Nani kasema Rushwa imeipungua Tanzania? tusidanganyane.

Rushwa haiwezi kwisha, juzi kuna daktari aligoma kutujazia kibali cha mazishi kwenye mojawapo ya hospital kubwa tu ya serikali hapa arusha na alikuwa anasema waziwazi kama hatutaki kumpa chochote hatajaza, ilibidi tumpe atakacho ndio akajaza na tukaruhusiwa kuchukua maiti, tumezika jana tanga

sent from my Sony Xperia using jamii forums mobile app
 
Tanesco nako hakupo nyuma, nilipia kila kinachohitaka lkn kuja kuniingizia umeme imekua shughuli, lkn tulivyofanya mazungumzo waliniletea Umeme jumapili yani adi utashangaa,
 
Rais Magufuli anastahili pongezi za dhati kwa uthubutu na hatua madhubuti anazochukua
 
Ila yatakiwa isiwepo, yawezekana nasi twafikiri hatuwezi kuishi bila rushwa! Yawezekana kuishi TZ bila rushwa, tusaidiane na wahusika tu..
 
Rushwa ni tabia.Huwa tabia hii sugu hustawi moyoni.Hustawishwa na kutokua na HOFU YA MUNGU.Kwa hiyo ni kama maradhi.Maradhi haya hayaondoki kwa sheria kali wsla vitisho.Maradhi huondoka pindi tu mtu mwenyewe akiweka nadhiri ya kubadilika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ili kukomesha hii rushwa ya barabarani serikali ingeweka utaratibu wa kupokea fine kwa installments kwa baadhi ya makosa, kwa mfano gari ime crack kioo au imekwajika rangi nk
Rangi kama imekwanjika sio kosa mkuu maana kinachoangaliwa ni namna gani hilo kosa linahatarisha maisha yako na ya watumiaji wengine wa barabara (inapokuja kwenye makosa yanayoendana na ubovu wa gari)
 
Wewe fuata utaratibu tu uone kama rushwa ipo...umekamatwa gari ina kosa ukalipishwa rushwa na wewe ukatoa (kosa la nani hapa kama sio wewe?usimlaumu polisi hata wewe mtoa rushwa pia humo kama una ujasiri si ukalipe faini yaishe, nitakubaliana na wewe na umebambikiwa kosa na kutengenezewa mazingira ya rushwa kutokana na kuwa maamumu wa sheria)...au uhamiaji umeambiwa process ya hati au jambo flani inachukua wiki mbili na wewe unataka ndani ya siku 4 (kosa la nani wewe ama wao maana kutokujiandaa kwako kumesababisha kujenga mazingira ya rushwa..suruhisho ni kwamba kama unajijua unataka kusafiri nje ya nchi anza mchakato mapema wa kuandaa safari yako ikiwemo pamoja na nyaraka za kusafiria)

Kuhusu NIDA...ukitoa rushwa umependa mwenyewe au wewe sio raia maana hakuna sehemu mtu amezuiwa kuhudumiwa kisa hana kitambulisho cha uraia au vinginevyo
 
Kazi zenyewe bila Rushwa hupati. ....hivyo kila mtu anajilipa mwenyewe ni hatari
 
Me naona huduma zote kama utafata utaratibu na vigezo unapata haki sababu usipopata au kucheleweshwa zipo mamlaka husika ushughulika ukiziona suala la rushwa ni pale mtu anatoa ili kuchepusha taratibu sababu huwezi toa hela bila kujua unatoa ya nini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom