wanashiriki kusurbotage viwanda vya ndani.
Kwahiyo si sahihi kusema eti serikali haipaswi kumiliki wala kujenga kiwanda chochote kwa hoja dhaifu wa Free Market Economy. Uchumi wa soko huria hauzuii serikali yoyote duniani kujenga kiwanda. Kuna mazingira serikali inaweza kujenga viwanda kama nilivyoeleza hapo juu. Kwa hiyo kusema viwanda vitajengwa na sekta binafsi tu ni uzwazwa.
Hujiulizi imekuaje Kenya ikatenga bajeti kubwa ya viwanda kama kweli ujenzi wa viwanda unafanywa na sekta binafsi.? Au mnadhani Trilioni 1 waliyotenga Kenya ni kwa ajili ya posho na marupurupu ya viongozi wa wizara.? Wenzetu wanawaza mbali, hawawezi kuiachia sekta binafsi kila kitu. Kuna mambo mengine serikali inabidi ijiingize. Sisi tumebweteka tu kama mazuzu eti viwanda vitajengwa na sekta binafsi, wenzetu wanatumia sekta binafsi na serikali kwa pamoja kujenga viwanda.
Ukweli ni kwamba serikali yetu bado ina hofu ya kuwekeza kwenye sekta ya viwanda kwa kuhisi ni kutupa mtaji na kushindwa kuzalisha (dead capital). Kumbuka kujenga au kufufua kiwanda kunahitaji mtaji mkubwa sana.
Ni ajabu kwamba Tanzania inatamba kuwa nchi ya kijamaa (kwa mujibu wa Katiba) lakini serikali yake haitaki kuwekeza kwenye viwanda na badala yake inategemea sekta binafsi ifanye. Sasa si tubadilishe katiba tujiite nchi ya kibepari tu. Nchi gani ya kijamaa inayotegemea mabepari wa sekta binafsi wajengee viwanda?
Wenzenu Kenya ni nchi ya kibepari lakini jukumu la kujenga na kufufua viwanda serikali inashiriki. Haijawaachia sekta binafsi peke yao. Sasa Tanzania yangu ya "kijamaa" lakini inategemea "mabepari" waisaidie kujenga viwanda. Hiki ni kichekesho kikubwa zaidi baada ya comedy za Mr.Bean.!
Maskini nchi yangu.!!
Malisa GJ.