Nani kamziba mdomo Waziri wa Mambo ya Nje Mulamula, kulingana na kauli ya ahadi aliyotoa mwenyewe kuhusu uraia pacha?

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Nimesema siku zote huwa siwaamini wanasiasa. NI mara chache sana mwanasiasa ataongea kitu nimwamini, na siku zote wanasiasa wenyewe wananipa sababu za kusimama katika msimamo wangu wa kutowaamini. Generaly speaking, wanasiasa ni watu waongo.

Sasa leo sintasema mengi, bali nitwakumbusha tu alichosema Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mulamula, kuhusu uraia pacha. Sasa muamue wenyewe ikiwa ninakosea ninaposema wanasiasa mara nyingi ni watu waongo

Kwa kuwakumbusha tu:

Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amesema Serikali inalifanyia kazi suala la uraia pacha na kabla ya mwisho wa mwaka huu wa fedha, litakuwa limepatiwa ufumbuzi.

Mwelekeo mpya kwa uraia pacha
Balozi Mulamula alisema suala la diaspora kupiga kura linahitaji utaratibu na miundombinu, hasa kwa kutumia teknolojia kama zinavyofanya nchi nyingine zilizofanikiwa kwa kutumia mifumo ya kimtandao.
www.mwananchi.co.tz
www.mwananchi.co.tz

 
Na kwa wale wanaopenda kupinga uraia pacha bila kuwa na ufahamu kuhusu uraia pacha, maelezo yangu hapa chini yatawasaisdia sana

1. Tanzania ikiruhusu uraia pacha, ni kwa ajili ya Watanzania pekee?
Hapana. Unaporuhusu uraia pacha inakuwa ni kwa ajili ya Watanzania wanaotaka kuchukua uraia wa nchi nyingine, na watu wa nchi nyingine wanaotaka kuchukua uraia wa Tanzania. Ni lazima Tanzania na nchi hiyo nyingine zote ziwe zinaruhusu uraia pacha. Masharti na vigezo huzingatiwa na hutofautiana.

2. Inakuwaje hadi mtu anakuwa na uraia pacha?
Kimsingi, huombi kuwa raia pacha, bali unaomba uraia wa nchi ya pili, na kama ukikubaliwa ndio unakuwa raia pacha, kwa kuwa sasa utakuwa na uraia wa nchi zaidi ya moja.

Jambo la msingi ni kwamba sio rahisi mtu kupata uraia pacha. Mara nyingi, mtu anapewa uraia pacha ikiwa ameishi kihalali mfululizo katika nchi ya pili kwa muda usiopungua miaka mitano. Na nchi nyingine zitataka upitie kwanza hatua ya kuwa mkazi wa kudumu (permanent resident) kabla ya kuomba uraia na kuwa raia pacha. Kwa hiyo basi, mtu toka Kenya hawezi kuja Tanzania leo na kuomba uraia pacha, sio rahisi.

Hivyo ieleweke wazi kwamba wewe Mtanzania ambaye hujawahi hata siku moja kuishi South Africa, huwezi kuondoka Tanzania leo hii kwenda bondeni ukaombe uraia ili uwe raia pacha. Vivyo hivyo mtu wa South Africa ambaye hajawahi kuishi Tanzania, hawezi kuja Tanzania leo ili apewe uraia wa Tanzania na kuwa raia pacha.

3. Nini hasa baadhi ya vigezo vya msingi vya kuwa raia pacha?
Inategemea nchi inaweka vigezo gani kwa raia wa nchi nyingine kuomba uraia pacha. Sharti kubwa la nchi nyingi ni kwamba usiwe na rekodi ya uhalifu (criminal record) ya nchi uliyotoka au nchi unayoishi na unaomba uraia, na uwe umeishi kwa muda fulani katika nchi unayoomba uraia ili uwe raia pacha. Nchi nyingine hata zinaweka sharti la kwamba lazima uongee lugha ya nchi , kama hapa kwetu Kiswahili, ili uwe raia wao.

Kama nilivyosema katika swali la kwanza, kigezo cha kawaida ni kuwa umeishi kihalali (sio kuzamia) katika nchi nyingine kwa zaidi ya miaka mitano. Sasa kuna nchi nyingine, ikiwa umeoa au kuoelewa na raia wa nchi hiyo basi unapata uraia wa nchi ya mume/mke wako na kuwa raia wa nchi hiyo, hivyo kuwa raia pacha. Sasa kuna baadhi ya nchi ziliona hili lilitumika vibaya, watu walioa au kuoelwa ili tu kupata uraia. Hivyo walibadilisha huu utaratibu na kusema lazima uishi katika ndoa, na kuthibitisha unaishi na mumeo/mkeo kwa angalau miaka 3 kabla ya kuomba uraia.

Kwa hiyo kila nchi inakuwa na vigezo vyake, na Tanzania tukiamua kuruhusu uraia pacha lazima tutaweka vigezo vyetu. Hatuwezi kutoa uraia kama sadaka ili watu wawe raia pacha.

4. Kuna watu wanakuwa na uraia pacha wa kununua?
Ndio, zipo nchi zinauza uraia. Kwa mfano, kuna nchi zinaweza kusema ukiingiza katika nchi hizo mtaji kuanzia Dola 250,000 basi una haki ya kupewa uraia. Kwa hivyo nchi kama hizo zitasemwa zinauza uraia. Tanzania hatulazimishwi na mtu yeyote kuuza uraia wa Tanzania, kwa hiyo tunaweza kuruhusu watu wa nje kuwa na uraia wa Tanzania bila kuwa na kigezo cha kununua uraia wa Tanzania

5. Je, Tanzania tunaweza kuwawekea Watanzania masharti ya kuwa na uraia pacha na nchi nyingine?
Sio rahisi, kwa sababu ni sawa na kusema tutaziwekea hizo nchi masharti ya wao kumpa Mtanzania uraia wa nchi hizo. Ila sasa, Tanzania tunaweza kuweka masharti kwa Watanzania walio na uraia pacha ili kulinda vitu kama usalama wa nchi yetu, nk

6. Je uraia pacha hauwezi kutuletea athari za usalama wa Tanzania?
Hii ni hoja potofu na imetumika vibaya na watu wengi. Ili mtu kusababisha athari za usalama wa nchi yetu sio lazima awe raia pacha. Na pia kama kuna maeneo ambayo tunaona uraia pacha unaweza kuhatarisha usalama wa Tanzania basi tutawawekea watu wenye uraia pacha masharti fulani ili kuzuia hilo. Kwa mfano, tunaweza kusema Mtanzania mwenye uraia pacha haruhusiwi kugombea nafasi za kisiasa kama ubunge na uraisi, au kutumika katika vyombo vya usalama kama JW, Polisi, na TISS.

7. Uraia pacha unakuwaje na manufaa za kiuchumi kwa Tanzania?
Hili ni swali la msingi sana. Jambo la kukumbuka ni kwamba unapokuwa wa nchi ya kigeni, kunakuwa na masharti yanayokuzuia kufanya mambo fulani katika nchi nyingine. Kwa mfano, si rahisi kwa Mtanzania kutuma fedha za kigeni kwenda nchi nyingine, na ndivyo isivyo rahisi kwa mtu aliye Mtanzanaia katika nchi ya nje kutuma fedha za kigeni Tanzania. Sasa unapokuwa unaishi nchi ya kigeni na una uraia wa Tanzania, moja kwa moja unakuwa na kitu tunaita haki ya kutuma faida kwenye nchi yako (repatriation of profits) bila masharti magumu. Na kumbuka kwamba, kwa upande wa Tanzania, unakuwa na urahisi wa kuwekeza ukiwa na uhakika kwamba investments zako Tanzania ziko salama kwa kuwa unalindwa kwa haki za kuwa raia. Mtu kama Aliko wa Dangote huwezi kumlinganisha katika uhuru wa investments zake kama alionao MO kwa kuwa MO kama raia wa Tanzania ana wigo mwepesi na mpana zaidi wa kufanya biashara Tanzania kuliko Dangote.

Kwa hiyo Watanzania waliochukua uraia wa nje watajisikia huru zaidi kuhamisha mitaji yao kuja Tanzania wakijua kwamba wanahamishia mitaji Tanzania kama raia wa Tanzania bila kuhofu kubadilika kwa upepo wa kisiasa au hata kutaifishwa mali zao

Lakini zaidi, raia wa nje wenye uraia pacha na Tanzania wanakuwa na uhuru zaidi wa kuwekeza Tanzania ikiwa watakuwa na uraia wa Tanzania. Itakuwa rahisi sana na kutompa hofu yoyote Dangote kuhamishia mtaji mkubwa Tanzania akijua anafanya hivyo kama raia wa Tanzania

8. Vipi ikiwa nchi ya nje ambayo una uraia pacha nayo inataka uihujumu Tanzania, sio rahisi hilo kufanyika kama raia pacha?
Suala la nchi uliyonayo kukutaka uihujumu nchi yako ya kuzaliwa ni suala la uhalifu kama uhalifu mwinginme wowote wa kimataifa, na linaweza kufanywa na mtu yeyote hata asiye na uraia pacha. Nikiukana uraia uraia wa Tanzania na kuchukua tuseme uraia wa Burundi, kama Burundi watataka kunituma kuihujumu Tanzania sio lazima niwe raia pacha. Bado wanaweza kunituma kufanya hujuma hata bila kuwa na uraia pacha. Na kimsingi, ni rahisi mie kukataa kuja kuihujumu Tanzania nikiwa na uraia pacha kuliko kama niliukana uraia wa Tanzania kwa kushurutishwa ili nipate uraia wa Burundi. Sababu unakuwa umenilazimisha niukane uraia wa nchi yangu wakati bado naipenda lakini kuna fursa nazitaka na ili nizipate inabidi nichukue uraia wa nchi nyingine. Kwa hiyo unanijengea chuki dhidi ya nchi yangu ambayo wewe kama kiongozi unanikatalia haki ya kuishi, na nitakuwa na hasira na wewe. Kwa hiyo ni hoja poofu kuhusianisha uraia pacha na watu kuihujumu nchi yao ya kuzaliwa, ni bora umruhusu mtu kuendelea kuwa raia ili mapaenzi na nchi yake yaendelee kuwapo hata kama amechukua uraia wa nchi nyingine.

9. Je uraia pacha hauathiri uzalendo wako kwa nchi yako ya kuzaliwa?
Kwanza nini hasa maana ya mzalendo, na uzalendo au kutokuwa mzalendo kunathibitishwa na matendo gani? Je ndio tuseme mtu akiwa na uraia pacha na anaishi Tanzania atakuwa fisadi, mwizi, mhujumu uchumi, mvivu na mtoro kazini kuliko yule Mtanzania asie na uraia pacha? Hii pia ni hoja potofu inayotumiwa vibaya na watu wengi. Wengi watakubali kwamba Tanzania kwa sasa inapigika sana, watu wanafuja fedha za serikali na wanafisadi sana nchi hii. Sasa ndio tuseme watu wanaofanya haya ni raia pacha? Jambo moja la kuelewa ni kwamba, ni raisi kwa mtu asiye na uraia pacha kufanya ufisadi katika nchi yake kuliko yule aliye na uraia pacha.

10. Vipi raia pacha akifanya uhalifu na kukimbilia nchi nyingine aliko na uraia wa pili?
Dunia ya sasa ni kama kijiji. Unapofanya uhalifu wa aina yeyote ukiwa raia pacha, usidhani kwamba kukimbilia nchi nchingine kutakuokoa. Kumbuka katika masuala ya uhalifu kuna Interpol, polisi ya kimataifa, ambayo ni rahisi Tanzania kuitumia na wewe kukamatwa hata ukiwa umekimbilia nchi nyinge. Ukiiba gari Tanzania ukakimbilia USA ambako una uraia pacha, usidhani kwamba utapona. Na kumbuka kwamba, nchi nyingi zinaruhusu uchukue uraia wao kwa masharti ya kutokuwa na rekodi ya kihalifu (criminal record). Kwa hiyo sidhani kwamba utafanya ubakaji Tanzania ukimbilie USA na kuwa salama. USA watatengua uraia wako wa USA na utarudishwa Tanzania kwa nguvu (deportation) kwa sababu tayari umekiuka mashart ya kutokuwa na criminal record. Dunia ni kijiji siku hizi.

11. Je ukiwa uraia pacha, Tanzania inaweza kuutengua?
Inawezekana. Kama vile tu USA wanaweza kuutengua uraia wa Mtanzania kule USA kwa sababu ya makosa ya jinai, ndivyo Tanzania tunavyoweza kutengua uraia wa Tanzania wa Mchina ambaye anafanya makosa au uhalifu akiwa anaishi hapa Tanzania kama raia pacha. Ila sidhani kama haki za binadamu zinaruhusi kutengua uraia wa asili wa mtu na kumfanya stateless.

12. Je kuna Watanzania wenye uraia pacha kwa sasa?
Sio rahisi, hasa ikiwa waliupata uraia wa nchi nyingine ukubwani. Mara nyingi ili uwe raia wa nchi nyingine, lazima nchi hiyo ipeleke taarifa za ombi lako la uraia kwenye ubalozi wa nchi yako. Tanzania wanapopata ombi hilo basi wataubatilisha uraia wako wa Tanzania. Kuna nchi mtu unakuwa raia kwa kuzaliwa katika nchi hiyo. Ndio maana Tanzania kwa watu waliozaliwa nje, wenye birth certificate za nje, lazima uthibitishe uraia wako wa Tanzania ukifikisha miaka 18. Hiki ndicho tumesikia katika nyanja za siasa kwamba fulani sio faia wa Tanzania. Hii ni mara nyingi kwa wale waliozaliwa nje ya Tanzania.

Na suala la kuthibitisha uraia linakuja kwa kuwa kuna nchi zinakupa uraia ukizaliwa kwenye hizo nchi, hata kama wazazi wako sio raia. Kimsingi, watoto wanaozaliwa nje ya Tanzania wapo ambao ni kama wana uraia pacha ikiwa nchi walikozaliwa iliwapa uraia kwa msingi wa kuzaliwa huko. Ndio maana wakifikisha miaka 18 Tanzania inataka wathibitishe uraia wao wa Tanzania au waende nchi walikozaliwa ambako wanaweza kutambuliwa kama raia. Unaweza usithibitishe uraia, lakini huenda siku moja ukakwama pale itakapoonekama una birth certificate ya nje na hukuthibitisha uraia wako wa Tanzania ulipofika miaka 18. Ndio utasikia fulani hana sifa za kugombea ubunge kwa kuwa sio Mtanzania ingawa wazazi wake wote unakuta ni Watanzania.

13. Nini tofauti ya ukazi wa kudumu (permanent residency) na uraia pacha?
Ukazi wa kudumu ni kwamba wewe unakuwa mkazi wa nchi fulani, na unaruhusiwa kufanya kila kitu kama vile tu raia isipokuwa baadhi ya vitu hasa kugombea nafasi za kisiasa, kupiga kura na nchi nyinge huruhusiwi kumiliki ardhi.

Huruhusiwi kujihusisha na siasa. Huhitaji visa kuingia hiyo nchi, na unaruhusiwa hata kufanya kazi bila kibali cha kazi (work permit) na hata kufanya kazi serikalini. Na ukazi wa kudumu unaweza kuupoteza ikiwa hutaishi katika nchi ya ukazi wako wa kudumu kwa kipindi cha muda fulani. Kwa hiyo ukazi wa kudumu huwezi kabisa kuulinganisha na uraia pacha. Uraia pacha unakupa uhuru zaidi na hauna kikomo wala masharti ya kuendelea kukaa katika nchi muda wote.

14. Vipi kwa walioukana uraia wa Tanzania na sasa ni raia wa nchi nyingine, wanaweza kupata uraia pacha?
Hili ni jambo gumu kidogo, na litahitaji ufikirio maalum wa kibinadamu (special consideration on humanitarian grounds) wa serikali. Uraia pacha si kwa ajili ya raia wa Tanzania ambaye aliukana uraia wa Tanzania na sasa anaishi nje ya Tanzania kama raia wa nchi nyingine. Ikiwa Mtanzania alishaukana uraia wa Tanzania na sasa anaishi nje ya Tanzania, kimisingi, ili aweze kuwa raia pacha inabidi aombe uraia wa Tanzania upya kama mtu mwingine tu ambae sio raia wa Tanzania. Huenda kwanza arudi Tanzania, na labda aishi kwa kibali (residence/permanent permit) nchini kwa muda usiopungua miaka mitano, na ndio ataomba tena kuwa raia wa Tanzania na kumfanya awe raia pacha - ikiwa nchi ambayo ni raia wake kwa sasa inamruhusu kuwa raia pacha, na Tanzania itakubali kumpa tena uraia. Sasa ndio maana nimesema serikali inaweza kutoa ufikirio, kwa sababu kimsingi huyu mtu ni mzaliwa wa Tanzania, na hivyo wakasema hawa watarudishiwa uraia wa Tanzania kwa msingi wa kuzaliwa Tanzania ili wawe raia pacha na nchi ambayo wana uraia kwa sasa.

15. Hadi sasa, ni nchi ngapi katika Afrika zinaruhusu uraia pacha?
Ni rahisi zaidi kuongelea ni nchi ngapi katika Afrika haziruhusu uraia pacha kuliko ni ngapi zinaruhusu uraia pacha, kwa kuwa karibu nchi zote za Afika sasa zinaruhusu uraia pacha isipokuwa Tanzania, Ethiopia, Eritrea, DRC, Malawi, Zambia, Liberia, Lesotho, Sao Tome na Cameroon, kama ramani hapa chini inavyoonyesha.

1628326239668.png



Maswali mengine yanakaribishwa japo nahisi vipengele nilivyoweka vinajitosheleza
 
Nimesema siku zote huwa siwaamini wanasiasa. NI mara chache sana mwanasiasa ataongea kit nimwamini, na siku zote wanasiasa wenyewe wananipa sababu za kusimama katika msimamo wangu wa kutowaamini. Generaly speaking, wanasiasa ni watu waongo.

Sasa leo sintasema mengi, bali nitwakumbusha tu alichosema Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mulamula, kuhusu uraia pacha. Sasa muamue wenyewe ikiwa ninakosea ninaposema wanasiasa mara nyingi ni watu waongo

Kwa kuwakumbusha tu:


Mwelekeo mpya kwa uraia pacha

Balozi Mulamula alisema suala la diaspora kupiga kura linahitaji utaratibu na miundombinu, hasa kwa kutumia teknolojia kama zinavyofanya nchi nyingine zilizofanikiwa kwa kutumia mifumo ya kimtandao.
www.mwananchi.co.tz
www.mwananchi.co.tz

Kwani kwa maneno hayo ya Mulamula, wewe unafikiri alitoa ahadi gani?
 
CCM hawapendi maendeleo ya watu wake ,nchi ambayo inakataa uraia wa watu wake inataka watu milioni 80 wawe maskini wa kutupwa
 
Naona sasa wameacha wimbo wa uraia pacha wanaimba hadhi maalum

Siku mbayo Tanzania itakubali uraia pacha ni pale ambapo raisi aliyeko madarakani atakuwa na watoto wanaotaka uraia pacha
 
Ahadi ya kufanyia kazi suala la uraia pacha
Tatizo lenu Watanzania wengi mna utamaduni wa kuwa vague. Ndiyo maana hata viongozi wenu wanatoatoa tu ahadi ambazo haziwawajibishi. Ahadi ambazo hazipo well defined kiongozi anatoa kirahisi halafu hata kumbana huwezi.

Sasa ukiahidiwa kufanyia kazi suala la uraia pacha umeahidiwa nini?

Hapo kuna kitu gani concrete?

Kufanyia kazi maana yake nini?

Mtu akiandika mambo na kupendekeza na kuachia wakubwa zake waamue amefanyia kazi au hajafanyia kazi suala?

Kuna metrics gani za kufuatilia?

Kuna timeline gani ya kufuatilia?

Kuna accountability tree gani ya kuiangalia?
 
Ahadi ya kufanyia kazi suala la uraia pacha
Actually suala la uraia pacha liliamuliwa na kukubaliwa na Bunge wakati wa Kikwete. Sasa tatizo likawa kwamba Kikwete akasema badala ya kutia shihi sheria ya uraia pacha, kwa nini lisiingizwe kwenye Katiba Mpya ili liwe chini ya Katiba badala ya kuwa chini ya sheria tu?

Hapo ndipo kosa lilifanyika, maana hata kina Tom na Jerry wasiojua maana ya uraia pacha, na kina Dick wenye kuonea wivu watu watakaokuwa raia pacha, wakapata fursa ya kuleta ubishi usio na maana
 
Actually suala la uraia pacha liliamuliwa na kukubaliwa na Bunge wakati wa Kikwete. Sasa tatizo likawa kwamba Kikwete akasema badala ya kutia shihi sheria ya uraia pacha, kwa nini lisiingizwe kwenye Katiba Mpya ili liwe chini ya Katiba badala ya kuwa chini ya sheria tu?

Hapo ndipo kosa lilifanyika, maana hata kina Tom na Jerry wasiojua maana ya uraia pacha, na kina Dick wenye kuonea wivu watu watakaokuwa raia pacha, wakapata fursa ya kuleta ubishi usio na maana
Mkapa alisema no to uraia pacha, over my dead body.

Sasa kafariki labda ndiyo kuna nafasi.

Ila, alijiapiza kwenye uhai wake Tanzania haiwezi kuwa na uraia pacha, labda special status.

Na mpaka anafariki alifanikiwa.

This is a political thing, viongozi wa CCM wanaogopa diaspora watakuja kisiasa.
 
Tatizo lenu Watanzania wengi mna utamaduni wa kuwa vague. Ndiyo maana hata viongozi wenu wanatoatoa tu ahadi ambazo haziwawajibishi. Ahadi ambazo hazipo well defined kiongozi anatoa kirahisi halafu hata kumbana huwezi.

Sasa ukiahidiwa kufanyia kazi suala la uraia pacha umeahidiwa nini?

Hapo kuna kitu gani concrete?

Kufanyia kazi maana yake nini?

Mtu akiandika mambo na kupendekeza na kuachia wakubwa zake waamue amefanyia kazi au hajafanyia kazi suala?

Kuna metrics gani za kufuatilia?

Kuna timeline gani ya kufuatilia?

Kuna accountability tree gani ya kuiangalia?
Pata context yote ya aliyosema sio kubwabwaja bila kujua kauli hiyo ilitia mambo gani. Wewe ukipapasa sehemu ina nywele basi unachukulia ni kichwa ? Haya ndio alisema;

1665066882373.png
1665067452125.png
 
Pata context yote ya aliyosema sio kubwabwaja bila kujua kauli hiyo ilitia mambo gani. Wewe ukipapasa sehemu ina nywele basi unachukulia ni kichwa ? Haya ndio alisema;

View attachment 2378943View attachment 2378947
Sasa hapo kuna context gani ya ziada?

Kuna kipi cha zaidi hapo?

Unajuaje sina context wakati alivyokuja Marekani nilikuwepo kwenye kikao na nikaona alivyokuwa vague akichekacheka mwanzo mwisho?

Unataka kuniambia serikali hii ya CCM ikitaka uraia pacha wabunge watashindwa kupitisha sheria?

Are you really falling for this bullshit unayoita context?
 
Back
Top Bottom