..jamani hii habari ndiyo imenithibitishia kwamba Raisi wetu hayuko serious hata kidogo.
..Raisi anakabidhiwa ripoti ya suala zito kama madini halafu anatumbukia kwenye stori za MPIRA.
..hii ripoti ilishamfikia Raisi kwa hiyo ungetegemea huo ungekuwa muda mzuri wa kuuliza na kuijadili kwa kina ripoti akiwa na wajumbe.
..kwa kweli Kikwete tutamkumbuka kwa SAFARI na MPIRA WA MIGUU.
..Prof.Lipumba hakukosea kwamba Kikwete angefaa sana kuwa Waziri wa Michezo.

Kikwete aipa tano SBL
na Salehe Mohamed
RAIS Jakaya Kikwete, ameipongeza Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kwa misaada yake kwa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) ambayo kwa kiasi kikubwa imesaidia kufanya vizuri kwa timu hiyo katika michuano mbalimbali.
Pongezi hizo alizitoa jana Ikulu jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa SBL, Jaji Mark Bomani, mara baada ya kumkabidhi taarifa ya mapitio ya mikataba ya madini.
Alisema kutokana na kazi nzuri hiyo ya SBL anatarajia kukutana nao kuwapongeza wao na timu ya taifa, kwa mafanikio waliyoyafikia kiasi cha kuanza kuleta heshima kwa Tanzania katika medani ya soka.
"Nawapongeza sana Serengeti kwa kuwasaidia vijana wetu wa Taifa Stars, ambao hivi sasa wameanza kufanya vizuri katika michezo yao na mimi nafanya utaratibu wa kuonana nanyi wote ili kuwapongeza," alisema Kikwete.
Alisema hivi sasa yeye na Watanzania wengine wameanza kutembea kifua mbele kutokana na vijana wanaosakata soka kufanya vizuri ndani na nje ya nchi.