Mwanamke yeyote yule ni lazima uwe mrembo japo si kwa kujipaka yale mapoda mpaka tukusahau. Mwanamke hata kwa vitabu vya dini anasemwa ni pambo, sasa pambo likikaa hovyo hovyo utalitamani??
Hata ukiwa mzee jiweke vizuri, (tafadhali sizungumzii mkorogo wa kienyeji na ule wa madukani). Hata mzee kama Bi Kidude anastahili kupambwa. Mwanamke hata kama uko nyumbani hebu paka kale ka wanja kidogo, bana ua chana nywele vizuri, vaa vazi la heshima na tanashati, si mikanga kutwa nzima, nyonyo linacheza ndani ya nguo, akibisha hodi mgeni unakimbilia ndani!!!
Hata ukizeeka kale ka pedo kako ka heshima hebu vaa tu. Na wanaume ni vema wake waambie wawe mnavyotaka na ndoa itadumu. Kwa nini ukimbilie wa pedo na lipstik mitaani wakati wa kwako unaweza kumwambia unataka apake lipstik na pedo? Tena ikiwezekana nenda dukani ukamfanyie shopping ya vile vitu ambavyo unataka awe navyo na vinakufurahisha. Tuokoe na kuponya ndoa/mahusiano yetu, ni rahisi tu.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.