Nani kasema Maisha Bora kwa kila mtanzania hayapo!! Kazi kwenu

Arafat

JF-Expert Member
Nov 17, 2009
2,581
758
Jamani, nchni inaenda wapi? Petrol Bei bado ipo juu zaidi, Umeme bei juu na haupo, Kodi zote zimepanda ya Duka ndio husiseme, Kodi ya nyumba inazidi Mishahara, mchele na nyama bei yake ni zaidi robo ya mshahara wa kima cha chini, starehe sasa wanafanya RA, JK, Chenge na EL na watoto wao peke yao, Serikali inategemea bia kupata kodi wakati Quaran na Biblia hairuhusu kunywa pombe, Msikitini na Kanisani sadaka imepandishwa hawataki silver wanataka noti lasivyo watanamwita EL na RA kuzindua kanda na kufungua majendo ya ibada, mahari ndio husijaribu manaa wana hasira ya mwanao kufukuzwa shule kwa ajili ya ada,rate ya dola haishikiki, school fee utadhani unanunua majengo ya shule, Polisi wana uwa raia kama panzi sasa hii ni maisha bora kwa kila Mtanzania jamani au ni maisha bora kwa Kikwete na familia yake! Jamani huyu Bwana kashindwa kadorora kazeeka akili tuingie mtaani kudai nchni yetu imetekwa.
 
Arafat, haya unayoyasema kwenye post nyingine unawaponda wachangiaji wengine au msimamo wako huwa tofauti. Hii hali ndio inayozungumziwa kwa zaidi ya asilimia 70 ya michango humu jamvini!

Maneno yako 'tuingie mtaani...' ni kutoka moyoni au ni kwa ajili ya mada?
 
Tatizo wakipandisha mshahara tutabanana nao kwenye starehe nao wanataka wajinome lol
 
Wewe ni Msando Mheshimiwa spika au Msando yupi? au ni avatar tu! maneno na maada inajieleza Mkuu hii hali si sawa na si haki.
 
Tatizo wakipandisha mshahara tutabanana nao kwenye starehe nao wanataka wajinome lol

What do you mean Roza by these words "tutabanana nao......................wanataka wajinome" au ilimradi kuandika!
 
Maisha bora yapo nyie hamuyaoni au hamuishi tz nini? Acheni kumsema vibaya mkwere wa watu baba riz1
 
Maisha bora yapo nyie hamuyaoni au hamuishi tz nini? Acheni kumsema vibaya mkwere wa watu baba riz1

Hata Wazambia mmekodiwa kweli CCM haina watu sasa inatetewa na wazambia!!!!
 
Arafat, haya unayoyasema kwenye post nyingine unawaponda wachangiaji wengine au msimamo wako huwa tofauti. Hii hali ndio inayozungumziwa kwa zaidi ya asilimia 70 ya michango humu jamvini!

Maneno yako 'tuingie mtaani...' ni kutoka moyoni au ni kwa ajili ya mada?

Hata mimi nimeshangaa kidogo kwa mada ya Arafat leo. Kimetokea nini?
Au ndio kuna mtu amekuibia password yako?
Kama ni mwenyewe Arafat, uliwaza nini leo mpaka ukaandika post hii?
Hongera!
 
Hata mimi nimeshangaa kidogo kwa mada ya Arafat leo. Kimetokea nini?
Au ndio kuna mtu amekuibia password yako?
Kama ni mwenyewe Arafat, uliwaza nini leo mpaka ukaandika post hii?
Hongera!

Nonda kulikoni maana shida zimezidi tumekaa kijiweni hadi suluali zinaliwa na mchwa sasa umachinga ukifanya unakamatwa na Mgambo sijui kwanini wamachinga tuna kamatwa!
 
pdg mkwere nchi haiwezi kuongozwa na mtu aliyeweka starehe mbele kuliko maslahi ya taifa.
 
Back
Top Bottom