MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,966
Nashangaa sana kwa wale wanaodai eti rushwa imekomeshwa Tanzania. Hususani kwenye idara za serikali,UHAMIAJI,NIDA na POLISI waanapokea rushwa wazi wazi ,kilichopo ni hofu tu kwa wafanyakazi wa umma na sio kwamba Rushwa imeisha au imepungua.
Kwa ujumla bado kuna tatizo kubwa sana kwenye idara nyingi za wizara ya mambo ya ndani. Kuna watu wanalalamika pake NIDA makao makuu kama vitambulisho vyako vina matatizo ukipitia mgongo wa nyuma mambo yanakwenda sawa, ila kama mfuko wako umetoboka basi utakaa foleni na kusugua miguu mpaka basi, Uhamiaji kule mambo yale yale passport yako au Viza ina shida kupitia mgongo wa nyuma ni fasta tuu, polisi barabarani kama mtu hana ile faini ya 30,000/= basi anatoa hata 10,000 isyoandikiwa kokote mambo yanasonga.
Utaratibu wa siku hizi ni mazungumzo tuu ndio wazi wazi lakini malipo ni M-PESA au Tigo pesa maisha yanaendelea.Kinachofanyika ni kupeana namba za simu kwa wahusika wawili wakati wa process basi baadae mambo yanasonga.
Rushwa ni ngumu sana, hakuna anayeweza kuisimamia ikaisha kabisa. Na hivi sasahivi watumishi wa umma nyongeza za mishahara hakuna, tutaona zaidi ya tulikotoka.