Nani kaliiba fagio la chuma? Arejeshe Tafadhari..

Duduwasha

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
5,703
3,653
Dah! Nimelikumbuka Fagio la chuma, ambalo lilikuwa linafagia kila uozo serikalini yaani adabu na heshima ilikuwepo likipita. lilikuwa linawafagia hadi mabwana afya waliozembea na kuanza kupotea kwenye mitaa yetu, yaani walikuwa wanapita majumbani mwetu hadi tukawazoea ila sikuhizi siwaoni, lilifagia wala rushwa wazembe yaani maadili ikarea kwenye mistari lakini huyo aliyeliiba au kulistopisha tu hilo FAGIO LA CHUMA Basi uzembe ukarejea ufisadi uhujumu uchumi viwanda viaanza kufa uchafu ukaongezeka ndio maana uchafu kimekuwa kamakitu cha kawaida nchini mwetu wasaidizi wa j.k watakao soma hapa wampelekee kilaza wetu anaweza waona wa maana akawaongezea na mishahara kabisa. aliyeiba FAGIO LA CHUMA ALIREJESHE. Ni ombi.
 
Fagio la Chuma inavyoonekana liliibiwa na EL na kufichwa na RA. Mwenye ubavu wa kulifuata kwa watu hao simuoni ndani ya CCM, hata kilaza mwenyewe ameonyesha kutokuwa na uwezo huo wa kulirejesha au kuwakamata mwizi na aliyelificha. Habari ndo hiyo.
 
Ahaa ndo lile alilokabidhiwa mzee ruksa enzi zilee?Kama ndilo basi tuliyemkabidhi ndo aliridhia kuliuza kama chuma chakavu kule zenji.
 
Mikingamo ndio Sauti ya Uma na Fagio la Chuma Ndio Lifaialo Uozo kama Huu Uendeleao Nchini
 
umenikumbusha wimbo mzuri wa enzi hizo " usipowajibika ole wako utakumbwa na fagio la chuma * 2" nilikuwa bwana mdogo sana wakati huo sikumbuki bendi gani iliimba huu wimbo. dah watu wameliiba kweli hili fagio la chuma halitajwi tena kwa sasa
 
Tena Riz1 Hataki kabisa kusikia hiki kitu haha Huo Wimbo hata mie Sikumbuki aliuimba Nai ila ulikuwa Poa Sana
 
Duh long time. Nakumbuka wimbo wa kwaya ya shule yetu hukoo Ruangwa Lindi tuliimba hv:
Mwinyi ameshakamata.....lile ....fagio la chuma....ole ..ole wao wote ..wale walanguzi wote...wale watoro kazini...wale wazembe....mwinyi ameshakamata lile fagio la chuma laku... Lakuwafagia ...wale viongozi sugu!! Duh e bwana ehe
 
umenikumbusha wimbo mzuri wa enzi hizo " usipowajibika ole wako utakumbwa na fagio la chuma * 2" nilikuwa bwana mdogo sana wakati huo sikumbuki bendi gani iliimba huu wimbo. dah watu wameliiba kweli hili fagio la chuma halitajwi tena kwa sasa

Mkuu ilikuwa mkusanyiko wa waimbaji wakatunga na kuimba huo wimbo ili kuhanikiza uwajibikaji serikalini. Baada ya mzee mwinyi kukabidhiwa fagio akaja mtu anaitwa waziri wa mambo ya ndani na naibu waziri mkui: ukichelewa tu ofisini unakuta kitu chako hakiposasa utajua mwenyewe ukae chini ama ukakikomboe kwa kikombozi. Ukifanya kosa mtwara unaambiwa ukamuone mzee Kolalacha basi ikawa ni mchafukoge tu. Nadhani fagio aliondoka nalo Lyatonga manaks alijaribu kufagia pale airport akakumbana na moto hadi ufagio ukayeyuka nadhani!
 
...lilipitiwa na moto likayeyuka.
Tutafute maji tuuzime, unaunguza taifa zima sasa.
Watu hawawajibiki hata kwa maisha yao binafsi.
 
Hivi hilo Fagio likirejeshwa kuna kiongozi kwenye hii serikali litamkosa?
 
umenikumbusha wimbo mzuri wa enzi hizo " usipowajibika ole wako utakumbwa na fagio la chuma * 2" nilikuwa bwana mdogo sana wakati huo sikumbuki bendi gani iliimba huu wimbo. dah watu wameliiba kweli hili fagio la chuma halitajwi tena kwa sasa

Uliimbwa na Juma Ubao.

Back
Top Bottom